RESOLVED DAWASA warekebisha bomba karibu na Kituo cha Daladala Gongo la Mboto lililovuja zaidi ya miezi miwili

RESOLVED DAWASA warekebisha bomba karibu na Kituo cha Daladala Gongo la Mboto lililovuja zaidi ya miezi miwili

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2026-09-19_09-47-04.jpg

photo_2026-09-19_08-47-03.jpg

Baada ya Mwananchi kuwasilisha hoja Mtandaoni kuhusu tatizo la maji kutitirika eneo la Gongo la Mboto, kituo cha magari yanayoenda mjini kinachoitwa Maliasili, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeshughulikia changamoto hiyo.

Mafundi wa DAWASA wamefika eneo la tukio wameziba bomba lililokuwa linatiririsha maji na sasa kila kitu kinatarajia kurejea kwenye hali yake nzuri.

Ikumbukwe, mnamo Septemba 5, 2026, Mdau alisema maji yamekuwa yakitiririka kwa takribani mwezi mmoja, huku yakielekea hadi eneo la makaburi, na kwamba wahusika wa maji walifika kuona changamoto hiyo lakini hatua hazikuchukuliwa.

Pia soma:
~ DAWASA: Tunafuatilia kero ya maji kutiririka Gongolamboto
~ Gongo la Mboto karibu na Kituo cha Daladala cha Maliasili kuna tatizo la bomba la maji kuvuja sana:
 
Hebu fikiria lita ngapi za maji yamepotea kwa miezi hiyo miwili
Tutabaki masikini tu
Wenzetu siku ya kwanza tu wanajua wapi panavuja
 
Back
Top Bottom