DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Naomba kujua gharama ya kuunganisha maji kimara , nyumba iliyo mita kama 70 kuanzia sehemu ilipopita bomba lenu

Pia naisikia kuna uwezekano wa kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha miezi kumi na miwili
 
Maji Taka yanatiririka Dar nzima, na nyie huwa mnakusanya malipo kwa huduma hiyo. Why, kwanini?
ndugu mwananchi. huduma ya Majitaka kwa jiji la Dar es salaam linalohudumiwa na Dawasco ni asilimia 13. maeneo mengi yaliyobaki wanachi wanatumia matanki yao ya kuhifadhi majitaka maarufu kama "Septic tank". tunakusanya malipo ya huduma ya majitaka kwa maeneo yenye mtandao wetu. hivyo basi tusaidie kujua eneo gani lenye kutiririsha Majitaka ili tukasafishe
 
Naomba kujua gharama ya kuunganisha maji kimara , nyumba iliyo mita kama 70 kuanzia sehemu ilipopita bomba lenu

Pia naisikia kuna uwezekano wa kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha miezi kumi na miwili
gharama itapatikana pindi mpimaji atakapofika na kufanya makadirio ya eneo lako. ni kweli tuko kwenye ofa ya maunganisho ya wateja wapya ambapo mteja ataunganishwa huduma ya Maji bure na atakuwa akilipa kidogo kidogo ndani ya miezi 12.
kwa mawasiliano ziadi tafadhali piga huduma kwa wateja dawasco kimara 0743 451865
 
Anayekadilia alifika akapima nikatumiwa taarifa kuwa inatakiwa shilingi laki tano apo kidogo nikasita nikaona gharama kubwa sana, nikahisi kama nataka kuibiwa vile
 
Hongereni sana Dawasco kwa huu uzi,mimi nlikua na maswali kadhaa ambayo kama tukipata majibu yake itasaidia sana.
1.Maeneo ya mbezi juu tuliwekewa mabomba kwenye mradi al maarufu kama mabomba ya wachina,ila tangu wayaweke hayo mabomba hayajawahi kutoa hata upepo,ila ni hapa jirani tuu maeneo ya Africana maji yapo mengi sana,ni kwa nini Dawasco wasiongeze pressure ya maji ili na sisi tuweze kupata huduma hii??

Asanteni.natumai tutapata majibu mubashara hapa jamvini.
Eneo la Mbezi juu,Ndumbwi,Baraza la mitihani na maeneo jirani hayapati huduma licha ya miundombinu yetu kwasababu ya mwinuko Mkali.Hivi sasa Tunajenga matenki makubwa lita milioni6 salasala (Kwa Mboma) sehemu yenye muinuko na yatatusaidia kuhudumia maeneo tajwa.
 
Anayekadilia alifika akapima nikatumiwa taarifa kuwa inatakiwa shilingi laki tano apo kidogo nikasita nikaona gharama kubwa sana, nikahisi kama nataka kuibiwa vile
gharama zote zinalipwa kwa njia ya bank. usikubali kutoa fedha yako kumpa mtu mkononi. kama umeshapewa makadirio tafadhali fika dawasco Kimara uweze kuingia mkataba wa kulipa huduma hiyo kwa mkopo wa miezi 12.
 
Maeneo mengi ya tabata kimanga, kisurukulu mabomba yanamwaga maji fanyeni myasibe
 
Hizo namba za huduma kwa wateja mlizoweka huwa hazipokelewi. Unaweza kupiga kutwa nzima na usijibiwe. Haya ni malalamiko ya baadhi ya Rafiki zangu waliopo Dar es Salaam
Hata mimi yamenikuta niko Dar
 
gharama zote zinalipwa kwa njia ya bank. usikubali kutoa fedha yako kumpa mtu mkononi. kama umeshapewa makadirio tafadhali fika dawasco Kimara uweze kuingia mkataba wa kulipa huduma hiyo kwa mkopo wa miezi 12.
Nashukuru sana
bahat mbaya nipo nje ya nchi ila nitawalazimisha walipaji wawe wananitumia risit
 
Kero kubwa niliyoiona ni kwa wateja wa mkataba! Ukilipa benki hawa-update taarifa mapema, matokeo yake wataendelea kukuletea bili inayojumlisha na pesa ulizokwisha kulipa! Kuna uwezekano mkubwa wa kulipa zaidi kuliko mkataba unavyotaka!
 
Kwanza niwape pongezi kwa kutengeneze hii thread ili muweze kuwasikiliza na kuwa karibu wateja wenu..Nina viwanja vyangu maeneo ya Goba...ila nimekuwa nikisita kuyaendeleza kutokana na kutokuwa na uhakika wa maji ya Dawasco. Katika maeneo yenye shida ya maji kwa Dar Goba ni eneo mojawapo. Mna mpango gani wa karibu na wa muda mrefu kusupply maji ya bomba kwa wakazi wa maeneo hayo
Hili swali halijajibiwa: Wakuu mmeliona hili
 
linapokuja swala la wafanyabiashara wakubwa zikiwemo ofisi kubwa mfumo wa malipo uboreshwe kuwa tofauti, ikiwa ninalipa kwa check inabidi niletewe bill yangu ya maandishi siku 14 kabla ili niweze ku-process malipo ktk utaratibu mzuri, utaratibu wenu mnatuma msg kitu ambacho si kithibitisho kizuri. nashauri utaratibu wa msg ufanyike kwa wateja wadogo wadogo.

Ameshakariri kuwa ukipata message kalipe ndani ya siku saba hajui kuwa kuna wateja wakubwa kulipa bili ni mpaka process na zote hulipiwa bank au kwa cheque. Yeye kakazanana Tigo pesa sijui mpesa.

DAWASCO chukua hii kama changamoto na muifanyie kazi kwa wateja wadogo sawa kwa utaratibu huo ila kwa wateja wakubwa jaribuni kufikiria njia mbadala.
 
DAWASCO Hoyeeeeeeee!,sasa nimekubali mmekomaaa,vyeti feki havipo sasa kwenye shirika na ndio maana mmethubutu kusikiliza kero za maji hapa JF great thinkers.
 
asante kwa taarifa..tunaomba utuelekeze ni maeneo gani kwa pale Ubungo Terminal
Kuanzia maeneo yote ya Ubungo Kibo, Ubungo Msewe na maeneo ya apa Kona. Maji yakitoka mito inafurika maji. Mabomba yanapasuka yanamwaga maji sana.
Jana tarehe 16.05.2017 Bomba limepasuka maeneo ya daraja la Riverside pale ubungo lilikuwa linamwaga maji hatari, alafu ni Bomba kubwa.
Alafu maeneo ya ubungo Msewe maji yakitoka Mabomba yanamwaga sana
 
tafadhali tunaomba kujua eneo linalovuja ili team yetu iweze kufika kwa wakati
Mkuu swali langu lililenga ni lini mtaleta maji maana majibu naona ni yale yale ya kila cku
 
Mkuu naomba unijuze ni lini mtatuletea maji sisi tunaoishi mbezi machimbo barabara ya mpiji magoe?.
 
Back
Top Bottom