DART yaingia mkataba wa miaka 12 na Emirates National Group kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam

DART yaingia mkataba wa miaka 12 na Emirates National Group kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam

Ebu fikiria Mtendaji mkuu anaambiwa na waziri wake kuwa andaa usafiri wa SGR kutoka Dar hadi Dodoma Mh. Rais na timu yake watatumia kama sehemu ya kuizindua na posho juu....hiyo gharama ni hasara tupu.

Ulishawahi kuona malipo ya Mh. Ameipatia ndege timu ya Yanga au Simba? Hasara tupu.

Waziri mkuu anajengewa nyumba binafsi....Kuna ujinga ujinga mwingi sana...

Inachosha sana. Mimi niliwahi kumgomea boss wangu kwa kuniletea ujinga wa kufanya mradi private ya waziri kisa CEO ameidhinisha ujinga huo.
Nchi hii....Maendeleo tusahau bali maendeleo ya mwendo wa konokono.
Misingi mibovu tangu ngazi za juu mpaka ngazi za chini ( wananchi kwa ujumla)
 
KUEREKEA WUCHAGUZI WURU GESHI RA PORISI RIBUNAFUSISHWE
 
HASARA ZINAZOWEZA KUTOKEA

1. Mikopo na Deni la Serikali
- Kama serikali imechukua mkopo wa NMB kununua mabasi, hii inaweza kuongeza mzigo wa deni la umma.
- Kama huduma haitatoa mapato ya kutosha, serikali itabidi kutumia kodi za wananchi kulipa deni hilo.

2. Uwezekano wa Kuongezeka kwa Nauli
- Kwa kuwa ENG ni kampuni binafsi yenye lengo la faida, inaweza kusisitiza kuongeza bei ya abiria ili kufidia gharama zao.
- Hii inaweza kuwapa wananchi wa kawaida shida, hasa kama mishahara haikupanda.

3. Utekelezaji wa Miaka 12 bila Kubadilika
- Kama mkataba haujakusudiwa vizuri, inaweza kusababisha ukandamizaji wa serikali kwa mfumo wa usafiri kwa muda mrefu bila uwezo wa kufanya mabadiliko.

4. Utekelezaji wa Ahadi za UAE Kampuni
- Kama kampuni haitatimiza ahadi zake (kama vile kuboresha huduma), basi serikali itabidi kuingilia kwa gharama kubwa.
 
Ndiyo,wakatangaza tenda kwenda kuendesha brt,kwa hujapeleka kampuni yako?
Tumeunga watu wa DARCOBOA na TABOA, tumepigwa chini.
Tukasema basi apewe mmoja mmoja ambaye ni mzoefu na amefanikiwa kwenye manegement ya biashara ya mabus au daladala,wakagoma.

Hii PPP ni nzuri sana,lakini kwa usiri wa mikataba, tunaenda kupigwa na kunufaisha kikundi cha watu wachache.

Kwa nini hawataki uwazi kwenye mikataba ya PPP ili wazawa tujipange kujua tumekwama wapi ili next projects tujue tujipange vipi??
 
Mchakato huo ulianza mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi. Mnamo 2020, serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, na ENG ikaibuka mshindi

Hiyo para imechomekwa makusudi ili kupoza kelele za kupewa wajomba!

BTW:Juzi tu tumeoneshwa mabasi mapya ya kutumia gesi kwamba ni kwa ajili ya huo mradi na Leo tena PPP!

Si ajabu mabasi yote ni nyinyi huyo mwekezaji ni "bosheni" tu,mambo ya 10% hapo!
 
Na nyie hebu acheni utopolo wenu! Huyo mtu wenu msimtwike mzigo mzito hana huo uwezo! Ni mtu average sana
 
tuambizane ukweli, tumemkopea mwarabu mabasi ya mwendokasi au hii ni miradi miwili tofauti?
 

Attachments

  • Screenshot_20250617-014407_Instagram.jpg
    Screenshot_20250617-014407_Instagram.jpg
    206.2 KB · Views: 24
Hayo mabasi 177 ukute pesa zimetoka tanzania
yaani tunamkopea mwarabu bil 170, kununua bus 225 yaani kila basi 755m, hizi ni MAN au hizihizi howo za mchina? bus 225 kwa masaa 24 maana yake kila bus 10 zitaondoka ndani ya saa moja na kila basi litafanya trip moja tu kwa siku, nadhani tunatumia akili mnemba
 
Back
Top Bottom