DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Wahusika kama nilikuwa nalipa bill kwa Maxmalipo au Selcom bahati mbaya nikakosea akaunti namba malipo yakaenda kwenye akaunti nyingine nawezaje kurekebisha ili malipo yaende kwenye akaunti iliyokusudiwa?
 
Nyie Dawasco vipi? Sasa mbona watu wanauliza halafu hamtoi majibu? Hamjui mtu mmoja akiuliza linaweza kuwa ni tatizo la wengi hivyo kupitia huyo wakapata majibu? Toeni majibu kwa haraka jamani vinginevyo kutakuwa hakuna haja ya kuwa na Special Thread
 
Hivi Dawasco hii special thread kwa ajili ya wateja kutoa maoni/ malalamiko ni GERESHA? Mbona hakuna MAJIBU WALA HATUA ZINAZOCHUKULIWA kutatua KERO?
 
Jambo lolote ukiiga ni lazima uchemke , hawa jamaa awakujipanga kabisa na hii huduma kiko wapi sasa wamekula kona.
 
Dawasco narudia tena pale mtaa wa omary londo na swahiki Gerezani kuna tatizo gani mbona kinyesi na sisi kila siku ?mnashindwa nini nyie si mna ma engineers tatizo liko wapi..au mnafurahi.sisi tuishi na vinyesi?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Ununio hatuna maji siku ya pili mfululizo na hakuna taarifa yeyote!
 
Nimeunganisha maji tangu dec 2017 ila sijawahi pata maji hata siku moja.
Nimeshangaa leo nimeletewa bili na deni eti nadaiwa 53,000 sasa sielewi ni la nn maana hela ya kuunganishiwa maji nililipa na maji hayajawahi kutoka tangu kipindi kile.
Sasa sielewi bili na deni ni la nn
 
Nipo Goba,, sorry
 
Je kwa nini DAWASCO hailengi kuongeza wateja wapya na badala yake inahangaika na wale wale wa siku zote? Hamuoni kuwa kuna fedha nyingi mnaziacha kwa potential customers ambao wanashindwa kupata huduma zenu kwa vile tu hamuendi kwa wananchi?

Fikiria maeneo kama Mbagala Gongolamboto, Kigamboni nk sidhani kama mmeyafikia maeneo hayo
Kukamilika kwa miradi ya kimbiji na mpera kutaleta neema ya Maji kwa maeneo hayo na maeneo ya jirani
 
Hizo namba za huduma kwa wateja mlizoweka huwa hazipokelewi. Unaweza kupiga kutwa nzima na usijibiwe. Haya ni malalamiko ya baadhi ya Rafiki zangu waliopo Dar es Salaam
Tafadhali uko kituo gani tukutumie namba ya eneo husika
 
Safi sana, unaona faida za mitandao ya kijamii habari kama hii mungeiweka TBC au gazeti la uhuru mimi nisingeiona, lakini kupitia JF nimeiona, hongera sana.

Sasa, muwe mna toa ushuhuda kwa viongozi wa kisiasa kuwa mitandao ya kijamii na hasa JF inasaidia sana kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi
Sawa
 
Nimeunganisha maji tangu dec 2017 ila sijawahi pata maji hata siku moja.
Nimeshangaa leo nimeletewa bili na deni eti nadaiwa 53,000 sasa sielewi ni la nn maana hela ya kuunganishiwa maji nililipa na maji hayajawahi kutoka tangu kipindi kile.
Sasa sielewi bili na deni ni la nn
Tunaomba Account namba yako tufatilie kwa ukaribu
 
Wahusika kama nilikuwa nalipa bill kwa Maxmalipo au Selcom bahati mbaya nikakosea akaunti namba malipo yakaenda kwenye akaunti nyingine nawezaje kurekebisha ili malipo yaende kwenye akaunti iliyokusudiwa?
Inawezekana ..fika ofisi ya dawasco unayohudumiwa ili wafanye kitu kinaitwa adjustment
 
Back
Top Bottom