DART yaingia mkataba wa miaka 12 na Emirates National Group kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umeingia mkataba wa miaka 12 na kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam.

Pia soma > Serikali imekuchukua mkopo NMB ili kumnunulia mabasi mwekezaji wa Mwendokasi. Mkopo utalipwa na Serikali kwa kodi za umma

Mkataba huo ulisainiwa rasmi Ijumaa, ukiashiria hatua muhimu katika jitihada za serikali kuboresha huduma za usafiri wa umma katika jiji la kibiashara.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dk. Athumani Kihamia, ENG itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177 yatakayoongeza ufanisi na upatikanaji wa huduma jijini.

Mchakato huo ulianza mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi. Mnamo 2020, serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, na ENG ikaibuka mshindi.

Hatimaye, mchakato huo sasa umekamilika kwa kutiwa saini kwa mkataba rasmi wa utekelezaji.
 
Unakuta ni mkataba wa mtu fulani mkubwa serikalini ila ameamua tu kupiga dili kupitia kampuni ya nje. Kama kweli hakuna wataalam wa kuendesha mradi wa DART basi hata ikulu itafutiwe mwekezaji wa kimataifa aiendeshe.
 
Barabara ya mbagala inazidi kuchakaa.

Hii nchi sisiem sijui wameijambia mavi Gani asee!
PXL_20250327_051025935.jpg
 
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umeingia mkataba wa miaka 12 na kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam.

Pia soma > Serikali imekuchukua mkopo NMB ili kumnunulia mabasi mwekezaji wa Mwendokasi. Mkopo utalipwa na Serikali kwa kodi za umma

Mkataba huo ulisainiwa rasmi Ijumaa, ukiashiria hatua muhimu katika jitihada za serikali kuboresha huduma za usafiri wa umma katika jiji la kibiashara.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dk. Athumani Kihamia, ENG itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177 yatakayoongeza ufanisi na upatikanaji wa huduma jijini.

Mchakato huo ulianza mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi. Mnamo 2020, serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, na ENG ikaibuka mshindi.

Hatimaye, mchakato huo sasa umekamilika kwa kutiwa saini kwa mkataba rasmi wa utekelezaji.
Hili ninaliunga mkono. Watanzania hawa walioshindwa ku print hata Tshirts za CCM ndiyo wakaendeshe mradi wa Mabasi yaendayo kasi?
Achilia mbali mradi mzima, madereva tu kuyaendesha kama mabasi yanawashinda
 
Back
Top Bottom