David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

Jamaa ni mweupe.
Ukopaji wa US na China unaendana na ukubwa wa uchumi wao, maendeleo ya kiviwanda na wingi wa wananchi walionao.
Tanzania ni nchi masikini na inazidiwa wingi wa wananchi kulinganisha na US au China, hata kipato cha mtu mmoja mmoja tunazidiwa mbali sana.

Hivyo kimahesabu Tanzania inakopa pesa nyingi zaidi kuliko US na China....

Ni sawa na mfanya biashara A mwenye biashara yenye mzunguko wa milioni 100 kwa mwezi akope milioni 200.
Halafu mfanya biashara mwingine B mwenye biashara yenye mzunguko wa milioni 1 kwa mwezi akope milioni 50.

Kati ya hao wawili, mmoja ana mkopo mkubwa lakini upo ndani ya uwezo wake, mwingine ana mkopo mdogo lakini kwa uchumi wake atahangaika sana kurejesha.

Hivyo kimahesabu Tanzania inakopa pesa nyingi sana sana. Wasitake kutuona sisi hatuna akili.
 
Huyu ni kichwa kwenye nchi ya Wapumbavu, Marekani wanakopa yes je wanakopa kufanhia ujinga kama huu wetu? au China wanakopa kufanyia ujinga
 
Sawa ungeleta evidence Sasa ya ulichokiandiaka
 
Kafulila ni hazina kwa Taifa
 
Nashauri mama akiondoka atuachie Kafulila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…