DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Someni hii sheria kama mnaielewa DAWASA
Screenshot_20210312-222146_Instagram.jpg
 
Dawasa mna matatizo, kwa kweli nanyi yabidi mtumbuliwe tu. Leo ni siku ya 5 mimi na watoto tukioga tunawashwa mwili mzima kama mtu aliye na allergy ya Chloroquine.

Hivi shirika kubwa kama hili hamna wataalam kweli? Mama Samia tafadhali wamulike tochi hawa wahalifu, wako very incompetent[emoji1747][emoji1418]
 
Hivi kwanini msilete Mita mpya za maji ambazo zinafanana na luku kuliko hizi tunazotumia sasa hivi
 
Dawasa hivi unit moja ya maji kwenu ni bei gani, maana nimeshangaa kuona kila mwezi bili inaongezeka wakati kwenye matumizi hakuna kilichoongezeka hapa kwangu,bili iliyoanzia 25k kwa mwezi ila mpaka leo hii nimetumiwa bili ya 65k kwa mwezi,pia mnakuja muda gani kusoma hizi mita au mnakadiria tu na kutuma kwa mteja?
 
Dawasa hivi unit moja ya maji kwenu ni bei gani, maana nimeshangaa kuona kila mwezi bili inaongezeka wakati kwenye matumizi hakuna kilichoongezeka hapa kwangu, bili iliyoanzia 25k kwa mwezi ila mpaka leo hii nimetumiwa bili ya 65k kwa mwezi, pia mnakuja muda gani kusoma hizi mita au mnakadiria tu na kutuma kwa mteja?
DAWASA ni mijizi. Baada ya kubambikiwa sana bili nikaanza mfumo wa kusoma meter kila siku. Kama bahati safari hii msomaji meter amekuja nikiwepo pia, tumesoma wote meter. Cha ajabu baada ya siku 2 inakuja bili ikiwa na units 4 zaidi ya zilizosomwa. Na hapo ndipo nilipogundua jinsi gani wanabambikia watu bili. Leo units 4 kwangu inamaanisha ni swala la wakati tu kabla hawajabambika units 10 zaidi.
 
Pamoja na jitihada za upatikanaji wa maji Dar... Lakini umekuwa ni Jambo la kawaida maji kukatika kwa masaa karibu kila siku.. eneo linalopata maji kwa mgao ni maeneo jirani na hotel ya best point, Zambezi, na maeneo kuelekea external.

Haieleweki na haijaelezwa Nini tatizo na lini litaisha.

Maji yanapokatikana yanakuwa na presha kubwa Lakini Mara yanakatika na kupatikana baada ya masaa 8 kila siku.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Kwanini mnatupa mgao wa maji ubungo Riverside maeneo ya best point na Mandela Rd?
 
DAWASA, naomba nafasi ya kazi kwenu

I'm an expert in water treatment (kutibu maji viwandandani) kwa kutumia njia kama vile sand filtration, coagulation, alkalinity reduction, membrane filtration (utra-filtration,micro filtration & reverse osmosis), chlorination &carbon filtration, iron & nitrate removal, UV systems, De- aeration pamoja na ozone technology.
 
Nimeibiwa Meter ya maji mwezi Jana na mafundi wa Dawasa waliokuja wakiwa na bajaji ya shirika. Meter ilikuwa na 000000 readings.

Nilireport kunakohusika nikaambiwa ni uzembe wangu na nikaambiwa nikitaka maji nilipie nipewe meter mpya.

Clientele ni zero dawasa hawawezi hata kutafuta ilipokwenda fungwa na badala yake napata punishment mie mteja.

Mama Samia miwani yako ielekeze Huko pia.
 
Sijapata bill yangu ya mwezi April mwaka huu.
Naweza kuipata kupitia akaunt number yangu?
Msoma mita wangu sijamuona tangu january
 
Nadhani itakuwa jambo jema kama wakati wa usomaji mita awepo mwenyeji na pia kuwepo na form maalum inayoonyesha unit zilizosomwa wakati huo na wote (msomaji mita & mteja) wasaini kwenye iyo form..!!!
 
DAWASCO mnapita mitaani kusoma mita, nawashauri mkumbuke pia na kufanya matengenezo pale ambapo mnakuta kuna changamoto ya miundo mbinu.

Kwa mfano, mnakuta bomba linavuja, mwananchi kajitahidi kufunga bomba na mpira ili kupunguza upotevu wa maji, lakini nyie mnasoma mita kila mwezi na uharibifu huo mnauona lakini hamchukui hatua, mara nyingi mabomba hayo ni ya barabarani (mitaani) ambako yanakumbana na changamoto za shughuli za kijamii na kiasili( mmomonyoko na pia vyombo vya moto).

Maji yanapotea na nyie kila mwezi mnapita mnayaona na hamchukui hatua, mnataka mpewe taarifa gani wakati mmeona kwa macho yenu?


Wananchi tunajitahidi kulipa bili ili shirika liweze kujiendesha ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo kama hayo. Mnakwama wapi? au kunasheria ya matengenezo kwa watumiaji? tufahamishwe kama sheria hiyo ipo.
 
Mita yangu inazunguka kwa speed kubwa, tupo watatu tu ndani ya nyumba kwa mwezi nalipa 18000 naomba marekebisho ya mita
 
Mita yangu inazunguka kwa speed kubwa, tupo watatu tu ndani ya nyumba kwa mwezi nalipa 18000 naomba marekebisho ya mita
Mkuu jaribu kufunga bomba/ koki zote alafu angalia kama meter yako itakuwa inazunguka. Kama itakuwa inazunguka baada ya kufunga koki zote basi kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na leakage kwenye bomba lako mbele ya meter, hivyo tafuta fundi wa bomba akurekebishie leakages kwanza.

Kama metere itaendelea kuzunguka basi itakuwa ni ubovu wa meter na utatakiwa kuripoti ili watakupatie meter nzima.

Nikiangalia bili yako nahisi tatizo litakuwa ni leakage ndogo upande wa bomba laka mbele ya meter kwani ingelikuwa tatizo la meter bili yake ingelikuwa kubwa sana.
 
pre paid meters ndio suluhisho la matatizo yote na pia serikali itajihakikishia kukusanya mapato yake bila kupotea hata shilingi 1
 
Dawasa jifunzeni kwa Tanesco kwa kufuatilia miundo mbinu yenu, na on time responds.

maji yanamwagika mitaan siku tatu na pengine wiki maji yanamwagika huku watu wengine hawana maji na wananunua maji kwa bei kubwa mitaan,

Mwisho wa siku mnapandisha bili za maji kwa sisi watumiaji wa maji kisa garama za uendeshaji.

Ikiwezekana magari yenu yapite mitaani na matangazo mkiwaomba watu kuwapa taarifa na mje haraka sio taarifa inatolewa leo mnakuja kesho .

Na magari, bajaji zenu bandiken numba za simu za emejens ili watu wawapigien kuja kuziba mabomba ya maji yaliyopasuka.

#Ushauliwangu.
 
Back
Top Bottom