DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Hongereni kwa kuongeza na kuweza kugawa maji kila siku kibaha na kwa pressure kubwa, tatizo kubwa lililojitokeza ni mabomba kupasuka hovyo sababu ya uchakavu, ombi langu wakati huu wa mvua muendelee na mgawo ili muweze ku spot sehemu zote mbovu na mzifanyie matengenezo ili hapo baadae mtakapotoa huduma 24/7 basi pawe na upotevu kidogo wa maji kuliko hivi sasa, vijana wenu wanajali tu endapo bomba kubwa limepasuka na si haya madogomadogo ya mtaani... pamoja na yote Hongereni
 
Mabomba mengi bado yanamwaga maji maeneo ya Ubungo Terminal. yazibeni bana ni keroo
HukuTabata Kisiwani aka Tabata Mwananchi ndio usiseme. Mqji yanamwagika kila baada ya nyumba tatu ya nne inamaji yanavuja. Sijui hao wasoma mita wao hawaoni.
 
Ahughulikieni mambo haya mawili kwanza.

1. Upotevu wa maji ikiwemo na wezi. Pamoja na kuongeza customer base.

2. Ukusanyaji wa madeni kwa matajiri na mawaziri. Kama ifanyavyo TQNESCO
 
Ubungo external njia ya kueleke take away maji njian ya dawasco yanamwagika daily..... Rekebishen maaana ni hasara.
 
Hongereni kwa kuongeza na kuweza kugawa maji kila siku kibaha na kwa pressure kubwa, tatizo kubwa lililojitokeza ni mabomba kupasuka hovyo sababu ya uchakavu, ombi langu wakati huu wa mvua muendelee na mgawo ili muweze ku spot sehemu zote mbovu na mzifanyie matengenezo ili hapo baadae mtakapotoa huduma 24/7 basi pawe na upotevu kidogo wa maji kuliko hivi sasa, vijana wenu wanajali tu endapo bomba kubwa limepasuka na si haya madogomadogo ya mtaani... pamoja na yote Hongereni
asante sana
 
HukuTabata Kisiwani aka Tabata Mwananchi ndio usiseme. Mqji yanamwagika kila baada ya nyumba tatu ya nne inamaji yanavuja. Sijui hao wasoma mita wao hawaoni.
asante kwa taarifa itafanyiwa kazi
 
Ahughulikieni mambo haya mawili kwanza.

1. Upotevu wa maji ikiwemo na wezi. Pamoja na kuongeza customer base.

2. Ukusanyaji wa madeni kwa matajiri na mawaziri. Kama ifanyavyo TQNESCO
asante kwa ushauri..tutaufanyia kazi
 
Hili swali halijajibiwa: Wakuu mmeliona hili
ndugu mwananchi. kwa eneo la goba mtandao wetu umeanzia pale Tank bovu hadi goba mwisho maarufu kama zahanati. na maeneo yanayopata Maji ni kwa Pembe...Kunguru...contena...njia panda ya kinzudi hadi kwenye zahanati. tunaomba kufahamu eneo lako ni wapi
 
ndugu Dan..bili zinatolewa pindi tu mita yako inaposomwa na msoma mita wetu. inawezekana kupata bili yako hata tarehe 1 na kuendelea kutokana na usomaji mita. jinsi unavyosomewa mita ndivyo utakavyopokea bili yako. ukisomewa bili yako Leo utapokea bili yako kwenye simu kesho yake
VIP kuhusu wakazi wa maeneo ya kimara esp maeneo ya mavurunza,saranga,bonyokwa na maeneo jiran na hayo? Mlitoa matangazo,wananchi wakajaza formu,na wengine kulipia kabisa ili waunganishiwe Maji,lkn mpaka sasa ni zaidi ya miezi6_8, hakuna kinachoendelea
Hebu toeni muongozo wananchi wa maeneo haya wafanye nini kuyapata Maji? Maana yanapita kimara kwenda seven zngine, lkn wao hawapati
 
Dawasco Bunju maeneo ya nyuma ya chuo cha dogodogo center Bomba litapita lini? Ndugu yangu pia yupo Changayikeni chuo cha Takwimu analalamika mabomba yapo ila maji ya dawasco hawapati lini mtatufikia?
 
Maeneo ya Mbezi beach tank Bovu Kwa Juu kidogo upande wa kushoto Kwa Kwenda Bagamoyo mita chache chache toka Bomba kubwa la Maji lakini miaka nenda wananchi hawapati Huduma ya Maji , maeneo ya Mbezi Juu , na kuendelea hakuna Maji , Maji yanaizwa bei kubwa sana lita 1000 Kwa shilingi 15,000/- Na kuendelea wakati Kumbe Kwa bei ya Dawasco ni shilingi 1,664/- tu , Watu wanafamilia kuna jamaa zangu pale wame fuatilia Dawasco Kawe Kwa miaka mingi hadi leo hawana Maji , halafu wanasema wako mita chache sana kutoka Bomba kuu ambapo Hata Kilomita moja haifiki, eti wanaambiwa Maji hayawezi kupanda kwenye mwinuko hivi hiyo inaingia akilini Kweli ? Kuna mwinuko gani pale jamani? Maeneo Kama ya Moshi nasikia kuna milima mingi lakini mbona Maji yanatoka mabombani? Watu wa kule wana usongo Na nyie vibaya sana Kwa Kukosa Maji Na ubabaishaji wenu! Hadi wananchi wengine wanazani labda baadhi yenu huenda mnafaidika na hiyo miradi ya Maji yanayouzwa labda kuna % mnapewa! Hamstahili pongezi yoyote nyie! Mmeshindwa kuifanya Dar es salaam kuwa Jiji la mfano Kwa upatikani wa Huduma ya Maji popote mwananchi alipo! Over 55 years of Independence of Tanganyika mmeshindwa kabisaa!
 
Dawasco acheni wizi
Mwezi huu mvua zimenyesha mfululizo sijatumia maji yenu sana nashangaa mnaleta bili na kudai 35,000/= eti mnadai nimetumia unit 25 acheni upuuzi
Huu ni utapeli uliopitiliza
 
Kudos DAWASCO kwa kuanza mawasiliano na raia, ila basi muyashughulikie, tutafika, tatizo kubwa ni mabomba kukatika, mnapoteza maji mengi sana sana, mpaka inauma, tena waweza kuta staff wenu wapo mtani wanaona, lakini hawajali zaidi ya kukaa kwenye viti bar na kunywa vinywaji tu
 
Dawasco acheni wizi
Mwezi huu mvua zimenyesha mfululizo sijatumia maji yenu sana nashangaa mnaleta bili na kudai 35,000/= eti mnadai nimetumia unit 25 acheni upuuzi
Huu ni utapeli uliopitiliza
Mimi ningependa kujua mita zao zinasomaje ili tuwe tunaenda sambamba,
DAWASCO.
 
Kunduchi mtongani pia kuna bomba lenu limepasuka. Maeneo ya karibu na kota za polisi ila ukitokea mtongani kwenyewe ile barabara ya mikokoni ambako gari haIpiti kuelekea kota za polisi kuna bomba lenu linavuja sana.
Nashukuru taarifa imefika, leo watu wenu wamekuja ila wamefunga maji, na kukata kipande kilichokuwa kimepasuka, hatuna maji mitaa hii, tunaomba warudi fasta kuweka kipande kipya tuendelee kupata huduma, msichukue muda mrefu.
 
Inashangaza sana mimi account yangu haina deni la mwezi april, dawasco wameniletea bill (50,000) ya mwezi may, siku NNE zimepita wanakuja kukata maji. Mwezi haujaisha mnakuja kukata maji, ni kwa nini kama sio dalili za kutengeneza mazingira ya rushwa kwa anayekuja kurudisha maji. Hii si haki hata kidogo. Najipanga kuwapandia huko huko ofisini kwenu, mkishindwa kutoa maelezo nawapandia kwa waziri. Ninyi ni waonevu sana. Cc: mtumbua majipu
 
asante kwa taarifa..tunaomba utuelekeze ni maeneo gani kwa pale Ubungo Terminal
Hata external pale, baada ya mataa njia ya kwenda mabibo/maziwa opposite na Marriot hotel mabomba yanamwaga maji njia nzima ni tope
 
Mimi ningependa kujua mita zao zinasomaje ili tuwe tunaenda sambamba,
DAWASCO.
Wameniboa kinoma
Maana mwezi April sikuwa na deni
Halafu mwezi huu watu tumetumia maji ya mvua mwanzo Mwisho halafu wanasema nimetumia unit 25 sawa na 35,000 huu ni wizi maana nalipa bili kila mwezi hivyo matumizi yansjulikana
 
ndugu mwananchi. kwa eneo la goba mtandao wetu umeanzia pale Tank bovu hadi goba mwisho maarufu kama zahanati. na maeneo yanayopata Maji ni kwa Pembe...Kunguru...contena...njia panda ya kinzudi hadi kwenye zahanati. tunaomba kufahamu eneo lako ni wapi
Nashukuru kwa majibu mazuri: Nazungumzia Goba Kulangwa, Maeneo ya Round About na maeneo yote ya kwenda njia ya Madale ili kuungana na Wazo karibu na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kulangwa etc
 
Back
Top Bottom