Unapo mchapa mtoto kwa kukosea jambo fulani huwa unaenda mahakani kuthibitisha?
utafungwa wewe nenda kasome vizuri sheria ya mtoto, (The Law of the Child Act 2009) inakataza adhabu kwa mtoto bila utaratibu
Ni Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 ambayo inampa mamlaka waziri wa elimu kutunga kanuni za masuala mbalimbali zitakazokidhi utekelezaji wa masuala ya sheria hiyo. Mojawapo ya kanuni zilizotungwa ni
The Education (Corporal Punishment) Regulation G.N.294 ya mwaka 2002. Kanuni hizi zinatoa mwongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani.
Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4 kwa tukio lolote.
Sheria inampa mamlaka mwalimu mkuu wa shule husika kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa adhabu hiyo.Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.
Kanuni ya (5) inataka kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu, ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu. Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na mkuu wa shule.
Sheria hii inataka uchunguzi na kujiridhisha kuwa mwanafunzi amehusika moja kwa moja na kosa analotuhumiwa nalo ndipo hatua ya kupeleka suala lake mbele ya mwalimu mkuu ili atumie mamlaka alopewa kisheria kutoa adhabu stahiki kwa mwanafunzi linafuata.
Acha kutetea upuudhi wa huyo DC na pia uwe unajisomeasomea sheria mbalimbali za nchi la sivyo utakuwa unachania upupu na upuudhi kama uliochangia hapa.
Nakushauri acha tabia ya kuadhibu watoto hasa kwa viboko, kuna njia nyingi tu nyingine za kumrekebisha mtoto kama kakosea bila kutumia viboko la sivyo yanaweza kukukuta usiyotegemea hata kama mtoto umemzaa wewe, tambua kwamba mtoto analindwa kwa sheria mbalimbali
Huyo DC kachemka sana inatakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu na mamlaka yake