DAWASA: Tumerekebisha bomba lililopasuliwa na Mkandarasi Keko Juu na huduma imerejea

DAWASA: Tumerekebisha bomba lililopasuliwa na Mkandarasi Keko Juu na huduma imerejea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Ufafanuzi na hatua zimechukuliwa na mamlaka husika ya maji muda mfupi baada ya Mwananchi kupitia JamiiForums.com kuandika “Wakazi Keko Juu tuna shida kubwa baada ya Mkandarasi kukata mabomba ya maji kwa takriban wiki nzima."

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema imekamilisha kazi ya kuunganisha mabomba ya ukubwa wa inch 4 yaliyopasuliwa na wakandarasi wa ujenzi wa barabara Keko na hivyo kuanzia sasa huduma imesharejea kwa wateja wao.

‎
‎Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Bi. Everlasting Lyaro amesema "Bomba lilirekebishwa tarehe 28.5.2026 na hadi muda huo wateja 8 kati ya saba wamesharudishiwa na sahizi mafundi wapo site wanamalizia mmoja."
 
Back
Top Bottom