A
Anonymous
Guest
Naomba nitoe kero kuhusu huduma ya maji katika maeneo ya Pugu Mwakanga.
Bomba kubwa la DAWASA linalosambaza maji kwa wateja limeharibika kutokana na kuchakaa. Taarifa zilitolewa kwa DAWASA, na wahusika walifika eneo la tukio na kujionea hali halisi. Hata hivyo, cha kushangaza, badala ya kutekeleza wajibu wao wa kukarabati bomba hilo, wamewaeleza wananchi ambao ni wateja wao kuwa wanapaswa kuchangishana fedha kwa ajili ya matengenezo.
Tulipouliza utaratibu huo unatokana na nini, tulijibiwa kuwa ofisi haina vifaa kwa sasa. Cha kushangaza zaidi, badala ya kutupatia namba ya malipo (Control Number), tunaelekezwa kuchangia fedha kupitia akaunti ya benki ya ofisi hiyo.
Sasa ni takribani wiki mbili tumekosa huduma ya maji, hali inayotulazimu kununua maji katika maeneo ya mbali na tunapoishi.
Tunaomba DAWASA itoe ufafanuzi kuhusu utaratibu huo wa kuchangisha fedha kwa wateja kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu yake, pamoja na kuchukua hatua za haraka kurejesha huduma ya maji katika eneo letu.
Maji ni hitaji la msingi, na wananchi hawapaswi kuendelea kuteseka kwa muda mrefu bila huduma hiyo.