DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Tumelichukua tutakupa mrejesho
 
Kazi ya kulaza mabomba ikikamilika tutaanza kuwatangazia wananchi waje kuunganishiwa huduma ya Maji
 
Dawasco tunafanya maunganisho chini ya mita 100 . Kwa wale walio mbali na umbali huo tunawashauri kuomba mradi kabisa wa eneo lao ili gharama isiwe kubwa sana.
 
naomba kufahamu mtu anatakiwa aache umbali wa kiasi gani toka eneo ambalo bomba lenu kubwa na maji masafi limepita kwa maeneo ya Tabata Chang'ombe
 
Hongereni sana kwa jambo hili.
Sikujua kama na nyinyi ni member humu, kumbe mko kitambo tu tangu 2010??

Nazishauri taasisi nyingine ziige mfano huu wa kuwa na accounts kwenye mitandao ya kitanzania badala ya kwenda twitter na Instagram na Facebook
 
Hongereni sana kwa jambo hili.
Sikujua kama na nyinyi ni member humu, kumbe mko kitambo tu tangu 2010??

Nazishauri taasisi nyingine ziige mfano huu wa kuwa na accounts kwenye mitandao ya kitanzania badala ya kwenda twitter na Instagram na Facebook
Asante sana
 
Tupatie jina ulilotumia kuombea maji na kituo cha dawasco ulichoombea
 
Jaman wanajamvi

Naomba sanaaa kama kuna mtumishi DAwasco PWANI anisaidie naitaj kuunganishiwa maji nipo kongowe ya baada ya mbagara ya rangi Tatu!
Bado hatujafikisha huduma kongowe..kuna huduma ya visima huko
 
Makumbusho kijitonyama hatuna maji karibia wiki sasa, kulikoni
 
Tangu december nimekuwa nikipata bill sizielewi elewi. Lakini kwa kawaida bill ina range 15,000 - 25/30,000 kulingana na watu ninaoishi nao ndani. Sasa nashangaa leo nimeletewa bill 79,000? tena watu wamepungua sana kwangu kwa lipi? namba ni 90071710 KAwe
 
Nawezaje kupata bill yangu ya maji? Situmiwi notification kwenye simu huu mwezi wa nne sasa
 
Ivi Dawasco Tabata wako serious kweli? Kama mmeshindwa kununua hizo rola za bomba za maji kutoka St Rosalia kufikisha kwa wananchi zaidi ya 100 waliokwisha jaza fomu huu sasa mwaka basi njooni mtuchangishe tununue ili tupate maji. Ni aibu kwenu kama ofisi pale mlipoliachia bomba wakati mnajua walioomba waliko.
 
Tunafuatilia tutakupa mrejesho
 
Tena Bora nimewaona,
Ukweli mmeniboa sana aisee,
Iko hivi, mimi niliacha kutumia maji yenu nikachimba kisima changu mwaka 2010, nanyi mkawa kila mkileta bili kuanzia hapo inasoma zero,

Juzi kati hapa mmekuja kubadilisha mita mnaniletea bili ya laki 2, eti mnadai miaka yote hiyo maji yalikua yakivuja taratibu, cha ajabu nimewaomba mnipatie au mnionyeshe hiyo mita iliyoonyesha hiyo bili ya laki 2 ili nizione hizo units zilizovujia chini mnadai haipo na haionekani, hii si sawa kabisa.

1) Kwanini wakati mnaibadilisha mita msingenionyesha nikaiona? nitaamini vipi kama kweli maji hayo yalipita kwenye mita yangu na hamjanibambikia?
2) Na nitalipiaje maji ambayo yamevujia chini sijayatumia?
3) Kwanini miaka yote hiyo maji yanapita kwenye mita na kuvuja mlikua mnaleta zero bili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…