Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Nilikuwa siwezi kula mahindi ya kuchoma, siwezi kula maharage mfululizo, siwezi kula dagaa, siwezi pilipili,
Na maisha ya hapa nyumbani maharage ndio kwa sana,
Nilitumia kila aina ya dawa za kienyeji mfano mafuta ya kondoo, asali ya nyuki wadogo, juisi ya kabichi, maji ya vuguvugu kila asubuhi, na majanimajani naletewa nnayoambiwa , na kushauriwa kula kwa wakati kutoacha tumbo wazi,

mwisho nmepona sijui dawa iliyonponesha,, au kilicho ponesha , nakula vyote nlvyokuwa Sili, kinachomsumbua sasa ni kiungulia tu tena kinanisumbua nnapokula maharage alafu nisile tunda....
Namshukuru Mungu
Hongera sana
 
Members humu kwema? Kwa ambaye amepata dawa ya vidonda vya tumbo anifahamishe vinanitesa sana, hapa mwili umeisha, nimeshatumia madawa ya kila Aina sasa umeshaangusha hata uchumi wangu, inshort ni maumivu usiku na mchana hakuna amani , mwenye kujua dawa anisaidie tafadhari
Usiku wa kuamkia tarehe 17 Mwezi November mwaka jana niliugua maumivu makali ya tumbo.

Asubuhi nikajitosa moja kwa moja kwenda zahanati kupima.

Vipimo vikaja kama ifuatavyo
Screenshot_20240429-152609.png

Kwa maelezo ya daktari ni kuwa nikisumbuliwa na magonjwa mawili. Vidonda vya tumbo na Typhoid.

Nilipata ukakasi kwenye Typhoid kwasababu circle yangu ya maisha nimekuwa mtu makini sana kwenye usalama wa vyakula na maji.

Nikaandikiwa dawa hapo kama shilingi 25K kwa ajili ya kutibu magonjwa yote mawili, lakini nikawajibu kuwa kwa saizi sina hela ngoja nikajipange.

Nilipotoka hapo nikachukua boda kwenda kwenye hospitali binafsi kwenda kupima tena kuhakiki.

Nilipofika pale nilichukuliwa vipimo vya damu na vipimo vilikuwa kama hivi.
Screenshot_20240429-152929.png

Daktari akanipa ufafanuzi wa kinacho nisumbua akiniambia kuwa ni vidonda vya tumbo pekee, hakuna ugonjwa mwingine zaidi ya huo.

Dawa akaniandikia gharama zake kuwa ni 99,000 nikasema ngoja nikajipange.

Nikaongea na ndugu yangu akanipa ushauri wa dawa moja ambayo aliwahi kuitumia mke wake.

Dawa hiyo ilikuwa inajina linalofanana na "morpezoel"

Lakini mimi mwenyewe sikuacha kujiongeza. Nika Google nikakutana na link ya uzi wa mtu ambaye alitoa ushauri wa kutumia bamia kama dawa.

Bamia unaziloweka kwenye maji zinakaa kwenye maji kwa muda wa masaa 8 kisha unakunywa yale maji yake kwa kutwa mara mbili.

Kwa kufanya hivyo ndio nimejikuta nimepona vidonda vya tumbo.
 
Usiku wa kuamkia tarehe 17 Mwezi November mwaka jana niliugua maumivu makali ya tumbo.

Asubuhi nikajitosa moja kwa moja kwenda zahanati kupima.

Vipimo vikaja kama ifuatavyo View attachment 2976749

Kwa maelezo ya daktari ni kuwa nikisumbuliwa na magonjwa mawili. Vidonda vya tumbo na Typhoid.

Nilipata ukakasi kwenye Typhoid kwasababu circle yangu ya maisha nimekuwa mtu makini sana kwenye usalama wa vyakula na maji.

Nikaandikiwa dawa hapo kama shilingi 25K kwa ajili ya kutibu magonjwa yote mawili, lakini nikawajibu kuwa kwa saizi sina hela ngoja nikajipange.

Nilipotoka hapo nikachukua boda kwenda kwenye hospitali binafsi kwenda kupima tena kuhakiki.

Nilipofika pale nilichukuliwa vipimo vya damu na vipimo vilikuwa kama hivi.View attachment 2976752

Daktari akanipa ufafanuzi wa kinacho nisumbua akiniambia kuwa ni vidonda vya tumbo pekee, hakuna ugonjwa mwingine zaidi ya huo.

Dawa akaniandikia gharama zake kuwa ni 99,000 nikasema ngoja nikajipange.

Nikaongea na ndugu yangu akanipa ushauri wa dawa moja ambayo aliwahi kuitumia mke wake.

Dawa hiyo ilikuwa inajina linalofanana na "morpezoel"

Lakini mimi mwenyewe sikuacha kujiongeza. Nika Google nikakutana na link ya uzi wa mtu ambaye alitoa ushauri wa kutumia bamia kama dawa.

Bamia unaziloweka kwenye maji zinakaa kwenye maji kwa muda wa masaa 8 kisha unakunywa yale maji yake kwa kutwa mara mbili.

Kwa kufanya hivyo ndio nimejikuta nimepona vidonda vya tumbo.
Brother asante sana pia pole sana , ulitumia Kwa muda Gani? Ratiba ilikuaje asubuhi , mchana na jioni au? Ulikuwa unatumiaje na Kwa muda Gani?
 
Brother asante sana pia pole sana , ulitumia Kwa muda Gani? Ratiba ilikuaje asubuhi , mchana na jioni au? Ulikuwa unatumiaje na Kwa muda Gani?
Wiki Moja tu nilianza kuona changes

Asubuhi na jioni ndio ilikuwa dozi yake wakati huo ukiendelea kuepuka ulaji wa vyakula visivyo rafiki.

Lakini hayo yote yanaweza yasifanye kazi ikiwa wewe ni mtu wa stress muda mwingi.

Jitahidi kujichanganya na watu sehemu ambayo hautakuwa mpweke ili usiyape nafasi mawazo.
 
Kupona vidonda vya tumbo sio rahisi kwa sababu vipo ndani ya tumbo na tumboni kuna chemical na pia asilimia kubwa ya vyakula vina kemikal , ili upone lazima utafute namna ya kuepuka Vyakula vyenye kemikal na kula vyakula vyenye uwezo wa kukabiliana na acid ili vidondo vipate mda wa kupona.
Kama bado vinasumbua nicheki inbobo
 
Kinachosababisha vidonda vya tumbo ni Helicobacter pylori na sio stress wala aina ya chakula unachotumia.

Ninauza dawa za uhakika kutibu kabisa vidonda vya tumbo na kiungulia chote kinaisha.

Ukitumia hizi dawa unapona kabisa na utaweza kula chakula chochote ukipendacho.

Hii ni biashara, anayetaka aje PM
 
Mkuu usihangaike na hii kitu. Kuna jamaa yangu alinipa dawa free ikaniponya kabisa, naweza nikamuomba akusaidie na wewe.
Kama atakutoza haiwezi shilingi 5000. Nakutumia namba inbox.

Mkuu Chivundu , nami nahitaji msaada wako kwenye hili la vidonda vya tumbo.
 
Kinachosababisha vidonda vya tumbo ni Helicobacter pylori na sio stress wala aina ya chakula unachotumia.

Ninauza dawa za uhakika kutibu kabisa vidonda vya tumbo na kiungulia chote kinaisha.

Ukitumia hizi dawa unapona kabisa na utaweza kula chakula chochote ukipendacho.

Hii ni biashara, anayetaka aje PM
95% of my patients with PUD h pylori was negative
 
Back
Top Bottom