Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa



 
Kumekucha, hivi logic ya kumshikilia mtu masiku mengi huwa ni ipi? Na ile sheria ya masaa 24 huwa kuna namna polisi wana-bypass? Naomba kujuzwa kwa ufahamu wangu maana mtu kama Manji ameshindwa, sie makapuku tusio na wanasheria najiwazia!
Sio kila kesi masaa 24
 
mentality za kuonewa ni kwa sababu ya kukoswa kitu cha msingi cha kusimamia.
Sasa kasingiziwa kwa maelezo yako, anaogopa nini kama hana tatizo. Kama kuna hila basi si atatoka akashtaki kesi nyingine ya pili, mpinzani gani muoga hivyo mkuu. Unabii na utabiri uweke kando kwanza, ngoja tuache watu wafanye kazi zao kama hana hatia ataendelea na mambo yake... uoga ni epidemic angalia usijekuwa muhanga
 
Nimesikitishwa sana na tukio la kukamatwa kwa mheshimiwa mbowe. Nimekaa nikajiuliza shida ni nini hasa mpaka ukamatwe kwa nguvu wakati amepewa mda mrefu kwenda kituo cha police kuhojiwa tu. Yafuayayo ni maswali niliyojiuliza labda wenzangu mnaweza kunipatia majibu.

1. Kwanini kama mheshiwa mbowe kama
hausiki vyovyote na shutuma za madawa ya kulevya asitesite kwenda police?

2. Kama njia aliyoitiwa sio sahihi kwanini watuhumiwa wengine wameenda bila shaka na wengine kuachiwa?

3. Au mheshimiwa Mbowe alitaka akamatwe huku akimulikwa na kamera ili iwe ushujaa kwa wafuasi wake?

4. Kwanini ajifiche kama anajihisi ni msafi na hana hatia?

Ndugu za haya maswali kwa MTU mwenye akili timamu ya kufikiri lazima ajiulize bila kujali itikadi ya chama uliyonayo. Tulitegemea mheshimiwa mbowe kuwa kioo na kuwa na taswira nzuri mbele ya macho ya watu kama kiongozi mkuu wa upinzani. Nawasilisha.
 
Kuna siku unayofurahia leo kesho utakuja kulia ukose hata wa kukusemesha.As long as anajiamini hatumii madawa sioni shida.
Tatizo maelezo kutoka juu. Wewe na mimi hatujui. Ila ninachojua huu upuuzi una mwisho.
 
Haya, kakamatwa at last. Ngoja nipitie kwenye masoko nione kama nafaka zimeshuka bei!
 
Wala hajimalizi kisiasa,Inawezekana pia amepelekewa summons na akaenda mwenyewe,hivyo sishangai UVCCM akija na mbia kama vile amefumaniwa.Ila Kesho mumsindikize Mkuu wa Mkoa Mahakamani.
Polisi hawana summons hiyo hutolewa mahakamani kwenye kesi ya madai au kwa shahidi.
 
kwani hujui hana kosa, serikali haijaanza Leo kumtafutia visa,
 
kama hana shida naamini ataendelea na maisha yake sasa kwa nini hofu inakuwa kubwa sana utadhani anakwenda kusulubiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…