Ukilipwa kwa Paypal unatoaje hiyo hela. Wewe unajua hata Paypal kweli? Hao Wajamaica gani wanapanga chumba wanalipa kwa Paypal??
Hapo Kenya wanauza vitu Online kwenye masoko ya dunia sababu wanapokea pesa Paypal na wanatoa through Mpesa. Yaani mchonga Kinyago pale Mwenge hana haja ya kwenda Europe kuuza,anauza online tu.
Watu wapo kwenye Uraia pacha now, Wanachuma nje wanawekeza kwao sisi bado tupo na Uraia wa nchi moja. Ukitoka nje unaonekana beberu. Kusajili YouTube channel hela, kurusha drone hela,tunazuia ndoto za vijana bila sababu ya Sera za kijinga.
Kama wewe ni kijana na huoni haya ni hasara kwa Taifa. Dunia ishakuacha nyuma.