DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Hivi nini maana ya Kichaa?!
 
Huyu DC hana maadili ya uongozi,huwezi kugombana hadharani na mtu mnayefanya naye kazi pamoja.Its a cheap popularity and abuse of power.
 
I dont have that look
 
Jinyoosheni wenyewe....tu
 
Hii nchi imearibiwa sana..how on earth Jerry muro anakuwa dc??
 
Huyu mkurugenzi nae alishiriki kununua madiwani kipindi Mnyeti akiwa DC,sasa nae aonje ladha halisi ya mambo aliyoyatamani kutokea. Watu hawana hofu
 
Mi nafikiri.
Busara ni kuwaacha hao watu.
WATIFUANE.
 
Muda utaongea hata aliemshika shati kumuweka hapo alipo...nae alianza kwa style hizo hizo za kudhalilishana,,,,,,,,,sasa nadhani ameanza kuelewa kuwa kuna maisha baada ya vyeo kuteuliwa .......ambapo kesho tuu unaachwa!!
 
upuuzi wa hali ya juu huu, haya ndio yale madaraka ya kukosa hekima, busara na weledi. watu wanachukuliwa mtaani na kupewa vyeo kama hivi na haya ndio matokeo yake.
Ilishindikana nini kumuuliza kwanini alichelewa tena kwa taratibu badala ya njia kama hii? huenda kulikuwa na dharura kubwa kiofisi. Shame on him!
 
Huyo jerry mbona ni mpenda sifa toka akiwa mwandishi habari....yani anapenda kudominate hadhira....tuseme amina!!
 
Msomi kama huyu anakubali kudhalilishwa na 'msaka tonge'! aisee nami ningemjia juu tena kwa sana hadi aone cha moto! mie ni mteule wa raisi kama yeye! kama vipi nirudi zangu chuoni!
 
DED NI PHD HOLDER na ni mkurugenzi wa Arusha DC
 
Huu upuuzi kabisa jiwe anateua wapuuzi kwenye nafasi ambazo hawana taaluma nazo
Lakini tukumbuke kuwa wanaiga toka kwa Jiwe kwa namna anavyoendesha nchi na yeye Jiwe mwenyewe anafurahia namna hao PhD holders wanavyodharirishwa mbele ya media!
 
PhD holder ana mshahara mkubwa kuzidi wa DED, DC hata mkuu wa Mkoa. Ukiongeza na uwezekano wa consultancy na winning big project, ni nonsense kuwa DED then ukatukanwa na vijana wa CCM. Pamoja kuna umuhimu wa kuwa na DED msomi ili atumie tafiti kuleta maendeleo ila ni aibu kutukanwa mbele za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…