Tena Bora nimewaona,
Ukweli mmeniboa sana aisee,
Iko hivi, mimi niliacha kutumia maji yenu nikachimba kisima changu mwaka 2010, nanyi mkawa kila mkileta bili kuanzia hapo inasoma zero,
Juzi kati hapa mmekuja kubadilisha mita mnaniletea bili ya laki 2, eti mnadai miaka yote hiyo maji yalikua yakivuja taratibu, cha ajabu nimewaomba mnipatie au mnionyeshe hiyo mita iliyoonyesha hiyo bili ya laki 2 ili nizione hizo units zilizovujia chini mnadai haipo na haionekani, hii si sawa kabisa.
1) Kwanini wakati mnaibadilisha mita msingenionyesha nikaiona? nitaamini vipi kama kweli maji hayo yalipita kwenye mita yangu na hamjanibambikia?
2) Na nitalipiaje maji ambayo yamevujia chini sijayatumia?
3) Kwanini miaka yote hiyo maji yanapita kwenye mita na kuvuja mlikua mnaleta zero bili?