Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Taarifa nilizopata kutoka kwenye chanzo changu cha kuaminika ni kwamba, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi baada ya jitihada za kukimbia na kujificha kushindikana.

Mbowe amekamatwa maeneo ya Mikocheni ambako alienda kujificha ili asikamatwe na Jeshi la Polisi.

Kwa sasa wapo njiani kuelekea Central ambako atahojiwa kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kulisababishia usumbufu na gharama jeshi la polisi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Mbowe amekamatwa akitolewa kwenye Appartment Moja kwenda nyingine akitumia gari Nyeusi, Tinted yenye namba za usajili T 830 DEW aina ya VX. Wamemkamata akiwa nje ya geti ya Appartment hiyo ambayo ni miongoni mwa majengo ya siri ( Safe House) yanayomilikiwa na CHADEMA

MBOWEE.png
 
Kumekucha, hivi logic ya kumshikilia mtu masiku mengi huwa ni ipi? Na ile sheria ya masaa 24 huwa kuna namna polisi wana-bypass? Naomba kujuzwa kwa ufahamu wangu maana mtu kama Manji ameshindwa, sie makapuku tusio na wanasheria najiwazia!
Sio kila kesi masaa 24
 
Hahahhahahah naona mnafurahia wanaCCM ila aliaye wa kwanza huwa anacheka zaidi kuliko achakae wakwanza.Kuna siku haya mtashindwa hata kuyabeba.

Muda ni dawa,ila nina uhakika haya mnayoyafanya mtakuja kuyajutia baadaye.Nina uhakika hata Sirro anafanya haya sababu anatetea kitumbua chake tu
mentality za kuonewa ni kwa sababu ya kukoswa kitu cha msingi cha kusimamia.
Sasa kasingiziwa kwa maelezo yako, anaogopa nini kama hana tatizo. Kama kuna hila basi si atatoka akashtaki kesi nyingine ya pili, mpinzani gani muoga hivyo mkuu. Unabii na utabiri uweke kando kwanza, ngoja tuache watu wafanye kazi zao kama hana hatia ataendelea na mambo yake... uoga ni epidemic angalia usijekuwa muhanga
 
Nimesikitishwa sana na tukio la kukamatwa kwa mheshimiwa mbowe. Nimekaa nikajiuliza shida ni nini hasa mpaka ukamatwe kwa nguvu wakati amepewa mda mrefu kwenda kituo cha police kuhojiwa tu. Yafuayayo ni maswali niliyojiuliza labda wenzangu mnaweza kunipatia majibu.

1. Kwanini kama mheshiwa mbowe kama
hausiki vyovyote na shutuma za madawa ya kulevya asitesite kwenda police?

2. Kama njia aliyoitiwa sio sahihi kwanini watuhumiwa wengine wameenda bila shaka na wengine kuachiwa?

3. Au mheshimiwa Mbowe alitaka akamatwe huku akimulikwa na kamera ili iwe ushujaa kwa wafuasi wake?

4. Kwanini ajifiche kama anajihisi ni msafi na hana hatia?

Ndugu za haya maswali kwa MTU mwenye akili timamu ya kufikiri lazima ajiulize bila kujali itikadi ya chama uliyonayo. Tulitegemea mheshimiwa mbowe kuwa kioo na kuwa na taswira nzuri mbele ya macho ya watu kama kiongozi mkuu wa upinzani. Nawasilisha.
 
Kuna siku unayofurahia leo kesho utakuja kulia ukose hata wa kukusemesha.As long as anajiamini hatumii madawa sioni shida.
Tatizo maelezo kutoka juu. Wewe na mimi hatujui. Ila ninachojua huu upuuzi una mwisho.
 
Haya, kakamatwa at last. Ngoja nipitie kwenye masoko nione kama nafaka zimeshuka bei!
 
Wala hajimalizi kisiasa,Inawezekana pia amepelekewa summons na akaenda mwenyewe,hivyo sishangai UVCCM akija na mbia kama vile amefumaniwa.Ila Kesho mumsindikize Mkuu wa Mkoa Mahakamani.
Polisi hawana summons hiyo hutolewa mahakamani kwenye kesi ya madai au kwa shahidi.
 
Nimesikitishwa sana na tukio la kukamatwa kwa mheshimiwa mbowe. Nimekaa nikajiuliza shida ni nini hasa mpaka ukamatwe kwa nguvu wakati amepewa mda mrefu kwenda kituo cha police kuhojiwa tu. Yafuayayo ni maswali niliyojiuliza labda wenzangu mnaweza kunipatia majibu.

1. Kwanini kama mheshiwa mbowe kama
hausiki vyovyote na shutuma za madawa ya kulevya asitesite kwenda police?

2. Kama njia aliyoitiwa sio sahihi kwanini watuhumiwa wengine wameenda bila shaka na wengine kuachiwa?

3. Au mheshimiwa Mbowe alitaka akamatwe huku akimulikwa na kamera ili iwe ushujaa kwa wafuasi wake?

4. Kwanini ajifiche kama anajihisi ni msafi na hana hatia?

Ndugu za haya maswali kwa MTU mwenye akili timamu ya kufikiri lazima ajiulize bila kujali itikadi ya chama uliyonayo. Tulitegemea mheshimiwa mbowe kuwa kioo na kuwa na taswira nzuri mbele ya macho ya watu kama kiongozi mkuu wa upinzani. Nawasilisha.
kwani hujui hana kosa, serikali haijaanza Leo kumtafutia visa,
 
Kumpima leo na kumkuta na madawa mwilini siyo rahisi ...... yaani week mbili baada ya kuanza hii kampeni? Unless kama ni mtumiaji basi aliendelea kutumia hata baada ya kusikia akina Manji wamepimwa. Kama ni mtumiaji na hajatumia muda huu wote basi vipimo vya damu au mkojo vitakuwa negative. Vipimo vikubwa kama vya vywele ...... Mkemia Mkuu hana huo utalaam!!

All in all namuonea huruma Mkemia Mkuu kwenye hizi kesi!!
kama hana shida naamini ataendelea na maisha yake sasa kwa nini hofu inakuwa kubwa sana utadhani anakwenda kusulubiwa
 
Back
Top Bottom