DART yaingia mkataba wa miaka 12 na Emirates National Group kuendesha mfumo wa BRT jijini Dar es Salaam

Karibuni sana wajomba.
 
Ni wazi tumeshindwa kuiendesha. Shida wanayopata watumiaji wa mwendokasi inathibitisha hilo.

Private sector ikiendesha labda huduma itaboreka.
CCM ndiyo iliyoshindwa,Usiseme tumeshindwa acheni Chadema waongoze inchi
 
Ina maana hakuna kabisa mwekezaji wa ndani .... mbona wapo wengi sana humu hela ingebaki tanzania yote hiyo kina shabiby ....kina azam kina mo, basi hata wao viongozi wangepeeana tu .ilimradi hels ibaki ndani ....sasa hela inaenda nje
Umemsahau kwa makusudi au kwa kudhamiria, Mh. Msukuma aliye mweusi kama sisi na badala yake umewachagua walewale unaotaka kuwakataa.
 
Hatimaye, mchakato huo sasa umekamilika kwa kutiwa saini kwa mkataba rasmi wa utekelezaji.
Hivi tuna haja ya kuwa na Shahada inayohusiana na masuala ya Transportation Management and Logistics hapa nchini kama wahitimu hawawezi kutusaidia katika hili?
 
Hivi tuna haja ya kuwa na Shahada inayohusiana na masuala ya Transportation Management and Logistics hapa nchini kama wahitimu hawawezi kutusaidia katika hili?
Swali hili laweza kuzihusu shahada nyingi tu nyingine - lakini shida hapo naamini haipo kwenye shahada, bali kwenye mifumo ya nchi yetu.

Maana wengi wa wahitimu wa vyuo vyetu hivi hivi wanafanya vizuri wakienda huko majuu. Wengine wanatia fora.
 
Kwa hiyo suluhisho lake ni kuboresha au kuwapa watu wengine waendeshe?
Kuboresha inaongelewa miaka nenda rudi bila matokeo. Bora wapewe wawezao. Kwa nini wasafiri waendelee kusota daima dumu?
 
Nafikiri itabiresha usafiri iwe kama dubai kwa wajomba
 
Kabla ya kumtafuta mwekazaji wa nje, hii tenda ilitakiwa itangazwe kwa wazawa na wapewe kwa kipindi cha miaka 5 tuone uwezo wao kwanza.
Mbaya zaidi, utaona watendaji wa juu wa mradi watakuwa watanzania wenyewe chini ya usimamizi wa mwarabu.
What a shame!
 
Dah, Samia🙌🏽🙌🏽
 
Inaaikitisha kwamba tukashindwa kuiendesha biashara ya daladala ambayo haina ushindani!

Tumeshindwa kukusanya nauli ,kupanga routes na kupeleka magari services!? Kama tukashindwa kuiendesha biashara ya daladala, je biashara ya SGR biashara ya ndege tutaweza kweli!?

Vijana tunawasomesha NIT wanasogea Transport management, kama wangepelekwa nje ambako kuna miradi kama hii, si wangeweza kujifunza kwa miezi 6 halafu wakaja kuiendesha mradi juu!? Au kama tungemchukua CEO kutoka kwenye makampuni yenye uzoefu wa kuiendesha miradi kama hii, asingeweza kutusaidia kutoa ujuzi kwa makampuni yetu ya ndani, kuiendesha miradi kama hii, badala ya kuleta Kampuni ya kigeni!?

Tunakwama wapi!?
 
Hili ninaliunga mkono. Watanzania hawa walioshindwa ku print hata Tshirts za CCM ndiyo wakaendeshe mradi wa Mabasi yaendayo kasi?
Achilia mbali mradi mzima, madereva tu kuyaendesha kama mabasi yanawashinda
Wafanyabiashara wengi wa bongo ni janja janja sana.... ule mradi ukifanya janja janja kidogo tu huwezi kubreak even...
 
Ninanukuu maneno ya Hayati All H Mwny
"Nchi yangu ni kichw cha Mwndwzm"
Ipo miradi ambayo inahitaji kuendeshwa na watu wenye mitaji na ziada, miradi kama hii kapuku ikiingangania ni lazima ikutoe roho mzima mzima, jambo la ubia si jambo baya, alimradi uwe ubia wa kugawana kipato kwa ukweli na haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…