DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

MBONA HUKU TABATA KISUKURU ENEO LA KILIMANJARO BAR KUNA TATIZO LA MUDA MREFU LA MAJI LAKINI HAKUNA SULUHISHO LICHA YA SISI WAKAZI KUTOA MALALAMIKO DAWASCO TABATA KILA MARA? MAJI YANATOKA MARA MOJA KWA MWEZI NA KILA TUNAPOWASILIANA NA WAHUSIKA BW. MAKELELE, BWANA PASCO NA INJINIA WAO JIBU NI LILE LILE KILA SIKU "KUNA MATENGENEZO KIMARA". KWA VILE SUALA HILI NI LA MUDA MREFU TUNATUMIA NJIA HII KWA SASA NA IKISHINDIKANA TUNAOMBA KWA RIDHAA YENU DAWASCO ILI TUUSHIRIKISHE UONGOZI WA MKOA TUPATIWE UFUMBUZI WA KUDUMU
Tumelichukua tutakupa mrejesho
 
kwanza nawapa pongezi kwa Kazi nzuri mlioifanya ya kutandaza mabomba ktk maeneo mbali mbali ya DSM na Pwani,
nataka kujua taratibu ili niweze kuunganishwa kupata Huduma ya maji nyumbani, maana tangu mradi huo ukamilike mwaka jana hadi leo sioni kinacho endelea wala sijaona dawasco wakitoa taarifa
Kazi ya kulaza mabomba ikikamilika tutaanza kuwatangazia wananchi waje kuunganishiwa huduma ya Maji
 
Mm nipo bunju A usalama
Mtandao wa maji umeishia pale kwenye kanisa la EFATHA, yaani bomba kubwa
Kutoka pale kanisani mbaka nyumbani kwangu ni umbali wa Mita kama 100
Ili nipate maji inahitajika niunganishiwe bomba kubwa kutoka pale EFATHA Kushuka bonde mbaka chini pale ni kama mita 50
alafu mm niunganishe tena hiyo mita 50 nyingine kwa bomba la kawaida dogo
Sasa Basi nilitaka kujua Coast yake endapo nitahitaji maji nyumbani kwangu yafike
au unanipa ushauri gani ? Kwa sababu huduma ya kuunganishiwa maji naitaka kweli kweli na pesa ninayo.
Dawasco tunafanya maunganisho chini ya mita 100 . Kwa wale walio mbali na umbali huo tunawashauri kuomba mradi kabisa wa eneo lao ili gharama isiwe kubwa sana.
 
naomba kufahamu mtu anatakiwa aache umbali wa kiasi gani toka eneo ambalo bomba lenu kubwa na maji masafi limepita kwa maeneo ya Tabata Chang'ombe
 
Hongereni sana kwa jambo hili.
Sikujua kama na nyinyi ni member humu, kumbe mko kitambo tu tangu 2010??

Nazishauri taasisi nyingine ziige mfano huu wa kuwa na accounts kwenye mitandao ya kitanzania badala ya kwenda twitter na Instagram na Facebook
 
Hongereni sana kwa jambo hili.
Sikujua kama na nyinyi ni member humu, kumbe mko kitambo tu tangu 2010??

Nazishauri taasisi nyingine ziige mfano huu wa kuwa na accounts kwenye mitandao ya kitanzania badala ya kwenda twitter na Instagram na Facebook
Asante sana
 
Aisee niliomba kuunganishiwa maji akaja surveyor nikafuata baada ya week makadirio ya bei nilipe hadi leo week ya nne mara fomu yako iko kwa engineer mara kwa manager mara kwenda na kurudi.Najiuliza hivi watu wako serious kweli hadi lini hiyo fomu itakuwa tayari maana napoteza nauli zangu na muda bure kwa kitu ambacho mnaweza kufanya hata kwa dakika kumi.
Tupatie jina ulilotumia kuombea maji na kituo cha dawasco ulichoombea
 
Jaman wanajamvi

Naomba sanaaa kama kuna mtumishi DAwasco PWANI anisaidie naitaj kuunganishiwa maji nipo kongowe ya baada ya mbagara ya rangi Tatu!
Bado hatujafikisha huduma kongowe..kuna huduma ya visima huko
 
Makumbusho kijitonyama hatuna maji karibia wiki sasa, kulikoni
 
Tangu december nimekuwa nikipata bill sizielewi elewi. Lakini kwa kawaida bill ina range 15,000 - 25/30,000 kulingana na watu ninaoishi nao ndani. Sasa nashangaa leo nimeletewa bill 79,000? tena watu wamepungua sana kwangu kwa lipi? namba ni 90071710 KAwe
 
Nawezaje kupata bill yangu ya maji? Situmiwi notification kwenye simu huu mwezi wa nne sasa
 
Ivi Dawasco Tabata wako serious kweli? Kama mmeshindwa kununua hizo rola za bomba za maji kutoka St Rosalia kufikisha kwa wananchi zaidi ya 100 waliokwisha jaza fomu huu sasa mwaka basi njooni mtuchangishe tununue ili tupate maji. Ni aibu kwenu kama ofisi pale mlipoliachia bomba wakati mnajua walioomba waliko.
 
Ivi Dawasco Tabata wako serious kweli? Kama mmeshindwa kununua hizo rola za bomba za maji kutoka St Rosalia kufikisha kwa wananchi zaidi ya 100 waliokwisha jaza fomu huu sasa mwaka basi njooni mtuchangishe tununue ili tupate maji. Ni aibu kwenu kama ofisi pale mlipoliachia bomba wakati mnajua walioomba waliko.
Tunafuatilia tutakupa mrejesho
 
Tena Bora nimewaona,
Ukweli mmeniboa sana aisee,
Iko hivi, mimi niliacha kutumia maji yenu nikachimba kisima changu mwaka 2010, nanyi mkawa kila mkileta bili kuanzia hapo inasoma zero,

Juzi kati hapa mmekuja kubadilisha mita mnaniletea bili ya laki 2, eti mnadai miaka yote hiyo maji yalikua yakivuja taratibu, cha ajabu nimewaomba mnipatie au mnionyeshe hiyo mita iliyoonyesha hiyo bili ya laki 2 ili nizione hizo units zilizovujia chini mnadai haipo na haionekani, hii si sawa kabisa.

1) Kwanini wakati mnaibadilisha mita msingenionyesha nikaiona? nitaamini vipi kama kweli maji hayo yalipita kwenye mita yangu na hamjanibambikia?
2) Na nitalipiaje maji ambayo yamevujia chini sijayatumia?
3) Kwanini miaka yote hiyo maji yanapita kwenye mita na kuvuja mlikua mnaleta zero bili?
 
Back
Top Bottom