DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Kwenu Dawasa, kwanza nawashukuru eneo nilipo napata maji bila shida,ila kuna tatizo moja inabidi mlifanyie kazi nadhani hii ni Customer care unit, kwa kweli ni makwazo sana na fedheha mtaani, mimi ni mteja wenu nalipa bill kila mwezi na sijawahi kulaza au kuacha kulipa, napata bill kwa wakati. ajabu , wiki 2 baada ya kupata bill wanakuja watu kukata maji sasa hua nashangaa sana, hivi mimi nakua na hela muda wote mfukoni yakulipa maji tu sina mahitaji mengine?

kwani ukija ukagonga ukanikumbusha haitoshi mpaka ujaze watu mtaani wajue kuwa nadaiwa. yaani ni kero sana wakt mwingine ni shs 5000/ imebaki, hebu jirekebisheni, hasa TBT .
 
Kwenu Dawasa, kwanza nawashukuru eneo nilipo napata maji bila shida,ila kuna tatizo moja inabidi mlifanyie kazi nadhani hii ni Customer care unit, kwa kweli ni makwazo sana na fedheha mtaani, mimi ni mteja wenu nalipa bill kila mwezi na sijawahi kulaza au kuacha kulipa, napata bill kwa wakati. ajabu , wiki 2 baada ya kupata bill wanakuja watu kukata maji sasa hua nashangaa sana, hivi mimi nakua na hela muda wote mfukoni yakulipa maji tu sina mahitaji mengine? kwani ukija ukagonga ukanikumbusha haitoshi mpaka ujaze watu mtaani wajue kuwa nadaiwa. yaani ni kero sana wakt mwingine ni shs 5000/ imebaki, hebu jirekebisheni, hasa TBT .
Kinyerezi imekuwa sugu watu wameanza kuzoea maji ya visima.hakuna tangazo wala maelezo yeyote wanaona ni kawaida tu.huduma muhimu kama hii.kwakweli ndio mnafanya wananchi wawaze kubadili uongozi.
 
Hv niwaulize Chanika sio eneo lenu la uwajibikaji?hakuna huduma za maji toka nchi imepata Uhuru,yale maji mmeleta kisarawe kwanini msiyalete huku zingiziwa? huduma ya umeme tunapata toka kisarawe nyie mnafeli wapi?
 
Naomba kujua unit moja bei na bei hutofautiana kati ya mikoa?
 
Maji Makongo juu week 5 sasa shida ni nini wakati msishajenga matank makubwa?
 
Samahani naomba kujua namba za gari la unyonyaji maji take wilaya ya Temeke.
 
Kimara Mwisho maeneo ya Kwa Kichwa mpaka Bonyokwa ni wiki ya pili sasa maji hayatoki na ukiuliza hamna sababu za msingi. Meneja DAWASA Kimara tunaomba maelezo
 
Kunani Kimara ( Bonyokwa, Mwisho, etc )
tunaoga mikojo huku mtuhurumie
mmekata zaidi ya wiki 3 sasa
 
DAWASA
Maeneo yote ya kipawa na msimbazi hamna maji, tunasikia bomba limeharibika. tupeni mrejesho hatua mliyofikia kwa matengenezo. Hatuna maji mwezi sasa
 
Wakazi wa kiwalani Sasa ni wiki ya tatu mmekata maji bila taarifa yoyote Kama Kuna tatizo gani mkumbuke mmewatoa watu kwenye visima vya wapemba mkatuhakikishia maji yatakuwepo tunaomba taarifa tupewe tafadhalli
 
Mnatumia vigezo gani kumkatia mteja maji?
Ni miezi mingapi au miaka mingapi bila ya kulipia ndio mnakata maji?
 
DAWASA maeneo ya Kunduchi barabara ya kwenda madini na barabara ya Mwakwembe , maji yanatiririka hii sasa ni wiki ya pili
 
Nafikiri huyu bwana Cyprian Luhemeja baada ya sifa nyingi sasa yeye amelala na anaowaongoza wameingia kwenye usingizi mzito mithili ya mtu aliyepewa dawa ya usingizi;

Inawezekana vipi kijiji/mtaa kwamatias Kibaha wote tumekatiwa maji bila taarifa leo siku ya tatu na Simu zao wamezima as if hakuna anayewajibika na tatizo letu?

Ustaarabu na uwajibikaji wa kila mmoja ni kuheshimu kazi na kuwaheshimu wateja wenu vile inavyotakiwa, fikiria kuwa unanyumba yenye choo ndani ambayo inahitaji maji ya kutosha kila pale watu wanapojisaidia lakini huduma hiyo hakuna je harufu itakayotoka hapo nyumba itakalika kweli?

Dawasa jaribuni kuwa wastaarabu hata kidogo mjitofautishe na enzi za NUWA
 
Mabadiliko hayo makubwa yamehusisha Watendaji mbalimbali wa Mamlaka hiyo yamewaacha baadhi yao wakihamishwa Idara au Vitengo, Walishushwa Vyeo Vyao na wengineo Wakipandishwa Vyeo.

Lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha ufanisi wa Mamlaka hiyo nyeti nchini inayokabiliwa na changamoto mbalimbali
 
Mie nauliza Dawasa/Dawasco kwanini wakati mwingine maji bombani yanatoka machafu yanakuwa hayafai kufanyia kitu chochote, shida ni nini

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
DAWASA bado hamjiwezi huduma mbovu
Angalieni miundombinu yenu bado kabisa
Haijakaa sawa kingine mnapenda kugombana
Na wateja wenu juu bili huwa mnachomekea sana bili haina uhalisia na matumizi
 
Mie nauliza Dawasa/Dawasco kwanini wakati mwingine maji bombani yanatoka machafu yanakuwa hayafai kufanyia kitu chochote, shida ni nini

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hawa watu wana uzembe mkubwa sana, hayo maji ambayo hutoka machafu ni sewerage system yao inaingiliana na mfumo wa maji safi. Ule uchafu ni kinyesi!

Mabomba yanapasuka hovyo hawafanyi marekebisho, kuna sehemu nyingine mifereji imegeuka mito sababu ya maji yanayomwagika.

Dar es salaam kuna maeneo mengi hayajafikiwa na huduma ya maji, miaka 59 ya uhuru jiji halina huduma ya maji!
 
Hawa watu wana uzembe mkubwa sana, hayo maji ambayo hutoka machafu ni sewerage system yao inaingiliana na mfumo wa maji safi. Ule uchafu ni kinyesi!

Mabomba yanapasuka hovyo hawafanyi marekebisho, kuna sehemu nyingine mifereji imegeuka mito sababu ya maji yanayomwagika.

Dar es salaam kuna maeneo mengi hayajafikiwa na huduma ya maji, miaka 59 ya uhuru jiji halina huduma ya maji!
Yaani ni shida jamani, unafungua bomba maji yanatoka meusi kabisa, huwezi kuyatumia kwa namna yoyote ile, na inaweza kuchukua hata masaa matano ndio yanaanza kutoka masafi
 
Hatari sana
Yaani ni shida jamani, unafungua bomba maji yanatoka meusi kabisa, huwezi kuyatumia kwa namna yoyote ile, na inaweza kuchukua hata masaa matano ndio yanaanza kutoka masafi.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom