David Djumbe, msaidizi wa Tundu Lissu aongea mazito akiwa uhamishoni nje ya nchi 07 Agosti 2026

David Djumbe, msaidizi wa Tundu Lissu aongea mazito akiwa uhamishoni nje ya nchi 07 Agosti 2026

Sijui lini hawa watu wataishi kama watanzania wa kawaida. Wana familia wanadeserve kuishi kama wananchi wa nchi hii.
Nchi imetekwa na majambazi hata hii CCM unayoiona sasa imeshikiliwa mateka na Majambazi.
 
Nilibahatika kufanya mazungumzo na asylum seekers 3 nilipotembelea nchi fulani baada ya kuwa wameshaingia katika mfumo rasmi na kuwa raia ila bado ile hali ya kutoondoka nyumbani kwa hiyari unaona kuna kitu wanakikosa .

Ni maisha ya upweke wanapitia na vitisho juu huku nyuma akina Madelu wanaaminisha kwamba wanalipwa mabilioni kuchafua nchi sijui kuhamasisha maandamano , hakuna shirika litatoa malipo ya mabilioni kwa wakimbizi wa kisiasa , maana wakifanya hivyo itakua ngumu kufanya scrutiny nani amekimbia tishio la usalama na nani ametafuta shortcut kwa ajili ya passive income ya stipends tu na kulala bure.

Leo hii unaweza usiamini kuna watu bado wanamsaka yule bwana mdogo Sativa wampoteze sasa kumteka walimteka wao miaka 2 imepita sasa na hawawezi kuchunguza sababu wao ndio walifanya tukio hilo sasa wanaoana njia pekee ni kumsaka na akina Maria wawapoteze.

Kimsingi kwa wasiojua ni kwamba hadi leo kinachowashinda hao jamaa kuwarudisha Tanzania ni sababu upo ushahidi wa wazi walifanyiwa ukatili na wengine bado wanafuatiliwa hivyo hawana nguvu ya kisheria kuomba extradition ya hawa watu maana hakuna nchi au shirika linalowapa hifadhi wakimbizi wa kisiasa litakubali kuchafua taswira yake kumtoa mtu akauwawe ndio maana unaona wanawatumia vibaka kama akina Msuya na Buyobe wakawarubuni ili wawasogeze wawateke .

Watu walioenda into Exile (uhamishoni) historia inaonesha hupekelea utawala katili kuanguka. Lazima utawala wa Samia Hassan unakosa usingizi kwa kuona waTanzania wapo uhamishoni baada ya kukimbia mikono miovu ya vyombo vyake vya usalama

HISTORIA
UTAWALA WA MAKABURU ULIOGOPA SANA WATU WALIOCHOROPOKA KWENDA UHAMISHONI, HIVYO WAKAANZISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KURIPOTI WATAKAORUDI KISIRI

Mfumo wa polisi wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Makaburu Afrika ya Kusini kuwatafuta vijana waliohama nchi


Utawala wa ubaguzi wa rangi uliwafuatilia vijana na wanaharakati waliokimbia nchi kwa kutumia Tawi la Usalama la Polisi wa Afrika Kusini (SAP), wakifanya kazi pamoja na idara za ujasusi za kijeshi na mashirika ya usalama wa serikali kama BOSS (Ofisi ya Usalama wa Nchi). Vikosi hivi vilitumia ufuatiliaji wa ndani, udhibiti wa mipaka, na shughuli za kuvuka mipaka ili kufuatilia, kujipenyeza, na kuwalenga wakimbizi.

Ufuatiliaji Muhimu na Mifumo ya Kipolisi
  • Tawi la Usalama (Tawi Maalum): Tawi kuu la polisi lililosimamia mitandao ya watoa habari wa ndani katika vitongoji ili kutambua vijana wanaoondoka kwenda uhamishoni kijeshi au kisiasa.
  • Sehemu ya G (Tawi la Nje/Nje): Kitengo maalum ndani ya Tawi la Usalama kilichopewa jukumu maalum la kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu shughuli za kupinga ubaguzi wa rangi na wanaharakati nje ya mipaka ya Afrika Kusini.
  • Uingiliaji kati na Wapelelezi: Mawakala wa siri (kama vile waendeshaji wa siri) walijipenyeza katika harakati za ukombozi na vikundi vya wanafunzi ndani ya nchi na nje ya nchi katika maeneo jirani kama Botswana, Lesotho, na Swaziland.
  • Uvamizi wa Mpakani na Vikosi vya Siri: Vikosi maalum na vikosi vya kijeshi vilifanya utekaji nyara, mauaji, na uvamizi wa mpakani katika nchi jirani ili kuwasaka na kuwaondoa vijana waliojiunga na jeshi.
  • Sheria za Pasi na Udhibiti wa Mipaka: Vizuizi vya ndani vya usafiri, vitabu vya pasi, na udhibiti mkali wa visa vya kutoka vilitumika kuashiria watu waliopotea na kufuatilia mabadiliko ya idadi ya watu katika miji midogo.

ENGLISH:
The apartheid regime tracked young people and activists who fled the country using the Security Branch of the South African Police (SAP), working alongside military intelligence and state security agencies like BOSS (Bureau for State Security). These units used domestic surveillance, border controls, and cross-border operations to monitor, infiltrate, and target exiles.

Key Tracking and Policing Mechanisms
Security Branch (Special Branch): The primary elite police arm that ran domestic informant networks in townships to identify youth leaving for military or political exile.

G-Section (External/Foreign Branch): A specialized division within the Security Branch specifically tasked with gathering intelligence on anti-apartheid activities and activists outside South Africa's borders.

Infiltration and Spies: Secret agents (such as deep-cover operatives) infiltrated liberation movements and student groups both inside the country and abroad in neighboring havens like Botswana, Lesotho, and Swaziland.

Cross-Border Raids and Covert Units: Specialized units and military forces conducted abductions, assassinations, and cross-border raids into neighboring countries to track down and eliminate young recruits.

Pass Laws and Border Control: Internal movement restrictions, passbooks, and strict exit visa controls were used to flag missing individuals and monitor demographic shifts in townships.
 
Watu walioenda into Exile (uhamishoni) historia inaonesha hupekelea utawala katili kuanguka. Lazima utawala wa Samia Hassan unakosa usingizi kwa kuona waTanzania wapo uhamishoni baada ya kukimbia mikono miovu ya vyombo vyake vya usalama

HISTORIA
UTAWALA WA MAKABURU ULIOGOPA SANA WATU WALIOCHOROPOKA KWENDA UHAMISHONI, HIVYO WAKAANZISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KURIPOTI WATAKAORUDI KISIRI

Mfumo wa polisi wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Makaburu Afrika ya Kusini kuwatafuta vijana waliohama nchi


Utawala wa ubaguzi wa rangi uliwafuatilia vijana na wanaharakati waliokimbia nchi kwa kutumia Tawi la Usalama la Polisi wa Afrika Kusini (SAP), wakifanya kazi pamoja na idara za ujasusi za kijeshi na mashirika ya usalama wa serikali kama BOSS (Ofisi ya Usalama wa Nchi). Vikosi hivi vilitumia ufuatiliaji wa ndani, udhibiti wa mipaka, na shughuli za kuvuka mipaka ili kufuatilia, kujipenyeza, na kuwalenga wakimbizi.

Ufuatiliaji Muhimu na Mifumo ya Kipolisi
  • Tawi la Usalama (Tawi Maalum): Tawi kuu la polisi lililosimamia mitandao ya watoa habari wa ndani katika vitongoji ili kutambua vijana wanaoondoka kwenda uhamishoni kijeshi au kisiasa.
  • Sehemu ya G (Tawi la Nje/Nje): Kitengo maalum ndani ya Tawi la Usalama kilichopewa jukumu maalum la kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu shughuli za kupinga ubaguzi wa rangi na wanaharakati nje ya mipaka ya Afrika Kusini.
  • Uingiliaji kati na Wapelelezi: Mawakala wa siri (kama vile waendeshaji wa siri) walijipenyeza katika harakati za ukombozi na vikundi vya wanafunzi ndani ya nchi na nje ya nchi katika maeneo jirani kama Botswana, Lesotho, na Swaziland.
  • Uvamizi wa Mpakani na Vikosi vya Siri: Vikosi maalum na vikosi vya kijeshi vilifanya utekaji nyara, mauaji, na uvamizi wa mpakani katika nchi jirani ili kuwasaka na kuwaondoa vijana waliojiunga na jeshi.
  • Sheria za Pasi na Udhibiti wa Mipaka: Vizuizi vya ndani vya usafiri, vitabu vya pasi, na udhibiti mkali wa visa vya kutoka vilitumika kuashiria watu waliopotea na kufuatilia mabadiliko ya idadi ya watu katika miji midogo.

ENGLISH:
Mfumo wa Samia Wameshaanza utaratibu wa makaburu wa Afrika Kusini kutumia wajumbe na wanafunzi kuripoti 'Wahamiaji'

07 Agosti 2026
Kinondoni, Dar es Salaam
Tanzania

DC SAAD MTAMBULE : WANAFUNZI MKAWAAMBIE WAZAZI JUU 'UHAMIAJI HARAMU' KINONDONI

View: https://m.youtube.com/watch?v=d7oFRuKVK-w
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amewataka wanafunz i kutokaa kimya na KUWAFICHUA wahamiaji haramu

Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kinondoni inatekeleza kampeni ya "Mjue Jirani Yako" na kuanzisha Klabu za Uhamiaji mashuleni ili kutoa elimu ya utambuzi wa wahamiaji haramu kabla ya kuchukua hatua za kisheria. Hatua hii inalenga kujenga uelewa kwa jamii na wanafunzi kuhusu sheria za uhamiaji.

Mikakati ya Elimu na Uhamiaji Kinondoni
Kampeni ya Mjue Jirani Yako: Inahimiza wananchi kuwajua majirani zao ili kubaini uwepo wa raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria.

Klabu za Uhamiaji Mashuleni: Zimeanzishwa ili kuwapa wanafunzi uwezo wa kumtambua mhamiaji haramu na kuelewa athari zake tangu wakiwa wadogo.

Ushirikiano wa Viongozi: Viongozi wa wilaya wanahamasisha jamii kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Tanzania kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria

1786226616506.png

Photo: Mayor Songoro Mnyonge during past event of CCM party rally 2025
 
Kenya wako strong kwenye intelligence kumbuka entire west inteligence wana vituo vyao kenya kuanzia CIA,MOSAD,MI6 na nyinginezo wapo kenya kabla ujafikiria kwenda kufanya utekaji au nia ovu tayari watakuwa na taarifa zako ..kumbukeni ya maria sarungi chap walivyomtoa kwenye mdomo wa mamba
Mbona Mzee Besigye alikamatwa kirahisi sana???!!
 
Dereva wa Lissu anusurika kutekwa, baada ya miezi kadhaa Dereva wa Heche anakutwa chumbani amefariki.
Ndicho tunachokiweza Tanganyika. Mbinu za kuuwa ziko juu kuliko Nchi zote duniani.

Na mbinu za maendeleo na technology ziko chini kuliko Nchi zote duniani. Na sio bahati mbaya.

Watawala wamechagua mwendo huo.
 
kun watu nikisikia wanautaka u-Rais na uwezo wao ni mdogo nao naumia sana
 
Simulizi hii ya Djumbe jinsi inavyopokewa na jumuiya ya kimataifa ni tofauti na wanaCCM wanavyojifariji kuwa yatakwisha, hayatishi, ni drama tu n.k

Lakini baada ya kupitia mitizamo ya walimwengu walivyochukulia hadithi za kale za waMatengo kama zilivyohifadhiwa na profesa Joseph Mbele ninashawishika kuwa kuna kubwa linakuja kuwapata waliohusika na matendo haya ya kuogofya

TOKA MAKTABA :

​

Wednesday, April 15, 2009​

Hadithi za waMatengo Minnesota​


Jana nilifika hapa mjini St. Joseph, Minnesota, nikiwa mgeni wa vyuo vya St Benedict/St. John's. Nilialikwa na Profesa Lisa Ohm, ambaye alihudhuria semina niliyoshiriki kuiendesha miaka michache iliyopita, kuhusu hadithi za waSomali. Katika semina ile, Profesa Ohm alipata fursa ya kununua kitabu changu cha hadithi za Wamatengo. Baada ya kukisoma, aliniandikia ujumbe akisema kuwa amekipenda sana na akanipa tafakari yake kuhusu yaliyomo katika baadhi ya hadithi zile. Tafakari yake ilinifungua macho, kwani alinionyesha mambo ambayo sikuwa nimeyawazia, ingawa mimi ni mMatengo.

Profesa Ohm alinieleza kuwa anatumia kitabu kile cha hadithi za waMatengo katika kozi yake ya hadithi. Alisema pia kuwa hapo mjini St. Joseph wana kikundi cha watu ambao wamekuwa wakizisoma na kuzijadili hadithi zile. Ziara yangu ilitazamiwa kuwa fursa ya wanafunzi wake na wanakikundi kujifunza zaidi kuhusu hadithi na utamaduni wa waMatengo na waAfrika kwa ujumla.

Jana tulijumuika katika huo mjadala, ambao ulidumu kiasi cha saa nzima. Nilijitambulisha kifupi, na nikatoa fursa ya wao kuuliza masuali. Walikuwa na masuali mengi kuhusu vipengele mbali mbali vya hadithi za kiMatengo na utamaduni wao, na pia masuala ya hadithi kwa ujumla, wakizingatia yale niliyoandika katika kitabu changu.

Baadhi ya masuala yaliyojitokeza ni athari za kurekodi katika maandishi hadithi ambazo kwa asili yake ni za masimulizi ya mdomo. Katika hali yake ya kawaida, ya masimulizi, hadithi hizi hubadilika muda wote, hata kama ni kwa kiasi kidogo sana, kwani wasimuliaji hawakariri maneno ya hadithi. Wakiambiwa kusimulia tena na tena hadithi ile ile moja, tofauti nyingi zinajitokeza. Ukirekodi mara moja hadithi hiyo, kama tunavyofanya, na kisha kuiweka kitabuni, unakuwa umeipa sura ambayo haibadiliki, wakati katika mazingira yake halisi, hadithi hii haina sura moja.

Hili ni tatizo moja, ambalo nimelielezea katika kitabu changu. Yako masuala mengi mengine. Kwa mfano, kuna dhana zilizomo katika hadithi, ambazo undani na maana yake sisi watu wa leo hatuzielewi. Ni dhana za kale mno, na hata lugha inayotumiwa aghalabu hatuielewi, kwani nayo ni ya kale mno. Suala hili linajitokeza zaidi kwenye nyimbo zilizomo katika hadithi, na msingi wa tatizo ni kuwa nyimbo huwa na muundo maalum ambao si rahisi kubadilika, na kila kizazi kinarithi nyimbo hizi na kuziimba kama zilivyo. Watafiti wanakubaliana kuwa nyimbo ni kati ya vipengele vya hadithi ambavyo ni vigumu kabisa kubadilika.

View: https://m.youtube.com/watch?v=f870_dcEc64
Suala jingine lililojitokeza ni vitendo vya kutisha vilivyomo katika hadithi, kama vile vifo visivyo vya kawaida na mapambano baina ya binadamu na majitu ya kutisha. Leo waMarekani wengi wanajiuliza kama mambo hayo yanastahili kusimuliwa kwa watoto au la. Kumekuwa na juhudi ya miaka mingi Ulaya na Marekani ya kujaribu kurekebisha hadithi ili kupunguza vipengele hivyo vya kutisha, kwa hoja kwamba vinaweza kuwa na athari mbaya kwa watoto.

Binafsi, ninazingatia kuwa tangu enzi za mababu na mabibi, kuanzia huko kwetu hadi Ulaya na sehemu zingine duniani, jamii asilia hazikuwa na tatizo lolote kuhusu suala hilo. Hadithi hizi ndizo walizokuwa wanasimuliwa watoto, na hazikuwaathiri. Hata hadithi za waJerumani wa zamani, ambazo hatimaye zilirekodiwa na watafiti kama akina Jacob Grimm na mdogo wake Wilhelm Grimm, ambao walianza kuzichapisha mwaka 1812, zilikuwa na mambo ya kutisha au "yasiyofaa." Kuna malumbano miongoni mwa watafiti kuhusu suala la kama hao jamaa walizirekebisha kabla ya kuzichapisha.

Wanasaikolojia wa Marekani wanahangaika na masuali hayo, lakini kwa mtazamo wangu na uzoefu wangu wa kusimulia hadithi hizi kwa watu wazima na pia watoto wa hapa Marekani, naona labda watu wazima hawawaelewi vizuri watoto. Kila nilipopata fursa ya kuwasilimua watoto wa kiMarekani hadithi, wameonyesha kuvutiwa nazo kwa namna mbali mbali, hata kama zina mambo ambayo watu wazima wangesema yanatisha. Naona kuwa saikolojia ya watoto ni fumbo ambalo sisi watu wazima wa leo bado hatujalifumbua. Ni suala linalohitaji utafiti zaidi. Hayo yote nilipata fursa ya kuyaeleza kwenye mazungumzo ya jana.

Baada ya mjadala huo wa darasani, nilipata fursa ya kuongea tena kwa undani na Profesa Ohm, nyumbani kwake. Tuliongea kirefu, yeye, mume wake, na mimi, na Profesa Ohm alieleza kwa undani zaidi uchambuzi na tafakari yake kuhusu vipengele mbali mbali vya hadithi za kiMatengo. Aliniuliza pia masuali ya kufikirisha. Niliona jinsi anavyozama katika uchambuzi na kufichua mambo ambayo sikutegemea, yanayoonyesha falsafa nzito katika hadithi hizo. Pamoja na kuwa nami ni mtafiti, na ni mzaliwa katika utamaduni wa kiMatengo, ninakiri kuwa ninayo mengi ya kujifunza kutoka kwa watafiti makini kama Profesa Ohm. Nimeamini kwa miaka mingi kuwa mtu wa utamaduni tofauti anaweza kukuonyesha mambo yaliyomo katika utamaduni wako ambayo wewe mwenye utamaduni yatakufungua macho na akili kwa namna ambayo hukutegemea.

Sitasahau jambo hili, la kukutana na wageni hao, waMarekani, ambao wanazama namna hii katika kutafakari hadithi na utamaduni wa kwetu. Ni fundisho kwetu pia, kwamba tujizatiti kujifunza mambo ya wenzetu. Tutatambua tunavyofanana au kutofautiana, na tutajenga heshima kwa tamaduni zote, kwani kila utamaduni umesheheni hazina kubwa ya sanaa, falsafa na maadili ambayo kwa ujumla wake ni hazina kwetu binadamu
 
Nakubali kwamba waovu wanajuwa nguvu ya hawa Boda; ila siafiki hilo la "kuishi nao vizuri".
Mtu mwovu kamwe hawezi kuishi vizuri na asiyekuwa mwovu mwenzake.

Hizo unazoziita "mbinu" za kuwatuliza boda zina mwisho wake.
tuombe ziwe na mwisho na wanawatumia sana kupata taarifa "informer" kila kijiwe lazima awepo.
 
tuombe ziwe na mwisho na wanawatumia sana kupata taarifa "informer" kila kijiwe lazima awepo.
Ni kweli. Na hii ni kila nchi duniani.
Tofauti ni kwamba hawa 'informer' wa hapa kwetu wanawatumikia viongozi wanaofanya uovu dhidi ya wananchi.

Hata hivyo, uamini wangu ni kuwa hilo halitazuia kuleta mabadiliko.
 
Back
Top Bottom