Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Nashauri wampeleke Kisongo kwa mwenzie wakati wanafanya upelelezi
 
Hii yote ni kwa ushauri wakijinga wa tundulisu.
 
Vipi hao polisi watamchukulia lini hatua yule aliyeuza nyumba za serikali alipikuwa waziri?

Kila mkakati manoanzisha mnaishia kukwama hata huu nao tayari mshatumbukia
Na vipi yule waziri aliyenunua ile pantoni mbovu? Na yule waziri aliye tupigisha mkenge kwa ile meli ya kuvulia samaki?
 
Kuna uwezekano mkubwa yaliyomkuta Manji yanaweza kumkuta pia Mbowe, kwa style hii ni vigumu sana kupambana na vita vya madawa ya kulevya.

Ni vigumu Sana mkuu! Hao wanao jinasibu kuwa ndiyo vinara wakupambana wanaleta mzaha vitani ,utasjindaje?
 
Naomba kuuliza, eti kakutwa kwa kimanda, taarifa zilivuja baada ya K kupiga selfie na kutupia facebook? Wabongo kwa uongo ni mwisho.
 
Unaonekana ubongo umeganda kwa kupiga ramli
 
*mkuu umekodishwa..pengine umekuwa "mixer ya zege"...Tanzania hamna "jengo/hifadhi ya siri",au "banker"...ni nchi chache sana duniani ndo zinayo
 
Unakula pensheni yako ya buku 7 perdiem hapo Lumumba basi unajiona na wewe ni mwenye nchi unasahau shida zako zote za kijijini hakika Tanzania ni pagumu sana kuishi.
 
Yaani labda vipimo lakini kwa upande wa NYARAKA TANGU AITWE MPAKA LEO AWE BADO ANAZO TU MIMI SI DHANI.

Akikutwa nazo wamembambikia.
Hakuna mtu mzembe kiasi hicho.
hata kama kweli yalikuepo deki ya maana lazima imepita
 
Hii Vita ni nzuri sana nafikiri wataokoa vijana wetu wengi kwani ndo nguvu kazi Ya taifa lakini ops hii kuna watu wamekamatwa kama chambo lakini kuna watu naona kabisa wamekamatwa kama chambo lakini kuna walengwa wakubwa wanatafutwa! Kuna mtu ataongezewa vikesi ili vimtie hatiani na wengine kuachiwa ukizingatia ukamataji ulivyoenda na masogange katika list zote mbili hakuwemo kaingizwa ili awatulize munkali waliokuwa wakihoji mbona hayumo kwa baadae bwa sababu zao ndo akaitwa polisi na kwensa kumsachi, na haiwezekani akutwe na madawa ya kulevya ndani asiweze kuyaficha wakati anajua wazi mda wwt ataitwa na kupekuliwa! Hiyo haiwezekani ila kuna mtu anatafutwa kwa gharama kubwa!
 
Polisi bwana tokea wamtanganze,yeye kwani mjinga aache ushahidi ndani?

Tukisema Jeshi la Police Tanzania linahitaji ' mabadiliko ' makubwa ya kuanzia mfumo wake hasa wa Kiuweledi wengine tunaonekana ' Wachochezi '. Kama Mtoto mdogo tu asiyekuwa na ufahamu mkubwa akiona unaanza ' kumtishia ' au kumpiga ' mkwara ' huwa anajipanga kabisa na unaweza hata siku uliyopanga ' kumtandika ' akakutoroka vile vile sembuse leo mnajifanya kwenda ' kumpekuwa ' Mbowe mkidhani kuwa mwenzenu pengine ni ' Ngumbaru ' kama nyie na mtakamata chochote kitu. Tunachowaombeni tu kwakuwa tayari mmeshaonyesha ' udhaifu ' wenu wa Kiutendaji tunaomba tu mumtendee haki na msije mkaingia huko Kwake na Kete za Bangi au mifuko ya Unga ili ' mumbambikie ' Kesi ' kiaina.

Police Tanzani hivi huko TPC mnakokuwa Kozi huwa mnafundishwa kweli ' Medani ' za Kimakakati au huwa mnaenda ' kuzuga ' tu?
 
Walengwa wa madawa ya kulevya hawajafikiwa kwa sababu wanatumia karatasi za Makonda ambaye ndiye mpika dili ya kila kinachofanyika. Natamani sana kuiona Tanzania yangu ile ya zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…