DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

Kwani tangu balaa lianze, mafuta yamepanda kwa kiasi gani? Mbona kama ongezeko lote anabebeshwa abiria mmoja?

Au kila abiria anatumia lita yake kwa kila kilomita anayosafiri?
Kila abiria anatumia nusu Lita ya mafuta!?!!?
Hivi hawa wanatuchukuliaje watanzania!?!?

Nimewachukia ghafla! Kisa mshahara wa kima cha chini umepanda!?!!! Nao haujapanda hata Kwa asilimia 50!
Nasubiria kuona mapendekezo yakipitishwa Kwa kishindo, ndiyo maana huwa tunaamini tukisikia story mitaani za mafungu kutoka huko kuelekea Lumumba!
Haiwezekani!? Mwendokasi kugeuka kuwa mwendokero na mwendokaraha, na nauli juu!
 
Aiseeee hiiii nchi yaamani sana yani yani Mimi naomba tuuu mungu atuepushe namabaya ila mungu wape weredi viongozi wasirubuniwe namashetani wasioitakia mema nchi hiii kwani ipo siku raia watachoka alafu kitu kitakachotokea ?
 
Kwani tangu balaa lianze, mafuta yamepanda kwa kiasi gani? Mbona kama ongezeko lote anabebeshwa abiria mmoja?

Au kila abiria anatumia lita yake kwa kila kilomita anayosafiri?
MWENDOKASI TISA. KUMI NIMABASI YA MBEZI MLANDIZI. MAFUTA YAMEPANDA KWA MIA TATU LKN HUKU NAULI IMEPANDA KWA MIA $ITA (TOKA 1600 HADI 2200)
NINA IMANI WATU WA LATRA NDIO WANAOMILIKI MABASI YA MBEZI MLANDIZI.....
Mafuta yanapanda kwa asilimia kumi nauli inapanda kwa asilimia arobaini.
Mpaka 2025 Kuna watu watakua hawawezi kupanda vyombo vya moto
 
Habari nzuri kwa kuongeza kipato.. tupate huduma na mengi..

Kazi iendeleee....
 
1500 wamekosa ubunifu kabisa, hawana tofauti na msingida anaeamini watz wote Wana maisha bora. 1500 ni pesa mtu anaacha nyumbani.
 
Kabisa, njia jumuishi inaanzia wapi mpaka wapi? Mbona hakuna hiyo nauli ya 800, kuna 400,650,1050. Sijui hiyo jumuishi ni ipi Aiseee
Mkuu wangu hii TZ hatujui tunataka nini
Kupandisha nauli sawa je huduma zinazotolewa zilidhi mahitaji
Chukulia mtu anaenda kibaha au gerezeni/kivukoni may be yupo temboni huwa wanapakizwa kama mifugo tuu
Sasa sijajua wamejipanga vp kuboresha huduma au ndio kuboresha nauli kwanza
 
Ukitaka kutoa maoni yako kuhusu nauli ha mwendokasi iongezeke au laah tuma e mail kama walivyoelekeza kwenye hii attachmentView attachment 2239961
 
Hapana elf 1500 ni ndogo, ilitakiwa iwe sh elf5, ili chenji isisumbue
 
Lengo la usafiri wa uma ni kupunguza ukali wa maisha kwa mwananchi na sio 100% biashara .Naona wanasahau hilo
 
Naunga mkono hoja yako. Tatizo lipo kwenye hii menejimenti ya Dart. Wapigaji walikimbilia na kukwapua mradi. Serikali ilikwama wapi sijui.
 
Nadhani ingependeza iwe buku dasi kabisa ili tukome kabisa na viherehere vyetu. Na waruhusu daladala njia hiyo zianze kufanya kazi waione kazi
 
Nashauri iwe 3000 ili miradi iishe haraka tumalize na huo umeme huko vijijini tupumzike.WANAUME WA DAR TUNAHUDUMIA NCHI NZIMA HALAFU KUNA DUWANZI MMOJA AMEKAA KIJIJINI HUKO ANAJAMBA HOVYO ATALETA DHARAU.
Huku vijijini umbali kama huo kutoka kivukoni hadi kimara tunalipa 3000 siku nyingi na hatulalamiki ,kituo hadi kituo buku,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…