Mimi ni Mteja wenu tangu 2016,ninaishi Kibaha P/Ndege.Mwanzoni wakati naanza kutumia huduma yenu nilikuwa naletewa bill ya Tshs 8,000/= hadi Tshs 12,000/= kwa mwezi.Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda naona naletewa bill kubwa wakati matumizi yangu ni yale yale.Sina bustani nnayonyweshea kusema imeongeza matumizi ya maji,kwangu hakuna leakage maungio yote yamekaguliwa,isitoshe pipe zilizotandazwa kwa ajili ya kusafirisha maji sehemu mbali mbali kwenye nyumba ni ile ya Class "C"haipasuki kirahisi hata pressure ya maji ikiwa kubwa.Mwezi May 2019 nililetewa bill ya Tshs 30,000/= na mwezi huu June 2019 nimeletewa bill ya Tshs 50,000/=.Mpaka sasa hivi sijalipa nataka J'3 nikaonane na Meneja wa Dawasa Mkoa wa Pwani, akishindwa kusolve tatizo langu nitakwenda ngazi ya juu zaidi ili kupatiwa ufumbuzi wa hili tatizo. Kuna haja ya kufanya Vetting kwa hawa wasoma mita kuna uwezekano mkubwa baadhi sio waaminifu badala ya kusoma na kurekodi Units sahihi zilizotumika anaongeza units na hivyo kupotosha mahesabu.Silipi hii bill mpaka nipatiwe maelezo ni kwa nini bill yangu inakuwa kubwa ilhali matumizi yangu ni ya kawaida kabisa. Nilimwambia rafiki yangu mmoja akashangaa sana bill niliyoletewa.Anasema yeye ana wapangaji Sita na wote wanatumia maji kwa shughuli zote za nyumbani lakini analipa kila mwezi Tshs 12,000/= ikizidi sana analipa Tshs 15,000/=.Nawauliza hao wanaohusika kwa nini kunakuwa na Double standard?