DC Arusha, Kenani Kihongosi: Tutafundishana uzalendo mpaka tutaelewana vizuri

Azizi J Hamad

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
442
Reaction score
230

Alisikika Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Ndg. Kenani Kihongosi akisema, "Tutafundishana uzalendo mpaka tutaelewana vizuri" huku akiwatandika viboko wahujumu wa mali za serikali.

Mimi naungana nae na nadiriki kusema tunahitaji viongozi kama hawa wazalendo na wakali kwa watu wote ambao ni wahujumu wa mali za serikali, kwa hakika taifa letu litasonga mbele.

Endelea kuchapa kazi Kiongozi, watanzania tunaojitambua tupo pamoja nawe na tunaendelea kukuombea afya tele kwa Mungu wetu wa Mbinguni.

Pamoja Tuijenge Tanzania
 
Mtoa post utakuwa mmoja wa watanzania wasiojitambua.

Hakuna Sheria yeyote Wala utaratibu wowote unaoruhusu upuudhi aliofanya huyo dc mpuudhi
Angetakiwa ahakikshe watu hao wakashtakiwe mahakamani.

Dc ana uwezo wa kuamuru mtu awekwe mahabusu tena siozaidi ya masaa 48 na Kisha mtu huyo apelekwe mahakamani.

Alichofanya huyo dc ni upuudhi hao waanga nawashauri wakamfungulie huyo dc mashtaka on personal
 
Unapo mchapa mtoto kwa kukosea jambo fulani huwa unaenda mahakani kuthibitisha?
Hujui unachoongea mkuu.. nna wasiwasi na elimu yako, hata civics tu ya form two inaelezea hichi kitu..

Huwezi kujichukulia tu sheria mkononi bila mahakama kuthibitisha kama kosa limefanywa.

Wewe na huyo mkuu wa wilaya mna matatizo fulani ya akili ama elimu haitoshi
 
Unapo mchapa mtoto kwa kukosea jambo fulani huwa unaenda mahakani kuthibitisha?
utafungwa wewe nenda kasome vizuri sheria ya mtoto, (The Law of the Child Act 2009) inakataza adhabu kwa mtoto bila utaratibu
Ni Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 ambayo inampa mamlaka waziri wa elimu kutunga kanuni za masuala mbalimbali zitakazokidhi utekelezaji wa masuala ya sheria hiyo. Mojawapo ya kanuni zilizotungwa ni The Education (Corporal Punishment) Regulation G.N.294 ya mwaka 2002. Kanuni hizi zinatoa mwongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani.

Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4 kwa tukio lolote.

Sheria inampa mamlaka mwalimu mkuu wa shule husika kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa adhabu hiyo.Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.

Kanuni ya (5) inataka kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu, ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu. Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na mkuu wa shule.

Sheria hii inataka uchunguzi na kujiridhisha kuwa mwanafunzi amehusika moja kwa moja na kosa analotuhumiwa nalo ndipo hatua ya kupeleka suala lake mbele ya mwalimu mkuu ili atumie mamlaka alopewa kisheria kutoa adhabu stahiki kwa mwanafunzi linafuata.

Acha kutetea upuudhi wa huyo DC na pia uwe unajisomeasomea sheria mbalimbali za nchi la sivyo utakuwa unachania upupu na upuudhi kama uliochangia hapa.

Nakushauri acha tabia ya kuadhibu watoto hasa kwa viboko, kuna njia nyingi tu nyingine za kumrekebisha mtoto kama kakosea bila kutumia viboko la sivyo yanaweza kukukuta usiyotegemea hata kama mtoto umemzaa wewe, tambua kwamba mtoto analindwa kwa sheria mbalimbali

Huyo DC kachemka sana inatakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu na mamlaka yake
 
Hujui kwamba unaweza kushtakiwa kwa kumchapa mwanao? Hujui kwamba mambo kama haya yanaweza kuishia kama yale ya Dr. Kleruu na Mzee Mwamwindi wa Iringa kwasababu kuna wanaume hawatakubali kudhalilishwa kiboya hivi? Hebu fikiria ingekuwa wewe; je ungekubali kuadhibiwa kwa viiboko hadharani?
 
Hata mimi nimefurahishwa sana,inatakiwa DC na RC wote wawe wa kiume siyo mkuu wa wilaya anakuwa mwanamke mrembo hata kukaripia maovu hawezi.

Hivi mnajua kwa nini Baba wa Taifa Nyerere aliteua wanajeshi tu?
 
Alisikika Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Ndg. Kenani Kihongosi akisema, "Tutafundishana uzalendo mpaka tutaelewana vizuri" huku akiwatandika viboko wahujumu wa mali za serikali....
Hiyo sera ya kutandika viboko watu wazima ni ya KiKOLONI
 
utafungwa wewe nenda kasome vizuri sheria ya mtoto, (The Law of the Child Act 2009) inakataza adhabu kwa mtoto bila utaratibu
Ni Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 ambayo inampa mamlaka waziri wa elimu kutunga kanuni za masuala mbalimbali zitakazokidhi utekelezaji wa masuala ya sheria hiyo. Mojawapo ya kanuni zilizotungwa ni The Education (Corporal Punishment) Regulation G.N.294 ya mwaka 2002. Kanuni hizi zinatoa mwongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani.

Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4 kwa tukio lolote.

Sheria inampa mamlaka mwalimu mkuu wa shule husika kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa adhabu hiyo.Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.

Kanuni ya (5) inataka kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu, ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu. Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na mkuu wa shule.

Sheria hii inataka uchunguzi na kujiridhisha kuwa mwanafunzi amehusika moja kwa moja na kosa analotuhumiwa nalo ndipo hatua ya kupeleka suala lake mbele ya mwalimu mkuu ili atumie mamlaka alopewa kisheria kutoa adhabu stahiki kwa mwanafunzi linafuata.

Acha kutetea upuudhi wa huyo DC na pia uwe unajisomeasomea sheria mbalimbali za nchi la sivyo utakuwa unachania upupu na upuudhi kama uliochangia hapa.

Nakushauri acha tabia ya kuadhibu watoto hasa kwa viboko, kuna njia nyingi tu nyingine za kumrekebisha mtoto kama kakosea bila kutumia viboko la sivyo yanaweza kukukuta usiyotegemea hata kama mtoto umemzaa wewe, tambua kwamba mtoto analindwa kwa sheria mbalimbali

Huyo DC kachemka sana inatakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu na mamlaka yake
Shukurani kwa hili darasa, mkuu!
 
Hata mimi nimefurahishwa sana,inatakiwa DC na RC wote wawe wa kiume siyo mkuu wa wilaya anakuwa mwanamke mrembo hata kukaripia maovu hawezi.

Hivi mnajua kwa nini Baba wa Taifa Nyerere aliteua wanajeshi tu?
Wewe humtakii mema miss kidoti, lakini ukiumia shauri yako, kuna ‘afsa’ huko Kisarawe alitumbuliwa hivi hivi!
 
Unapo mchapa mtoto kwa kukosea jambo fulani huwa unaenda mahakani kuthibitisha?
Azizi angalia mambo kwa upana. Wale waliochapwa si watoto, halafu wale wanatakiwa kushtakiwa kwa kuhujumu mali za serikali yetu. Kinyume na hapo tuachane na utaratibu tuliojiwekea tuamie kwenye viboko na adhabu za papo kwa hapo kwa utashi wa kiongozi.
 
Alisikika Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Ndg. Kenani Kihongosi akisema, "Tutafundishana uzalendo mpaka tutaelewana vizuri" huku akiwatandika viboko wahujumu wa mali za serikali.

Mimi naungana nae na nadiriki kusema tunahitaji viongozi kama hawa wazalendo na wakali kwa watu wote ambao ni wahujumu wa mali za serikali, kwa hakika taifa letu litasonga mbele.

Endelea kuchapa kazi Kiongozi, watanzania tunaojitambua tupo pamoja nawe na tunaendelea kukuombea afya tele kwa Mungu wetu wa Mbinguni.

Pamoja Tuijenge Tanzania
Huyu dogo mpuuzi yuko smart ila ujinga bado haujatoka kichwani
 
Hata sisi wananchi tupewe ruhusa ya kuwachapa viboko viongozi wasiowajibika Kama ulihaidi ahadi wakati wa kuomba kura na utaki kuitekeleza ni viboko tu. Maana pasipo fimbo atuendi
 
utafungwa wewe nenda kasome vizuri sheria ya mtoto, (The Law of the Child Act 2009) inakataza adhabu kwa mtoto bila utaratibu
Ni Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 ambayo inampa mamlaka waziri wa elimu kutunga kanuni za masuala mbalimbali zitakazokidhi utekelezaji wa masuala ya sheria hiyo. Mojawapo ya kanuni zilizotungwa ni The Education (Corporal Punishment) Regulation G.N.294 ya mwaka 2002. Kanuni hizi zinatoa mwongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani.

Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4 kwa tukio lolote.

Sheria inampa mamlaka mwalimu mkuu wa shule husika kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa adhabu hiyo.Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.

Kanuni ya (5) inataka kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu, ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu. Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na mkuu wa shule.

Sheria hii inataka uchunguzi na kujiridhisha kuwa mwanafunzi amehusika moja kwa moja na kosa analotuhumiwa nalo ndipo hatua ya kupeleka suala lake mbele ya mwalimu mkuu ili....
Kwa uhalisia umesoma shule gani inayofuata huo utaratibu, nakazia mwanafunzi anastahili viboko anapokosea au kuhisiwa Kama katenda kosa
 
Back
Top Bottom