DC Hai atengua uhamisho wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Lyamungo, anusa harufu ya upigaji pesa ya ukarabati

DC Hai atengua uhamisho wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Lyamungo, anusa harufu ya upigaji pesa ya ukarabati

REO. na RAS kilimanjaro, ni wapiga dili ndio ukweli.kwa sababu. Aliyemuandikia mwalimu barua ya kuhama mwalimu wa lyamungo sekondari Mkurugenzi wa wilaya ya Hai amekiri kuwa ni REO na RAS kilimanjaro,na siku hiyo hiyo kwenye akaumt ya shule ziliingizwa TSH milion 800.kwa mantiki hiyo takukuru imerahisishiwa kazi ni kukamata REO na RAS kilimanjaro,then uchunguzi inaanza,kwenye uchunguzi watakamata watu kibao waTamisemi.peleka mahakamani,
Lakini unaandika ovyo na kufanya mawazo yako yawe ovyo.Jitahidi kwenye uandishi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
REO. na RAS kilimanjaro, ni wapiga dili ndio ukweli.kwa sababu. Aliyemuandikia mwalimu barua ya kuhama mwalimu wa lyamungo sekondari Mkurugenzi wa wilaya ya Hai amekiri kuwa ni REO na RAS kilimanjaro,na siku hiyo hiyo kwenye akaumt ya shule ziliingizwa TSH milion 800.kwa mantiki hiyo takukuru imerahisishiwa kazi ni kukamata REO na RAS kilimanjaro,then uchunguzi inaanza,kwenye uchunguzi watakamata watu kibao waTamisemi.peleka mahakamani,
Ila umesema pointi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DC Sabaya unahangaika sana.
Umeamua kuja hadi jf kutafuta sifa za kijinga!!! It's what it's.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sifa,hapa kaumbua matendo yaliyokuwa yamejificha kwa muda mrefu.Suala hili likifuatiliwa kuna madudu yataanikwa wazi.Kuna uonevu wa kipigaji sana kama huo alivyofanyiwa mkuu huyo wa shule.Rais anapambana sana na mambo kama haya lakini bado kuna utemi utemi wa kipigsji sana.

Kwa hili,DC yupo right 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dc wa Hai angetupia macho na Utendaji wa idara ya Ardhi hapo kwenye wilaya yake; angewasaidia sana wananchi wa wilaya hiyo. Idara hiyo inanuka rushwa; title deeds hazitoki bila hongo!!! Amuulize huyo afisa wake wa Ardhi [ JACOB] kwanini anawazungusha watu kupata hati zao?
Huna akili. Issue ya shule na Ardhi wapi na wapi. Kwa taarifa yako ktk mambo mazuri aliyoyafanya DC Sabaya hapo Hai ni pamoja na suala la Ardhi. Migogoro amemaliza hapo wilayani. Issue ya title sidhani kama anatoa afisa Ardhi,hiyo ni issue ya Kamishna wa Ardhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko hivi, Serikali ilitoa milioni 700+ kwa ajili ya ukarabati wa shule.

Pesa imeingia kama leo, kesho yake headmaster anapokea barua ya uhamisho kwenda shule nyingine wilaya hiyo hiyo kama headmaster.

Kisa cha kuhamishwa anadaiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na wenzake, pia hakupewa muda wala barua ya kumuita ahojiwe makosa yake.

DC kawasomea mwongozo wa hizo pesa headmaster atakuwa msimamizi mkuu na ndiye atasimamia pesa zote na kamati zitakazoundwa.

Akasema hapa ndipo tatizo.

Wambieni hilo dili sio serikali ya Magufulii huyu headmaster hatoki na mkurugenzi kaambiwa aandike barua kufuta huo uhamisho.

Aisee bado TAMISEMI hawajashtuka hii sio serikali ya dili kama walivyozoea enzi hizo, inasikitisha sana.

Well done Mr DC salute kwako mzee wa Hai.

Wamejisahau kwa awaking hii sio ya kupiga, wawaulize lugola na kigwangala.
 
Safi Sana DC !! hao walimhamisha mkuu wa shule ili wamweke mtu wao awasaidie kufanya ubadhirifu.
 
Iko hivi, Serikali ilitoa milioni 700+ kwa ajili ya ukarabati wa shule.

Pesa imeingia kama leo, kesho yake headmaster anapokea barua ya uhamisho kwenda shule nyingine wilaya hiyo hiyo kama headmaster.

Kisa cha kuhamishwa anadaiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na wenzake, pia hakupewa muda wala barua ya kumuita ahojiwe makosa yake.

DC kawasomea mwongozo wa hizo pesa headmaster atakuwa msimamizi mkuu na ndiye atasimamia pesa zote na kamati zitakazoundwa.

Akasema hapa ndipo tatizo.

Wambieni hilo dili sio serikali ya Magufulii huyu headmaster hatoki na mkurugenzi kaambiwa aandike barua kufuta huo uhamisho.

Aisee bado TAMISEMI hawajashtuka hii sio serikali ya dili kama walivyozoea enzi hizo, inasikitisha sana.

Well done Mr DC salute kwako mzee wa Hai.
DC kamrudisha ili ampe muongozo wa kupiga hizo pesa,sabaya ni tapeli na ndio mana kwenye gari yake akiwa chuga hukosi matapeli sugu humo ndani.
Omary matelephone na kundi zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dc wa Hai angetupia macho na Utendaji wa idara ya Ardhi hapo kwenye wilaya yake; angewasaidia sana wananchi wa wilaya hiyo. Idara hiyo inanuka rushwa; title deeds hazitoki bila hongo!!! Amuulize huyo afisa wake wa Ardhi [ JACOB] kwanini anawazungusha watu kupata hati zao?
Namjua huyo jamaaa kanisumbua kiazi yule
 
REO. na RAS kilimanjaro, ni wapiga dili ndio ukweli.kwa sababu. Aliyemuandikia mwalimu barua ya kuhama mwalimu wa lyamungo sekondari Mkurugenzi wa wilaya ya Hai amekiri kuwa ni REO na RAS kilimanjaro,na siku hiyo hiyo kwenye akaumt ya shule ziliingizwa TSH milion 800.kwa mantiki hiyo takukuru imerahisishiwa kazi ni kukamata REO na RAS kilimanjaro,then uchunguzi inaanza,kwenye uchunguzi watakamata watu kibao waTamisemi.peleka mahakamani,

Watawakamata kwa kosa gani kwani mpunga washaupiga?mission si imefeli bwana,labda kuwaondoa tu administrativelly sababu ya kuwa na nia ovu au kufanya vitu bila utaratibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dc wa hai ametufumbua sana macho.. Tusisubiri corona hii ya utapeli ikasambaa

Wakati muafaka serikali ianze kuzisimamia pesa zote zinazopelekwa mashulen kwa kazi yoyote

Ikumbukwe n kodi za wananchi ndizo zinasambazwa mashuleno

Kwa yaliyotokra lyamungo sec nilitarajia alieandika barua kwa mkk wa shule aondolewe mkurugenzi alieasaini pale hai hio barua wote waondolewe kabosa wapangiwe kazi zingine

Kumekuwa na upigaji sana tamisemi imefika wakati upigaji uangaliwe madharayake na faida yake angalia hapo mnapopigia mtotowako akienda kusoma itakuwaje kama awatakarabati madarasa maabara.

Wakati muafaka kusikia walioshiriki kutaka kumwondoa mwl mkuu lyamungo wote waondolewe posn zao hii n miradi mikubwa kati ya walimu wakuu na maofisa wa pale juu

Tukiliacha hili litasambaa zaidi ya corona
 
Naona DC kamuweka mtu wake ili wazipige vizuri hizo pesa za ukarabati
 
Siku chache Mara baada ya serikali wilayani Hai kusitisha uhamisho wenye utata wa Mkuu wa shule ya sekondari Lyamungo ,Adriano Mushi Mazito yameibuka huku chanzo kikielezwa ni fedha zilizotolewa na rais Magufuli sh,milioni 800 kwa ajili ukarabati wa shule hiyo.

Sakata la kuhamishwa ghafla kwa Mkuu huyo wa shule iliamuliwa na katibu tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (RAS),kwa madai kwamba hana mahusiano mazuri na walimu wenzake na kutakiwa kuhamia shule ya sekondari Lemira iliyopo wilayani humo.

Kwa mujibu wa barua ya Tar 23 mach,2020 iliyoandikwa na Shukuru Maleo ambaye ni fundi ujenzi kwenda kwa Mkuu wa shule ya sekondari Lyamongo akiomba kibarua cha ujenzi katika shule hiyo ,inaonyesha kwamba Flugence Mponji ambaye ni msimamizi wa miradi ya elimu mkoani humo ndiye aliyemdhamini fundi huyo aweze kupata kibarua .

Baada ya fundi huyo kuwasilisha barua yake ya maombi ya ujenzi April mosi mwaka huu,bodi ya shule hiyo iliketi na kufanya maamuzi ya kupitia maombi ya kazi ,ambapo kati ya majina yaliyopitishwa jina la Shukuru Maleo aliyetambulishwa na Mponji kwa mkuu wa shule halikuwepo hapo ndipo kimbembe kilipoanzia.

Hatua hiyo iliibua mtafaruku na chuki baina ya Mkuu wa shule hiyo na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya mkoa na kwamba mnamo tar 9,April mwaka huu Mkuu huyo wa shule alipokea barua ya uhamisho .

Kutokana na uhamisho huo wa ghafla wa Mkuu huyo wa shule baadhi ya walimu,wazazi na wananchi mbalimbali walihoji sababu ya uhamisho huo hasa Katika kipindi ambacho shule ilipokea sh, milioni 800 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo Kongwe wilayani humo.

Hata hivyo wakati sekeseke hilo likiendelea kuliibuka tetesi kwamba kuna kamati iliundwa kwa ajili ya kufuatilia mahusiano ya Mkuu huyo na walimu wenzake na kwamba taarifa ya kamati hiyo ilidai kwamba mwalimu huyo hakuwa na mahusiano na walimu wenzake .

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye kwa mujibu wa taratibu ndiye mwajiri wa Mkuu huyo wa shule hakushirikishwa suala hilo na kwamba hata Mkuu huyo pia hakuhojiwa na kamati hiyo.

Jambo hilo limeonyesha wazi kwamba kunampango wa maksudi ili kumwondoa Mkuu huyo wa shule kwa lengo la upigaji wa fedha hizo kutokana na kwamba Mkuu huyo alikuwa akisimamia utaratibu wa matumizi sahihi ya fedha za umma suala ambalo liliwachukiza baadhi ya wakuu wake wa kazi na kuamua kumhamisha ili kupata mianya ya kuchomeka watu wao katika mradi huo ili kujipatia maslahi binafsi.

Suala hilo linaibua dhana mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka na uonevu iliyofanywa na ofisi ya katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro na ni mwendelezo wa ukandamizaji wa watumishi wa kada za chini na kati hali ambayo imekuwa ikikemewa na rais John Pombe Magufuli.

Bila shaka vyombo vya dola ikiwemo Takukuru vitafuatilia kwa undani suala hili na kuibua yanayofanywa katika ofisi ya RAS na itakuwa mwanzo mzuri wa kulindwa kwa haki za wanyonge wanaonyanyasika mahala pa kazi.

End...

IMG-20200417-WA0013.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari niliiona,yaani jamaa wamecheza mchezo wa kijinga sana..hawakusoma alama za nyakati..hata hivyo pongezi zimuendee mkuu wa wilaya kwa kustukia harufu ya upigaji.
 
Back
Top Bottom