Dawasa Pwani acheni ubabaishaji, mnatuumiza na bill hewa tunalipia upepo maji hayatoki mita zinazunguka upepo ukipita, mnatulipisha bili kubwa tofauti na matumizi yetu ya maji, mfano unakuta kwa mwezi unaambiwa umetumia unit 75 za maji na maji hayajatoka wk takriban 2 au 3, ukienda kutoa hiyo shida hapa dawasa pwani unapewa majibu ya kuudhi na watoa huduma.
Halafu tulichogundua sisi wakaazi wa Mwanalugali tuliokuwa kwenye mradi wa maji wa wachina baadae dawasa wakauchukua huo mradi hawakufanya tathimini mfumo mzima wa maji hao wachina, ni kwamba mfumo mzima hawkufunga air valve kwenye mabomba yao kwa hiyo maji yakikatika yanaporudi huwa hewa inaanza kupita kwenye mabomba na mwisho inaishia kwenye mita zetu, kinachouma zaidi upepo ukipita kwenye mita huwa inazunguka kwa kasi ya ajabu sana na mita inasoma unit nyingi kwa muda mfupi na bili ikija huwezi amini utakoambiwa unakuta bili inasoma unit 120 au zaid kwa mwezi inauma sana kuona unaibiwa hivi na watu wamekaa oficn ukiwaeleza shida yako wanakununia sijui tuwaeleweje nyie dawasa?
Tumeshaliripotia sana hili tatizo lakini hakuna ufumbuzi wowote ule.
Tunazidi kuumia kwa kweli.
Na hadi navyo andika hii taarifa huku leo ni siku ya tano hakuna maji na hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa msg au radio, zaid mtakachokumbuka kutuma meseji ni kuhusu kulipa bili na sio kutatua matatizo yetu wateja.
Ama kweli nimeamini mteja wa dawasa kibaha hana thamani.
ASANTENI