Preciousvision
JF-Expert Member
- May 14, 2026
- 888
- 1,205
07 Agosti 2026
Uhamishoni
Nje ya Tanzania
Bw. David Jumbe msaidizi wa karibu wa mheshimiwa Tundu Lissu katika mahojiano exclusive 07 Agosti 2026 UHAMISHONI NJE YA TANZANIA
View: https://m.youtube.com/watch?v=sZ0ZZ6LjIck
David Jumbe, msaidizi wa karibu wa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA (Tundu Lissu), aliye trend / aligonga vichwa vya habari kufuatia tukio la kutekwa nyara usiku wa tarehe 20 Mei 2026. Sakata hili lilivuta hisia za wengi na kuripotiwa kwa kina na vyombo mbalimbali vya habari vya mtandaoni.
Katika mahojiano exclusive akiwa nje ya Tanzania afunguka mengi mazito, ikiwemo mashirika kibao ya kimataifa ku dokumenti yote kwa umakini yaliyompata tarehe 20 Mei 2026
Mashirika na taasisi za kimataifa zilimfuata ili kupata mambo yote baada ya kumuomba ridhaa wa- dokumenti ukatili wa vyombo vya nchi ya Tanzania chini ya utawala wa Samia, kwake yeye Djumbe pia kwa wanaCHADEMA, wanaharakati hata wale wasio na vyama ila waliopishana mtazamo na utawala (regime) wa Samia
David Jumbe asema wengi wamekimbia nje wapo nje ya Tanzania kunusuru maisha yao baada ya kutekwa, kuteswa na kuepuka kifo
David DJumbe aelezea hali ya mwenyekiti Tundu Lissu aliye kizuizini Ukonga gereza kuu Dar es Salaam. DJumbe alikuwa na tabia ya kumtembelea Tundu Lissu hivyo ana share mambo kibao kuhusu maisha ya mwenyekiti aliye gerezani kwa tuhuma za kesi ya uhaini anavyoweza kukabiliana na changamoto anayopitia huyu yupo tayari kwa hatima yoyote waliompangia watawala madhalimu waovu.
Bofya video hii upate simulizi kamili za kina exclusive from the horse's mouth (msimuliaji mwenyewe) ambazo zitakufanya uelewe hali halisi ya ukandamizaji, utekaji, kufuatilia wapinzani, kuwaumiza, kuwapoteza ili watawala wabaki madarakani kwa damu za watu
View attachment 3645685
Huyo mburukenge anajisumbua bure Rais wetu hakuna kima atamfanya chochote