Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa.

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo, yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana.
Nasikia watu wanasifia bamia
 
Kuna mahala niliona video;
1. Chukua ndizi 1 iliyokomaa Vzr
2. Ichomee hadi iwe kama mkaa iungue
3. Saga/ponda iwe unga
4.chukua unga huo changanya na asali
5. Tumia asbh, mchana na jioni kwa siku 14-20 utapona kbs.

Angalizo;
Try it on your own risk.
 
Aisee pole sana mkuu Ila inatakiwa ujue vidonda Aina gani unavyo kwani Kuna vidonda vinavyotokana na kurithi,Kuna vidonda vinavyotokana na bacteria,na Kuna vidonda vinavyotokana na kuto kula kwa wakati na stress,,kwa vidonda vya kawaida kunywa amoxlyn vidonge 4 kila baada ya masaa 12 kwa mda wa 1week n.k,changanya na omiprazole 1 kutwa mara 2 kwa mda wa wiki moja Ila kitaalamu unashauriwa utumie kidonge 1 kwa mda wa wiki nane,Kama vinatokana na bakteria utatumia omiprazole na fragile,, kingine acha stress acha kula nyama nyekundu acha kunywa mijuisi ya kiwandani,acha kula dagaa,maharage n.k,kula kwa wakati ,pendelea kunywa maji ya vugu vugu ,kunywa lita 3 kwa siku ili kulainisha mfumo wako watumbo
 
Nilishawahi kuugua vidonda vya tumbo. Nimepona kwa kula pilipili kali za mwendokasi.

Watu wengine wenye uelewa wa haya mambo watakuja kufafanua tiba ya pilipili.

Hunijui sikujui sina sababu ya kukudanganya
Ulikua unatumiaje maana nkila tu chakula chenye pilipili naumwa Sana tumbo
 
Kutafuna Karanga mbichi.

Siezi sema nimepona kabisa ila Tangu nitumie ni moja imeniondolee maumivu nlokuwa nayapata ya vidonda tumboni.

Pia nimezingatia ulaji wa chakula ambao Tumbo langu haloliendani navyo na kula kwa wakati.

Ila Asilimia 80 karanga mbichi imenisaidia sana.

Kabla ya hapo ilikuwa niamke kwa maumivu ya tumbo sa 10 usiku nitafute kitu cha moto itulie. Ila baada ya karanga naweza fika hata sa nne sijala kitu na nikawa sawa.

Huwa natafuna karanga muda ambao chakula kimeshapungua tumboni natafuna maji yake nameza.

Nilitumia dawa nyingi za kienyeji ila niliona zinanizidishis hali ila kwenye Karanga mbichi Ndo nilipo patia ahueni yangu.
 
Back
Top Bottom