DC Hai atengua uhamisho wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Lyamungo, anusa harufu ya upigaji pesa ya ukarabati

Upigaji hauwezi kuisha nchini! Na sababu kubwa ni kutokuwepo kwa mgawanyo walau unao karibiana wa keki ya Taifa. Wanao faidi ni wachache.

Na ndiyo maana kila anayepata fursa, hujiangalia yeye kwanza badala ya ile jamii anayo ihudumia.
 
Duh! Hapo hadi sasa naona kama kuna nafasi ya wazi ya RAS na REO, mungu nijaalie niipate mie moja ya nafasi hizo! Maana watu wanazichezea na hawaridhiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Informer wake wapo vizuri sana kwa kunusa harufu hii
Hakuna kitu,mbona ile issue ya reli walinusa hewa,iliishia wapi,mbona kimya mpaka leo? Hata hii tutajua tu jinsi walivyonusa hewa.Fuatilia vizuri,utajua tu.
 
Kiutumishi hana uwezo huo.
Lakini kwa awamu hii, katiba na sheria za nchi havina maana yoyote. Lolote asemalo mkubwa kwa utashi wake hufanyika.
 
Dili nyingi za upigaji halmashauri zinaanzia TAMISEMI hadi wizara ya fedha.

Zikishapigwa pesa,kila kitu kinaenda sawa kuanzia taarifa ya utekelezaji,ukaguzi wa ndani na nje pia.

Hakuna siku utasikia popote kuna hela zimepigwa.Labda ukute mbunge aliyepo ni CCM tena awe machachari.Akiwa upinzani,watasema mmezoea kulalamika kila kitu.Hakuna kitakachofuatiliwa.Ila namuona PM kama mtu makini sana.Anafanya kazi bila mhemko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitashangaa sana iwapo RAS na REO mkoa wa Kilimanjaro Kama Hadi sasa hawajachukua hatua za kujiizulu au wanagojea Hadi wasimamishwe kazi kwa aibu .ninawashauri wawajibike haraka iwezekanavyo
 
Huyu ndio Masai wa kweli. Sokoine mwingine huyu. Hapindishi wala kumumunya maneno. He is always firm on issues!

Hongera Simba.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikilizeni mkuu wa shule ya sekondari Lyamungo.ili mtambue afisaelimu mkoa wa Kilimanjaro na RAS mchezo wanao ufanya kuonea walimu ili waweze kupata njia ya kuiba fedha za serikali.Takukuru sikilizeni hii clip mjue pa kuanzia kukamata watuhumiwa.Dc hai shujaa.Mwl Paulina,REO Kilimanjaro,unangoja Hadi usimamishwe kazi?jiwajibishe mwenyewe.
 

Attachments

  • VID-20200419-WA0013.mp4
    25.2 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…