David Kafulila alitetemesha Bunge na kupokelewa kifalme

Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa David Kafulila Ameamsha hisia, kuwagusa waheshimiwa wabunge na kuwarejesha mbali sana kihisia. Chuma Kafulila kaliteka Bunge, kalitetemesha na kalitikisa kwelikweli. Hii ni baada ya kutambulishwa Bungeni kama Mkurugenzi wa PPP na Mheshimiwa Speaker Dkt Tulia Acksoni Mwansasu.

Ambapo Bunge zima na wabunge wote na kwa Umoja wao wamempatia heshima kubwa na ya kipekee sana utafikiri utambulisho wa Mfalme wa Uingereza ndani ya Bunge. Ambapo imeshuhudiwa meza zoootee za waheshimiwa Wabunge zikilindima kwa kishindoo cha makofi ya kumpigia na kumpatia heshima ya kipekee Mheshimiwa Kafulila.

Bila shaka waheshimiwa wabunge wote bado wana kumbukumbu vichwani mwao juu ya alama alizoziacha za kizalendo, alizoziacha mzalendo huyu na mchapakazi aliyetukuka wakati wa ubunge wake 2010-2015.ambapo ni yeye amewahi kuweka historia ya kulifanya Bunge likafanya na kuendelea na shughuli zake mpaka saa Tano usiku katika Historia ya Bunge letu wakati wa sakata la Escrow.

Imeonyesha bunge zima na waheshimiwa wabunge wote wana kiu kubwa sana na kumhitaji Mheshimiwa Kafulila ndani ya Bunge, wanatambua uwezo wake, mchango wake na sauti yake kuwa bado inahitajika sana Bungeni wanaona ni kama kuna kitu kimepungua Bungeni kwa kutokuwepo kwa Mwamba huyu wa kigoma David Kafulila.

Waheshimiwa wabunge wanaona kuwa mtu huyu asiye na makandokando, Mzalendo wa dhati, mpole, mtulivu, makini, jasiri, shupavu, hodari, Madhubuti, imara, mnyenyekevu na mwenye misimamo ya dhati katika kutetea Taifa letu bado mchango wake unahitajika ndani ya Bunge letu.

Waheshimiwa wabunge wanaona kuna kazi Mheshimiwa Kafulila anatakiwa akasaidiane nao ndani ya Bunge ndio sababu ya heshima kubwa walioweza kumpatia,ndio sababu ya mapokezi mazito walioweza mpatia,ndio sababu ya kuguswa kwa wabunge wengi baada ya utambulisho wake, ndio sababu ya kumshangilia na kumpigia makofi bila kukoma ,ndio sababu ya kumheshimisha na kumpa thamani yake.

Waheshimiwa wabunge waliokuwepo na ambao hawakuwepo wakati wa sakata la Escrow wanakumbuka na wanakumbukunbu nzuri juu ya kazi kubwa, ya kishujaa na kizalendo kwa Taifa letu iliyofanywa na mheshimiwa David Kafulila aliyekuwa amejitolea maisha yake kupigania Taifa letu bila kujali vitisho kutoka kwa mtu yeyote yule.

Waheshimiwa wabunge wametuma kwa Vitendo ujumbe mzito sana juu ya Hazina hii kwa Taifa letu kuwa Bado sauti ya Mheshimiwa David Kafulila inahitajika sana Bungeni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View attachment 3017339
Kafulila ni bonge la kiongozi aise
 
Waheshimiwa wabunge wameguswa sana mpaka wengine wameshindwa kuficha hisia zao za upendo kwa Mheshimiwa Kafulila.nakujikuta wakipiga makofi kwa hisia kali sana huku macho yao yakiwa ni kama yanataka kutokwa na Machozi
Kwahiyo kawatoa machozi sio?😂😂😂😂
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa David Kafulila Ameamsha hisia, kuwagusa waheshimiwa wabunge na kuwarejesha mbali sana kihisia. Chuma Kafulila kaliteka Bunge, kalitetemesha na kalitikisa kwelikweli. Hii ni baada ya kutambulishwa Bungeni kama Mkurugenzi wa PPP na Mheshimiwa Speaker Dkt Tulia Acksoni Mwansasu.

Ambapo Bunge zima na wabunge wote na kwa Umoja wao wamempatia heshima kubwa na ya kipekee sana utafikiri utambulisho wa Mfalme wa Uingereza ndani ya Bunge. Ambapo imeshuhudiwa meza zoootee za waheshimiwa Wabunge zikilindima kwa kishindoo cha makofi ya kumpigia na kumpatia heshima ya kipekee Mheshimiwa Kafulila.

Bila shaka waheshimiwa wabunge wote bado wana kumbukumbu vichwani mwao juu ya alama alizoziacha za kizalendo, alizoziacha mzalendo huyu na mchapakazi aliyetukuka wakati wa ubunge wake 2010-2015.ambapo ni yeye amewahi kuweka historia ya kulifanya Bunge likafanya na kuendelea na shughuli zake mpaka saa Tano usiku katika Historia ya Bunge letu wakati wa sakata la Escrow.

Imeonyesha bunge zima na waheshimiwa wabunge wote wana kiu kubwa sana na kumhitaji Mheshimiwa Kafulila ndani ya Bunge, wanatambua uwezo wake, mchango wake na sauti yake kuwa bado inahitajika sana Bungeni wanaona ni kama kuna kitu kimepungua Bungeni kwa kutokuwepo kwa Mwamba huyu wa kigoma David Kafulila.

Waheshimiwa wabunge wanaona kuwa mtu huyu asiye na makandokando, Mzalendo wa dhati, mpole, mtulivu, makini, jasiri, shupavu, hodari, Madhubuti, imara, mnyenyekevu na mwenye misimamo ya dhati katika kutetea Taifa letu bado mchango wake unahitajika ndani ya Bunge letu.

Waheshimiwa wabunge wanaona kuna kazi Mheshimiwa Kafulila anatakiwa akasaidiane nao ndani ya Bunge ndio sababu ya heshima kubwa walioweza kumpatia,ndio sababu ya mapokezi mazito walioweza mpatia,ndio sababu ya kuguswa kwa wabunge wengi baada ya utambulisho wake, ndio sababu ya kumshangilia na kumpigia makofi bila kukoma ,ndio sababu ya kumheshimisha na kumpa thamani yake.

Waheshimiwa wabunge waliokuwepo na ambao hawakuwepo wakati wa sakata la Escrow wanakumbuka na wanakumbukunbu nzuri juu ya kazi kubwa, ya kishujaa na kizalendo kwa Taifa letu iliyofanywa na mheshimiwa David Kafulila aliyekuwa amejitolea maisha yake kupigania Taifa letu bila kujali vitisho kutoka kwa mtu yeyote yule.

Waheshimiwa wabunge wametuma kwa Vitendo ujumbe mzito sana juu ya Hazina hii kwa Taifa letu kuwa Bado sauti ya Mheshimiwa David Kafulila inahitajika sana Bungeni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View attachment 3017339
Maza akiona au kusikia mtu anafagiliwa sana kwa misifa sifa mingi huwa anampotezea huyo mtu kama vile hayupo 😳😂😅😂

Huenda natania tu lakini inaweza kuwa kweli 😇🛫
 
Maelezo meeeeeeengi mpaka inachosha kuyasoma, muda wa kupoteza kwa kuandika maandiko hayo yote ni bora ungekuja na Andiko la nini kifanyike ili watanzania wawe na maisha bora. Inashangaza sana wanasiasa wanavyosifiwa kwa hali ya juu, huku watanzania asilimia kubwa wakiishi kwenye wimbi la umaskini uliopitiliza na watawala kuendelea kuneemeka.

Maprofesa na Madaktari wamevikimbia Vyuo Vikuu na kwenda kwenye Siasa manake wanajua ni sehemu ya kupiga hela kirahisi kutokana na akili za Watanzania zilivyo.
 
Hayo unayoyataka yanaendelea kufanywa kwa kasi sana na serikali ya Rais Samia.
 
Unalipwa kiasi gani maana watanzania kwa rushwa hatujambo. umekuwa mwijaku rapper sio kila ukiamka unamsifia Kafulila hivi anakufahamu kweli au ndio chawa uchawini bata batani
 
Maza akiona au kusikia mtu anafagiliwa sana kwa misifa sifa mingi huwa anampotezea huyo mtu kama vile hayupo 😳😂😅😂

Huenda natania tu lakini inaweza kuwa kweli 😇🛫
Ni uzalendo mkubwa sana na jambo jema sana kuwapongeza,kuwatia moyo na kutambua michango yao viongozi wazalendo aina ya Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan pamoja na Mheshimiwa. Najuwa watu aina yako hampendi tuwataje kwa kuwa mioyo inawauma sana.
 
Unalipwa kiasi gani maana watanzania kwa rushwa hatujambo. umekuwa mwijaku rapper sio kila ukiamka unamsifia Kafulila hivi anakufahamu kweli au ndio chawa uchawini bata batani
Silipwi kitu maana kazi yangu ni ya kizalendo .na nimekuwa nikifanya hivi tangia muda tu nilipojiunga na jukwaa hili.
 
Nikweli Wabunge wamethibitisha hilo
Waheshimiwa wabunge wameonesha kumkubali sana Mheshimiwa David Kafulila na kuhitaji kuona akiungana nao Bungeni hapo mwakani, kwa kuwa sauti yake inahitajika sana ndani ya Bunge
 
Back
Top Bottom