Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Una SHIDA ila hutaki kufuata maelekezo yeyote, kwa Maisha unayoishi unene utakuganda Sana.
 
Dawa ni Mtindo wa chakula unavyokula
1.Ningependa ununue mizani ya digital uwe nayo uweke chumbani ukitoka kuoga rekodi uzito uliopata asubuhi

2. Hakikisha umeacha Vilevi/Soda/Juice/Chai yenye sukari/Biskuti ambao ni ngano , kunywa chai bila sukari na michemsho ya asili au mayai mawili hata au moja tu

3. Mchana kula ugali na nyama ambayo haina mafuta au samaki na mboga za majani usile sana kula wastani wa kawaida

4. Vyakula vya kukaanga/wali usiku usile kula matunda tu sio mengi kwa kiasi na maji ya kunywa hakikisha kwa siku unakula mara moja tu ukifanya wiki utazoea utaona kawaida

5 ikifika wiki ukitoka kuoga pima utaona kuna gramu zimeshuka nenda hivyo wiki tatu utashusha gramu nyingi sana
 
Duh kwa wiki kilo 10 ayo si mauwaji
 
Tafuta Ozempic. Nje watu wengi wanatumia ozempic hivi sasa ila ukiacha bila kubadili lifestyle unene wote unarudi, the choice is yours. Uwe on Ozempic maisha yote au utumie for a little while then ubadili lifestyly. Kupanga ni kuchagua.
 
Unatakiwa ufanye kazi ya boda boda kama wiki mbili hivi mfululizo 😄 (just joking)
 
Miye nina kg 92 nahaingaika ni mwaka wa 3 huu ikipungua ni kg1
 
Safi
 
Tafuta muziki uwe unacheza huku unafanya mazoezi jioni na asubuhi halafu acha kula mafuta na sukari kwa wingi kisukari kipo njiani, oya umeacha zile pigo zako za kiwaki ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…