Hayo ya mkandarasi hayawahusu DART watafute wazee wa 10% ndio wahusikaHatutaki mkandarasi anayejenga mwendo kasi ya mbagala aje kujenga ya Tegeta, kwa sababu sipendezwi na spidi yake. Ni hilo tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo ya mkandarasi hayawahusu DART watafute wazee wa 10% ndio wahusikaHatutaki mkandarasi anayejenga mwendo kasi ya mbagala aje kujenga ya Tegeta, kwa sababu sipendezwi na spidi yake. Ni hilo tu.
Hawa wanaoogopa hata watu kupiga picha kwenye vituo vyao wana ubavu kweli?Itafika point mtawekwa uchi kwa utendaji wenu mmbovu, mmejiaandaje?
Sio kweli huwa wanakatisha kwenye saa nne hivi na wanarudisha huduma saa tisa na nusu, na kwakweli mimi naamua kuwatetea muda huo abiria wa moja kwa moja ni wachache sana, ni bora wapande gari mbili tuNaomba ufafanuzi hua sielewi kwanini mnakatisha ruti ya mbezi kutoka gerezani au kivukoni sa 2 : 30 ilihali abilia ni wengi ila mnataka afike kimara achukue gari nyingine. Hii inafanya mnapoteza fedha kwa sababu kuna baadhi akifika kimara kachoka kusubiri gari zenu mpaka zijae tena anahisi uvivu anaamua kwenda kupanda bajaji n'je kwanini kusiwepo na gari mpaka sa 4 : 30 angalau abiria wanaweza kua wamepungua kuliko kukatisha ruti ilhali bado kuna abira wengi.
Najua tutatangaziwa ila mimi nlikuwa nataka tu kujua kwa makadirio yenu nyinyi mnadhani ni lini au mwezi gani mtakuwa mmekailisha ujenzi na kuanza rootKwa sasa kazi zinaendelea kukamilishwa ikiwemo kumalizia ujenzi wa vituo vya kupandia na kushuklia abiria na kazi nyingine ndogo ndogo, muda ukifika wananchi watatangaziwa.
wewe ndio ujuelewi tiketi ya combo tu kutoka mbezi hadi gerezan ni 750+500 unalipa 1250 ndio utoke kibaha hadi gerezani kwa 750 labda ungesema unalipa tiketi mbili ya 700 kutoka kibaha hadi kimara na pia unalipa 750 kutoka kimara hadi gerezani jumla 1450 halfu iyo ya 750 unakuja kuchaniwa kimara ndio ningekuelewa lkn sio kibaha to gerezani kwa 750Ndio ilivyo unalipa 750/- pale Kibaha na tiketi haichanwi unakuja kimara unaendelea na safari ama kwenda gerezani au kivukoni!!! Swali kwani huwezi safiri kwa bei hiyo kutoka kivukoni/gerezani kwenda kibaha? Fanya utafiti kabla ya kuropoka!!!
Tunashukuru kwa ushauri wako tutaendelea kusimamia jambo hili kwa umakini zaidi , aidha zipo jitihada za kuhakikisha idadi ya mabasi inaongezeka tunawaomba mvute subra wakati huu serikali yenu ikipambana kuhakikisha kila jambo linakuwa sawa ikiwemo hili la kuongeza idadi ya Mabasi.Jaribuni kusimamia foleni za kupanda kwenye magari, hasa vituo vya mwanzo wa safari.
Vilevile kuongeza idadi ya magari hasa peak hours.
Tunashukuru kwa pongezi japo huduma bado haijafika katika viwango stahiki, tunaendelea na jitihada za kuongeza idadi Mabasi ama kwa hakika muda sio mrefu mambo yatabadilika kabisa.Nilikuwepo Dar tangu tarehe 24-28 may 2023 nilifikia Kimara Suka na nilikuwa nahudhuria mkutano pale Diamond Jubilee! Kwa karibu 95% ya safari zangu nilikuwa natumia usafiri wa wa UDAR! Kwakweli nashukuru safari zangu zote nilipata huduma nzuri! Hongereni mnajitahidi!
Mimi na watu wote wanasafiri hivyo. Pale kibaha kuna tiketi ya 750/- haichanwi pale inakuja kuchanwa Kimara! Mimi nimesafiri hivyo na ndio sbb ya mshangao niliouelezea!!!wewe ndio ujuelewi tiketi ya combo tu kutoka mbezi hadi gerezan ni 750+500 unalipa 1250 ndio utoke kibaha hadi gerezani kwa 750 labda ungesema unalipa tiketi mbili ya 700 kutoka kibaha hadi kimara na pia unalipa 750 kutoka kimara hadi gerezani jumla 1450 halfu iyo ya 750 unakuja kuchaniwa kimara ndio ningekuelewa lkn sio kibaha to gerezani kwa 750
Wewe Kweli unatoka hood MOYA na Mimi.....Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
There is any information kuhusu kuanza Kwa huduma ya mwendokasi mbagala route??Tunashukuru kwa pongezi japo huduma bado haijafika katika viwango stahiki, tunaendelea na jitihada za kuongeza idadi Mabasi ama kwa hakika muda sio mrefu mambo yatabadilika kabisa.
Nami nimeondoka rasmi mwaka 2000, na skuizi pamebaki kama njia tu pamoja na kwenda kuwaslimia wazazi.Wewe Kweli unatoka hood MOYA na Mimi.....
Nimetoka huko kitambo sanaa 😊😊😊
Way back 🔙
Yaah Mimi pia japo miaka Saba sijawai kanyaga ardhi ya mwanzaNami nimeondoka rasmi mwaka 2000, na skuizi pamebaki kama njia tu pamoja na kwenda kuwaslimia wazazi.
But Mwanza inajengeka kwa kasi sana....
Huduma either imewashinda au mnafanya kwa mipangilio yenu wenyewe.View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.
Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku
Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania
Barua pepe: info@dart.go.tz.
#usafiri wa umma nadhifu
#mwendokasi app