Dawa ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa!

Huu upumbavu upo Afrika tu [emoji3]
Fuatilia rekodi na historia ya top ya matajiri duniani wanaotumia njia hiyo sana.

Wenzio wamevuka KANUNI ya Kutoa ZAKA ya 1/10 wanatoa Hadi ZAKA ya 7/10 wewe hata ZAKA ya 1/10 unashindwa.

Nenda kaangalie matajiri wa Dunia wanatoa Bei Gani Kwa asasi zinazosgughulika na wajane na maskini duniani utarudi kuniambia.

Afrika pia tusipobadilika kurudi kuanza Kutoa Kwa wengine ,tutabaki tulipo.

Kutoa ni KANUNI Mungu ameweka Ili kupokea. Ficha vipesa vyako uvunguni uone kama utatoboa.
 
Kuna sehem niliona maandishi kua usimtafute mchawi Lipa zaka
 
Ukipeleka sadaka Yako Kwa manabii wa uongo imekula kwako,

Peleka sadaka pale muhimbili Kuna wazazi hawana pesa watoto wao wafanyiwe operation,

Peleka sadaka Kwa wajane, au somesha yatima.

Mungu atakubariki sana.

Amen
Kazi kweli
 
Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Haikuhusiana na kutoa
Hapa ilikuwa kitu kingine kabisa,kisa Cha shetani na Yesu!
Luka 4 pale soma vzr
Halafu soma Malaki 10....
Utaona tofauti yake
 
Ni kweli mkuu!

Hawa vijana wanaosoma sekondari ambao huishiwa wakati mwingine ukiwalisha chakula hakikauki ndani yaani huja na kufurika!!
 
Sadaka sahihi, sehemu sahihi, yenye Iman sahihi inamajibu makubwa zaidi kwako binafsi au hata na uzao wako. Mfano Sadaka ya Malimbuko, watu hawajui tu hii ni ulinzi mkubwa sana na ina baraka za ajabu katika ajira zenu.
 
Haikuhusiana na kutoa
Hapa ilikuwa kitu kingine kabisa,kisa Cha shetani na Yesu!
Luka 4 pale soma vzr
Halafu soma Malaki 10....
Utaona tofauti yake
Basi sawa, itakuwa kweli Biblia inajikanganya.
 
.
 
Nani amemjaribu Mungu Kwa matoleo na aje kutupa ushuhuda?

Usipotumia njia hiyo na upo katika ukata wa kifedha, utazidi kudidimia.

Mjaribu Mungu kupitia matoleo.

Amen
 
Tarehe 4/4/2024 nimepata kingine Cha kushuhudia kupitia kumjaribu Mungu Kwa matoleo.

Nina nyumba za kupangisha, ikapita kipindi Cha karibia wik mbili bila kupata mpangaji mpya baada ya waliokuwepo kuhama,

Nilipigiwa simu Kutoka Kwa Mchungaji mmoja mwenye huduma changa aliyeniomba nimchangie pesa kutimiza hitaji Fulani,

Nilimwambia, nakumbuka AHADI niliyokuahidi, ila napata changamoto ya kukosa wapangaji ,niombee,

Wakati namjibu hayo, ilikuwa saa nne asubuhi, ulipofika saa Moja jioni, alikuja mtu akapenda nyumba na kulipia hapo hapo rent ya miezi mitatu.

Nikisema Kweli Mungu unajibu maombi, pale pale nilituma pesa Kwa Mchungaji na kushukuru Kwa maombi.

Tumjaribu Mungu Kwa matoleo, anajibu.

Amen
 
Kwa hii habari ya sadaka, Mungu alinisemesha jambo Moja muhimu sana; tusitoe sadaka kama rushwa ili Mungu atutendee jambo fulani Kwa maana rushwa ni adui wa haki na Mungu katu hapokei rushwa. Rushwa wapeni wanadamu lakini si MUNGU. Unapotoa sadaka jiulize kama hiyo sadaka ni SHUKRANI au ni RUSHWA!!?? Ukiona umetoa sadaka na haupati majibu jua kabisa sadaka Yako ilikuwa na viashiria vya rushwa. Sadaka inaweza kuwa na viashiria vya rushwa kama imetolewa Kwa shinikizo la nje, imetolewa Mahali pasipo sahihi au watu sahihi, imetolewa wakati usio sahihi, imetolewa Kwa Nia isiyosahihi( hatupati kwasababu twaomba vibaya), imetolewa ungali ukiwa na uchungu na watu, imetolewa pasipo kuambatana na Toba( hakuna aliye mwema, mwema ni Mungu tu). Sadaka inaweza kuwa na viashiria vya shukrani ikiwa; utaongozwa na roho mtakatifu pasipo shinikizo la nje, utakuwa na amani wakati wa utoaji, itaendana na maelekezo aliyotoa Mungu mwenyewe, sadaka sahihi na Mahali sahihi n.k .Ukitoa sadaka kama shukrani mbele za Mungu inalipa sana.
 
Usitukane,

Nenda kamjaribu Mungu Kwa kuwanunulia chakula yatima wanaorandaranda usiku huu Kwa akiba ndogo iliyo nayo ukimjaribu Mungu sawasawa na (Malachi 3:10-12).

Amini nakuambia, utajibiwa haraka sana, na utarudishiwa zaidi ya ulichotoa.

Amen
Umejibu vyema! Hekima hii idumu kwako milele
 
Umenena vyema,

Sadaka haipaswi kuchukua viashiria vya RUSHWA,

Mada imelenga zaidi utoaji wa kumjaribu Mungu kama ambavyo ameruhusu katika maandiko.

Ubarikiwe 🙏
 
Ulivyo muingiza mwakasenge nimepuuza uzii.wewe ndo walewalee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…