Wakuu,
Inanisikitisha kuwa JF inageuzwa kuwa jamvi la hovyo hovyo. Nimesoma thread zote tangu Mkuu Mwanakijiji alivyotuarifu kuhusu taarifa za mazishi na kweli sipendezewi na mwenendo huu.
Mwanakijiji alisema vizuri...Ballali amekufa bila kushtakiwa hivyo ni raia huru. Kama wengine hatupendi hili, basi tuondolee uvivu vyombo ambavyo havikuweza kumshtaki na kumtia hatiani. Kama wengine hatuamini kuwa amekufa, basi endelea kuamini hivyo na kwa wanafamilia (na wengineo ambao wanaamini amekufa) wapeni nafasi ya kumaliza msiba wao.
Imedhihirika kuwa tunapoteza utu, mwelekeo, heshima na busara. Tukianzia na utu, desturi zetu zinaheshimu wafu, shughuli za msiba (hususan kwa wanafamilia) na maziko. Kama ukipata nafasi kuangalia tovuti ya nyumba ya mazishi tuliyopatiwa na Mwanakijiji, utaona kuwa haya mazishi na kila kitu ni private. Sasa kama wanafamilia wametaka iwe private, kwanini tuingilie? Inanishangaza kuwa watu wanafuatilia kuona ni state ngapi Ballali aliishi na kuna connection gani kati ya Ballali na watu wengine. Nafikiri hata kama wanaJF hawa wana nia nzuri, nafikiri imevuka mpaka kufikia kitu kinachoitwa stalking Hii ni kuivunjia hadhi JF na ni sawa na mapaparazi wenye kutafutia picha za uchi za celebrities kwa tabloids.
Baada ya kusema hayo, ningependa nisieleweke kama sina uchungu na nchi yangu au wizi uliotokea BoT. Lakini naamini kuwa tunapoteza mwelekeo. Bila kujali kuwa Ballali amefariki au la, yeye ni "tip of an iceberg". Kuna wengi waliohusika na ufisadi, wapo bado wanadunda tu na mali walizoiba, wengine bado wapo madarakani. Hivi kweli nguvu na juhudi zetu zielekezwe kwa Ballali ambaye haikujulikana alipo, hakuwa na nguvu kutokana na ugonjwa, na sasa tunaambiwa amekufa? Mch. Kishoka na wengineo waliuliza, mbona tumewaacha kina Meghji, Mramba, Mgonja, Yona, Mkapa, Chenge, Jeetu na wengine wengi? Naamini tuna uwezo wa kutambua zaidi ya kifo cha Ballali. Hivi kama kweli amekufa, na kuzikwa hiyo kesho, tutapata nini? Siri amekufa nayo (labda), pesa zimeibwa...tunataka tumfufue ili ajibu tuhuma?
Nilifadhaishwa pale mkuu Mushi aliposema "nobody cares" about MwK's friend. Personally I believe this is the lowest point of humanity na huyo asemaye hivyo hana tofauti na mafisadi wanaoliibia taifa. Inawezekana huyo rafiki wa MwK hatumjui wala hatuhusu, lakini ukweli ni kuwa kuna watu aliwagusa, akiwemo MwK ambaye ni mwenzetu. Kukebehi kifo chake kutotangazwa ni sawa na mafisadi wakisema "sijali kuwa watu wa Chole Samvula hawatapata zahanati kutokana na kuiba kwangu fedha za umma. Mimi naishi Dar."
Basi ombi langu ni kwenu wanaJF tuendelee na kuendeleza nchi yetu, Ballali aachwe apumzike kwani kuna wengi tu ambao ni wabaya zaidi yake na bado wanatucheka. Tuwe na usongo na hao.