DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Naomba kujua tunapata lini maji maeneo ya Goba hii njia inayoelekea madale, ni gharama sana kununua maji kwenye magari. Hebu tuoneeni huruma.
 
Tunaomba mtupatie huduma ya maji wakazi wa Bunju b njia ya kwenda mabwepande
Eneo hili ni jipya kuna viwanja vya serikali viliuzwa tukanunua tukajenga ila maji ni sheeda tusaidieni
 
Mikocheni A Uswahilini hapa. Watu wamejiunga kwenye system kinyemela bila kuwa na matanki ya septiki majumbani kwao na kukiziba hawawajibiki kwa kuwa hawaathiriki na maji yanayotiririka... Watu wa DAWASCO huja mara kwa mara lakini sioni suluhu ya kudumu. Baada ya siku kadhaa mbubujiko huanza upya....
 
Kunduchi mtongani pia kuna bomba lenu limepasuka. Maeneo ya karibu na kota za polisi ila ukitokea mtongani kwenyewe ile barabara ya mikokoni ambako gari haIpiti kuelekea kota za polisi kuna bomba lenu linavuja sana.
Nashukuru taarifa imefika, leo watu wenu wamekuja ila wamefunga maji, na kukata kipande kilichokuwa kimepasuka, hatuna maji mitaa hii, tunaomba warudi fasta kuweka kipande kipya tuendelee kupata huduma, msichukue muda mrefu.
Habari, bomba lenu mmelikata na kulifunga toka juzi na kuliacha hivyo hivyo, kwa hiyo maji hamna, tafadharini, leo ijumaa mje tusaidia kuliweka sawa maana tumeanza kuwa ma shida ya maji eneo hili.
DAWASCO.
 
Asanteni DAWASCO.Naona sa hivi mnajitahidi mbezi(ya kimara) tunapata maji,walau wiki haikatuki bila maji.Sasa basi naomba iwe hivo hivo isije ikawa ni kipindi hiki cha mvua tu (ambacho hata hatukuyatumia sana) kiangazi tukarudi kwenye tabu zetu.
Mbezi mwisho kuna bomba huwa linavuja mpaka limetengeneza mtaro wa kudumu naomba mkaangali kama ni mipira yenu.Maeneo haya yaliyo jengwa maduka mapya mengi baada ya bomoa bomoa.
 
Naomba kujua tunapata lini maji maeneo ya Goba hii njia inayoelekea madale, ni gharama sana kununua maji kwenye magari. Hebu tuoneeni huruma.

Dawasco vipi mbona maswali ya maeneo haya hayajibiwi vizuri,...any hope or plan for Goba
 
Tunaomba mtupatie huduma ya maji wakazi wa Bunju b njia ya kwenda mabwepande
Eneo hili ni jipya kuna viwanja vya serikali viliuzwa tukanunua tukajenga ila maji ni sheeda tusaidieni
bunju b eneo gani
 
Hata external pale, baada ya mataa njia ya kwenda mabibo/maziwa opposite na Marriot hotel mabomba yanamwaga maji njia nzima ni tope
asante kwa taarifa itafanyiwa kazi
 
ndugu mwananchi..utaratibu wa kulipa Maji ni siku 7 tangu kuletewa bili yako. zaidi ya hapo usikubali utaratibu wowote zaidi ya huo. jua sheria na taratibu zinazokulinda kama mteja ikiwa ni pamoja na kutoa muda wa siku 7 kuweza kulipia bili tangu ulivyopokea bili yako.
 
Dawasco acheni wizi
Mwezi huu mvua zimenyesha mfululizo sijatumia maji yenu sana nashangaa mnaleta bili na kudai 35,000/= eti mnadai nimetumia unit 25 acheni upuuzi
Huu ni utapeli uliopitiliza
bitoz dawasco haiwezi kukupa bili kwa maji usiyotumia. kaangalie kwenye mita yako uangalie jinsi mita yako ilivyozunguka na uzidishe kwa bei ya Tsh 1663 kwa unit
 
Habari, bomba lenu mmelikata na kulifunga toka juzi na kuliacha hivyo hivyo, kwa hiyo maji hamna, tafadharini, leo ijumaa mje tusaidia kuliweka sawa maana tumeanza kuwa ma shida ya maji eneo hili.
DAWASCO.
Latest:
Habari, bomba lenu mmelikata na kulifunga toka juzi na kuliacha hivyo hivyo, kwa hiyo maji hamna, tafadharini, leo ijumaa mje tusaidia kuliweka sawa maana tumeanza kuwa ma shida ya maji eneo hili.
DAWASCO.
 
HukuTabata Kisiwani aka Tabata Mwananchi ndio usiseme. Mqji yanamwagika kila baada ya nyumba tatu ya nne inamaji yanavuja. Sijui hao wasoma mita wao hawaoni.
Wapo bize kuwaunganishia maji kinyemera watu. Apa ubungo Msewe kuna Mama mmoja anaitwa Mama Kapinga anaiba maji. Wale wasoma mita wakija anawapa Tshs 3,500 na wanakausha. Shirika la dawasco linaujumiwa sana mpaka inasikitisha. Na huyu mama alishawai kukatiwa maji, na akamfanyizia mambo ya ushirikina, yule mama aliyemkatia maji akaamishwa sehemu ya kazi. Huyu Mama ana tank la Lita laki moja na anauza maji.
Sasa Lita laki moja kwa Tshs 3,500. Apo dawasco inabidi mtumie watu wenye uweledi la sivyo hujuma zipo nyingi.
 
habari DAWASCO mimi ni mteja wenu nimeunganishiwa toka mwaka jana ila sikutumiwa bili hadi leo, nilijaribu kuwafuatilia bila mafanikio hadi wiki hii nilikuja hapa jamvini kuomba msaada kwenu, sasa leo wamenitumia sms na kunipa a/c 90129292 units ni ni 30, sasa nisichoelewa ni kuwa deni langu ni 123,573.5 yani nashindwa kuwaelewa kabisa naomba msaada wenu, kituo changu ni boko!
 
Nimeenda Bagamoyo DAWASCO kuomba surveyor, eti anataka hela mafuta, mie nimeshindwa kwa kweli, maana hiyo ni rushwa kabisa, namshtaki hapa
tafadhali tutumie ujumbe mfupi ukiandika jina lako na surveyor aliyekuomba kiasi hicho cha fedha kwa hatua zaidi
 
Naomba unipe tofauti kati ya wholesome water ,potable water na palatable water
 
Kwa sasa mmeshajenga tenki kubwa la kusambaza Maji pale Luguruni. Je mitaa ya kwembe tutapataje Maji kwa sababu tumeshajaza fomu kwa ajili ya hitaji la Maji? Ombi langu msikae maofisini. Tulishajaza fomu tangu mwaka Jana tulipofuatlia tukaambiwa fomu hazionekani eti zimepotea! Inaonyesha hamko serious. Tukaambiwa tujaze zingine. Sjui nazo zitapotezwa au vipi. Tunahitaji Huduma tafadhali
 
Eti.ukiwa na mita ya zaman.alafu ikaharibika.mkaja kubadilisha.je inakuwa mmeitoa bure au nailipia kwenye bili?
2.maji mnauza sh ngapi kwa unit.kwa DAR?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…