Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Mbona mnamsemea mhusika! Tusubiri kauli yake kabla na baada ya kuwa kituo cha Polisi, kama walivyofanya wengine akiwemo Mch Gwajima. Tukumbuke aliiitisha wanahabari kabla kuwa hatokwenda, akaungwa mkono na wafuasi wake.
 
watanzania sie waoga....hatuwez kufikia yaliyotokea Rwanda au Burundi..so achana na habari za kumwaga damu! hakuna atakaye mwaga damu rabda amwage jasho
Jiongopee Mkuu, Cyprus walimwaga damu, endelea na ujinga wako.
 
Makonda amepata wapi pesa za kununua Lexus, Benz, na kujenga maghorofa na kununua apartment kama ilivyosemwa na wabunge? nani wa kumchunguza makonda kama na yeye anajihusisha na biashara za madawa ya kulevya au la?
 
... Hili bandiko linanikumbusha lile tangazo la Vodacom la kudata.. mtu anaulizwa Jina lako nani anajibu kuku akipanda baiskeli ana mbio.. Jikite kwenye hoja.
 
Hivi hayo yote maovu ya vyama bado yanapita na kusabanishwa na sheria za vyama ya Tanzania. Je hakuna haja ya kuangalia mienendo ya vyama na kufanya kitu, kwa nini tunatuhumu na kulalamika tu.
 
Chadema bana Mara wanakanusha hakukamatwa alijipeleka Mara wanakiri kakamtwa daah
 

Mimi sijalala kila nikiwaza makonda ni nani sipati jibu,bigup mbowe wewe ni HERO
 
We huna Akili, eti hii vita ya madawa ni ya chadema! Unataka kutuambia akina Wema, TID, Manji(diwani wa ccm) hao wote ni chadema? Uwe unatumia angalau sehemu kidogo ya ubongo wako iliyobakia kuacha mihemko na kuwa mkweli. Ovyo sana wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…