DOKEZO DAWASA yatoa notisi ya kusitisha usambazaji wa maji ya Visima kwa baadhi ya Maeneo ya Jiji la Dar es salaam

DOKEZO DAWASA yatoa notisi ya kusitisha usambazaji wa maji ya Visima kwa baadhi ya Maeneo ya Jiji la Dar es salaam

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
KUNA HAJA YA SERIKALI, KUWEKA MANAJEMENTI ZA WAHINDI, WACHINA KWENYE KUENDESHA HAYA MASHIRIKA.
NI RAHISI KUNUKUU SHERIA YA MWAKA FLANI, NA UKAACHA KUANGALIA HALI HALISI.
KUNA WATU WAMEWEKEZA KWENYE KUCHIMBA VISIMA KWA FEDHA NYINGI NA KUUZA MAJI KWA WENGINE. HII YOTE NI KWA SBB MAJI YA MAMALAKA SIO YA KUYATEGEMEA.KWAMBA MAJI YA VISIMA NI TEGEMO LA WENGI.
 
Sheria za mwendakuzimu hizi. Inabidi bunge lifanye kazi ya ziada kuondoa hizi sheria zilizowekwa na awamu ya 5. Zilikuwa sheria za hovyo za kidikteta. DAWASA hawana makosa... wabunge waliotunga hiyo sheria na Rais aliyeisaini ndo wakulaumiwa.
Aliweka sheria hizo lakini maji hayakukatika DSM yote hata siku moja kwa muda wote ambao alikuwa madarakani.
Kila mnoposhindwa kutekeleza majukumu yenu lawama kwa marehemu!! Amekufa hatorudi mbinu hii ya utetezi ina ukomo wake.
Fanyeni yenu haitasaidia kugombana na mfu.
 
Hii nchi ina laana sio bure.

Huo mfumo wanaodai umesambaa unaweza kaa wiki nzima bila ya maji.

Imekuwa kama vile utawala unapata faraja kwa watu kutaabika.
Mtalalamika sana lakini hakuna kitu mnaweza fanya huo ndio uzuri
 
Hao ndio CCM wanaongoza taifa miaka 40 ila bado story ya maji safi na salama zinaendelea. Je ikitokea muda mvua zikagoma miezi 5 tumejipanga vipi?.

Tanzania tumebarikiwa maziwa, vijito na ardhi yenye maji ila ni ujanja ujanja tu
Mtalalamika sana lakini hakuna kitu mnaweza fanya huo ndio uzuri
 
Wasambazaji binafsi maji hayakatiki hata siku moja na bill zao rafiki kwa watumiaji

Katika mashirika mabovu nchi hii ni Tanesco, TTCL na Hizo mamlaka za maji

Soko lipo ila ukiritimba na kuvuta miguu

Mfano TTCL ilikuwa ndio kampuni pekee ya Simu

Mimi niliomba kufungiwa nilikaa Miaka mitatu bila kufungiwa zilizokuja simu za mkononi nilienda personally kwenda ku cancel ombi kuwa mizimu yao ya midway sitaki tena.

Dawasa jiji lote soko lilikuwa lao lakini kufungiwa shida na mirushwa kibao ubabaishaji mwingi.

Mimi bomba la Dawasa linapita mlangoni kwangu lakini niligoma kuunga natumia private supplier toka afunge maji hayajawahi kukatika.
embu nifafanulie huyo private supplier nitampata vipi?na yy anatumia maji kutoka vyanzo gani?na wao wanasambaza mabomba au unaletewa na magari?
 
Mamlaka ya Huduma za Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) imetoa agizo la kusitisha biashara ya usambazaji wa maji ya visima katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam ndani ya siku thelathini (30) kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa kwa wahusika.

Agizo hili linatokana na kupanuka na kuongezeka kwa wigo wa miundombinu ya DAWASA katika kufikia wateja wengi ambao awali walikuwa hawawezi kupata huduma hii pamoja na ukiukwaji wa sheria ya huduma za usambazaji wa maji ya kisima kinyume cha Sheria ya huduma ya usambazaji maji na usafi wa mazingira Namba 5 ya mwaka 2019 ambapo imepiga marufuku mtu yoyote kujihusisha na usambazji wa maji isipokuwa mamlaka husika tu.

Oktoba 25, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla alithibitisha uwepo wa upungufu mkubwa wa maji mto Ruvu, hivyo kuwataka wakazi wa jiji hilo wajiandae na mgao wa maji.

View attachment 2398198


Kuhusu uwepo wa mgao wa maji kwenye jiji la Dar es salaam unaweza kusoma hapa: Rasmi Dar yakumbwa na uhaba wa Maji, RC Makalla athibitisha uwepo wa Mgao
.
Kweli mpumbavu hata ukimtwanga kwenye kinu upumbavu wake hautamtoka. Kama watu hawapati maji ya taasisi, wasikoge?
 
Kamati ya roho mbaya!! Ilifaa waongeze juhudi katika usambazaji maji na upatikanaji maji Kwa wakati!
Wateja wangewachagua wao tu
 
Hapa ndio unajiuliza hawa tuliowapa madaraka, wanatumia vichwa kufikiria ama makalio?
 
Wanataka ku monopolize huduma ya maji wakati wao wenyewe hawajitoshelezi kwenye usambazaji.

Wanategemea mito tu

Waachie ufala

Kuna maeneo mfano kitunda Nyantila kuna maji matamu sana ya visima chumvi huipati kabisa.

Wanaishi kwa system hio ya kusambaziana maji ya visima kwa litres sababu bomba la dawasco halijapita au liko mbali sana.

Dawasa waachie mambo ya kizamani.
 
Huko si ndio kwa matajiri? Wanashindwa nini kuchimba na wao?
Matajiri wakisikia maji ya visima, hudhani ni kwa ajili ya watu wa uswahilini, sasa cha moto wanakiona.
Kwa shida hii watatia akili waanze mipango ya kuwa na maji ya kutosha, maana karibia wataanza kuoga baharini,
 
Back
Top Bottom