Usiku wa kuamkia tarehe 17 Mwezi November mwaka jana niliugua maumivu makali ya tumbo.
Asubuhi nikajitosa moja kwa moja kwenda zahanati kupima.
Vipimo vikaja kama ifuatavyo
View attachment 2976749
Kwa maelezo ya daktari ni kuwa nikisumbuliwa na magonjwa mawili. Vidonda vya tumbo na Typhoid.
Nilipata ukakasi kwenye Typhoid kwasababu circle yangu ya maisha nimekuwa mtu makini sana kwenye usalama wa vyakula na maji.
Nikaandikiwa dawa hapo kama shilingi 25K kwa ajili ya kutibu magonjwa yote mawili, lakini nikawajibu kuwa kwa saizi sina hela ngoja nikajipange.
Nilipotoka hapo nikachukua boda kwenda kwenye hospitali binafsi kwenda kupima tena kuhakiki.
Nilipofika pale nilichukuliwa vipimo vya damu na vipimo vilikuwa kama hivi.
View attachment 2976752
Daktari akanipa ufafanuzi wa kinacho nisumbua akiniambia kuwa ni vidonda vya tumbo pekee, hakuna ugonjwa mwingine zaidi ya huo.
Dawa akaniandikia gharama zake kuwa ni 99,000 nikasema ngoja nikajipange.
Nikaongea na ndugu yangu akanipa ushauri wa dawa moja ambayo aliwahi kuitumia mke wake.
Dawa hiyo ilikuwa inajina linalofanana na "morpezoel"
Lakini mimi mwenyewe sikuacha kujiongeza. Nika Google nikakutana na link ya uzi wa mtu ambaye alitoa ushauri wa kutumia bamia kama dawa.
Bamia unaziloweka kwenye maji zinakaa kwenye maji kwa muda wa masaa 8 kisha unakunywa yale maji yake kwa kutwa mara mbili.
Kwa kufanya hivyo ndio nimejikuta nimepona vidonda vya tumbo.