DART yaingia mkataba wa miaka 12 na Emirates National Group kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam

DART yaingia mkataba wa miaka 12 na Emirates National Group kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam

Tanzania nzima hakuna kabisa mwenye uwezo wa kuendesha mradi huu hadi tulete wageni?
 
CCM ndiyo iliyoshindwa,Usiseme tumeshindwa acheni Chadema waongoze inchi
Shida unaongea uchama tu muda wote, sisi tunasema watanzania... kwani biashara ngapi za watanzania Baba akifa tu na biashara nayo imekufa..? Watoto wanakuwa masikini wa kutupwa??? Shida ni sisi hata ikiingia CDM kwa kuwa shida ni sisi hali itakuwa ni ile ile....
 
Lengo ni kuwa na ufanisi katika kutoa huduma, sasa kama wenyeji wameshindwa kwa nini tusitumie wageni. Maana wenyeji wanazidi kututia hasara tu kmmmk
 
Ipo miradi ambayo inahitaji kuendeshwa na watu wenye mitaji na ziada, miradi kama hii kapuku ikiingangania ni lazima ikutoe roho mzima mzima, jambo la ubia si jambo baya, alimradi uwe ubia wa kugawana kipato kwa ukweli na haki.

Kuendesha BRT kuna ugumu gani?..
Kama kila agency ya Serikali inashindwa kazi iliyopewa maana yake ni nini sasa.

Unataka kuniambia shida ni Serikali au hawa watendaji? Kwanini tusiamini tatizo linaanzia top office kushindwa kuweka na kusimamia standards..

Kweli Tanzania tumeshindwa kuendesha BRT, unahitaji mtaji kiasi gani kurun hiyo BRT..?..

Ok GOT imeshindwa kurun, tumeshindwa hata kumpata muwekezaji mzawa tukampa standards zetu then akarun business..

Nakuhakikishia hata mimi ukinipa huo mradi nauendesha kwa ufanisi kabisa..

Huo mradi ukipewa ni rahisi sana kusecure bank loan na kuchukua Magari yakiwango kama Volvo au mercedes na central workshop unawaachia wenyewe + spare parts supply wewe unabaki na operation tu + mapato.
Unaishinikiza Serikali iondoe daladala zote kwenye hiyo BRT network ili uwe na assurance na return kwa muda mfupi

Nakuhakikishia chief hakuna mradi rahisi kama huo kuuendesha, hapo ni watu tu wanataka kupiga hela, tuache ushabiki wa vyama tusimame kwenye urahisia, KIPI SASA TUNAWEZA?
 
Ipo miradi ambayo inahitaji kuendeshwa na watu wenye mitaji na ziada, miradi kama hii kapuku ikiingangania ni lazima ikutoe roho mzima mzima, jambo la ubia si jambo baya, alimradi uwe ubia wa kugawana kipato kwa ukweli na haki.
Tuombe radhi mkuu, hii nchi siyo ya makapuku ni nchi iliyokosa tu dira, malengo na mwelekeo, mwenye kumeza matonge makubwa ndo anayamenya....
Tupo:
5 bora ya kuwa na dhahabu (
achana na madini mengine kama Tanzanite yenye jina letu) Africa na 17 duniani
3 bora ya uwa na ng`ombe wengi Afrika na 10-15 duniani
10 bora yenye ardhi inayolimika na 20 duniani
5 ya Utalii Afrika
Bado vingine vingi kama Maziwa Tanganyika na Victoria...
 
Bado SGR, isipobinafsishwa inaenda kufa muda si mrefu.

Watanzania hatuwezi kuendesha mradi wowote kwa mafanikio. Hili limejidhihirisha tangu wakati wa mwalimu Nyerere. Viwanda na miradi ya maendeleo vyote vilikufa kwa kuuawa na wasimamizi watanzania wazawa sababu ya kuiba, kuhujumu, kukwapua, kupora, kuharibu, kujilimbikizia mali, na mengine mengi.

Hata sekta binafsi ukiweka watanzania (wazawa) umekwisha, haitodumu watahujumu na kuiua muda mfupi tu
Ebu fikiria Mtendaji mkuu anaambiwa na waziri wake kuwa andaa usafiri wa SGR kutoka Dar hadi Dodoma Mh. Rais na timu yake watatumia kama sehemu ya kuizindua na posho juu....hiyo gharama ni hasara tupu.

Ulishawahi kuona malipo ya Mh. Ameipatia ndege timu ya Yanga au Simba? Hasara tupu.

Waziri mkuu anajengewa nyumba binafsi....Kuna ujinga ujinga mwingi sana...

Inachosha sana. Mimi niliwahi kumgomea boss wangu kwa kuniletea ujinga wa kufanya mradi private ya waziri kisa CEO ameidhinisha ujinga huo.
Nchi hii....Maendeleo tusahau bali maendeleo ya mwendo wa konokono.
 
Ovyo kabisa hii issue, Kwanini wasipewe wazawa wa ndani Kuendesha huo mradi
Ni kweli sio salama sana Serikali kufanya Biashara ila ndio tuwape Waarabu?
Mradi gani wazawa mlisimamia ukafanikiwa!
Wakoloni waliacha mpaka viwanda vya matairi leo viko wapi?
 
Kabla ya kumtafuta mwekazaji wa nje, hii tenda ilitakiwa itangazwe kwa wazawa na wapewe kwa kipindi cha miaka 5 tuone uwezo wao kwanza.
Mbaya zaidi, utaona watendaji wa juu wa mradi watakuwa watanzania wenyewe chini ya usimamizi wa mwarabu.
What a shame!
Kwamba hukuona tangazo la tenda?
Na post iliwekwa humu jf.
 
Back
Top Bottom