DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Wateule wa Mh Rais wanakosea sana katika utendaji wao. Mambo kama haya anayofanya Jerry Muro ni kinyume na misingi ya Uwajibikaji katika nafasi za uongozi. Kiongozi hapaswi kumfokea na kumdhalilisha kiongozi mwingine hadharani.
Lakini tukumbuke kuwa wanaiga toka kwa Jiwe kwa namna anavyoendesha nchi na yeye Jiwe mwenyewe anafurahia namna hao PhD holders wanavyodharirishwa mbele ya media!
 
Na Malisa GJ

Mkuu wa Wilaya Jerry Muro anamtukana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dr.Wilson Mahela (PhD) mbele ya Mkuu wa mkoa na macamera ya waandishi wa habari yanawamulika. Uongozi wa kijinga sana huu. Kanuni za maadili ya uongozi haziruhusu kufanya huu utoto. Kama Mkurugenzi alichelewa kufika, kuna namna bora ya kumuwajibisha ambayo ingekua na tija kuliko huu ujinga uliofanya Jerry. Tatizo mnateuliwa teuliwa tu bila hata kupewa semina elekezi.

Mtu hajawahi kuwa hata CR darasani leo anakuwa DC ama RC what do u expect? Matokeo yake ndio haya ya kuja kutukanana hadharani na mnaona sifa kurekodiwa. Halafu wewe Jerry sio mamlaka ya nidhamu ya DED. Pengine huo uDC umekulevya. Mamlaka ya nidhamu ya DED ni RAS. Kwahiyo kama alichelewa ungeweza kuzungumza nae baadae na kumueleza masikitiko yako, na kama angekaidi ungemripoti kwa RAS. Sio kutukanana hadharani.

Unamtukana DED na kumuita mpuuzi na mpumbavu hadharani, halafu unategemea awasimamie watendaji wa Halmashauri. How that possible? Atawasimamiaje wakati wameona akiitwa mpuuzi na mpumbavu hadharani? Na wenyewe watampuuza tu kama ulivyompuuza wewe. Ni aibu viongozi kuzozana hadharani. Wahenga walisema wazazi wapumbavu pekee ndio wanaoweza kugombana mbele ya watoto. Kulikua na tatizo gani mngeendelea na hiyo ziara then badae mkae na kujadili?

Halafu kichekesho unamlaumu DED kwa kuchelewa dakika 10, lakini wewe umepoteza dakika nyingi zaidi kumtukana. Hivi lengo lako lilikua kuokoa muda kweli?

Huyu Dr.Wilson Mahela ni PhD holder. Amefundisha chuo kikuu UDSM muda mrefu wakati wewe ukifanya ukanjanja kwenye media. Amekuzidi umri, amekuzidi elimu, amekuzidi busara. Kama umeshindwa kumheshimu kwa nafasi yake basi ungemheshimu hata kwa umri wake tu.

Then huyo DED unayemdhalilisha ndo anayekuweka mjini. Tunajua maDC hamna budget. Mnalelewa na ofisi za DED kwa kila kitu. Hadi mafuta ya gari mnaomba kwao. Sasa how comes unamdhalilisha mtu anayekufanya usurvive? Kesho ukimuomba mafuta akikunyima utamfanya nini? Au ndo utaita tena macamera uanze kumtukana? Growup na uache sifa za kijinga. Uongozi ni kujifunza. Take time to learn from your elders kabla ya kukurupuka. Unajidhalilisha na kumdhalilisha aliyekuteua.!
Malisa let's just celebrate.... Wakati si milele.... Watunza kumbukumbu wapo na hawaachi kitu...
tapatalk_1536159688757.gif
 
Wateule wa Mh Rais wanakosea sana katika utendaji wao. Mambo kama haya anayofanya Jerry Muro ni kinyume na misingi ya Uwajibikaji katika nafasi za uongozi. Kiongozi hapaswi kumfokea na kumdhalilisha kiongozi mwingine hadharani.
Lakini tukumbuke kuwa wanaiga mfano toka kwa Jiwe kwa namna anavyoendesha nchi na yeye Jiwe mwenyewe anafurahia namna hao PhD holders wanavyodharirishwa mbele ya media

Wacha dereva Jiwe atutumbukize shimoni katika safari yake ya Lori analoliendesha, iwapo hatutampumzisha dereva Huyu
 
That is not how we are supposed to serve.

Kama mwanachama mtiifu wa CCM ambayo inajukumu la kuisimamia Serikali.

Naomba mheshimiwa D.C. aonywe na mamlaka ya uteuzi.
Kisa hujateuliwa hahahaaaa chama bomu hili
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile

Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'
Kwahiyo "dakika 10 tu" umemaanisha nini? Unaona dkk 10 ni muda mfupi sana? Ndio maana waafrika tuko nyuma sana, hatujui thamani ya muda. Na huyo ni DED ambaye ana gari na dereva. Tujifunze kuthamini muda.

Siku moja dada mmoja alienda ofisi fulani kwa bodaboda, kabla hajaingia ofisini akamwambia jamaa amsubiri dkk chache warudi nae, dada kakaa humo zaidi ya dkk 20. Alivyotoka jamaa akamwambia naomba kwanza sh 2,000 ya kuniweka hapa kabla hatujaondoka. Dada akakataa likazuka zogo jamaa kidogo amshushie dada kichapo baadhi ya watu wakaja pale kuamua na ikaonekana dada ana makosa msamaria fulani akatoa ile 2,000

Na maofisini ndio kuna ujinga zaidi, yani unaenda kwa ajili ya kuhamisha mtoto unaambiwa subiri, unakaa huko masaa kadhaa watu wanapiga zao story tu. Ukiingia tena ofisini jamaa anachukua fomu zako anasaini anakwambia hapa tayari nenda mkoani. Unajiuliza yani kumbe ilikuwa kusaini tu?

Pamoja na ukweli kuwa viongozi lazima waheshimiane lakini pia hata huyo DED kwa kuchelewa maana yake hakuwaheshimu DC na RC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Malisa GJ

Mkuu wa Wilaya Jerry Muro anamtukana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dr.Wilson Mahela (PhD) mbele ya Mkuu wa mkoa na macamera ya waandishi wa habari yanawamulika. Uongozi wa kijinga sana huu. Kanuni za maadili ya uongozi haziruhusu kufanya huu utoto. Kama Mkurugenzi alichelewa kufika, kuna namna bora ya kumuwajibisha ambayo ingekua na tija kuliko huu ujinga uliofanya Jerry. Tatizo mnateuliwa teuliwa tu bila hata kupewa semina elekezi.

Mtu hajawahi kuwa hata CR darasani leo anakuwa DC ama RC what do u expect? Matokeo yake ndio haya ya kuja kutukanana hadharani na mnaona sifa kurekodiwa. Halafu wewe Jerry sio mamlaka ya nidhamu ya DED. Pengine huo uDC umekulevya. Mamlaka ya nidhamu ya DED ni RAS. Kwahiyo kama alichelewa ungeweza kuzungumza nae baadae na kumueleza masikitiko yako, na kama angekaidi ungemripoti kwa RAS. Sio kutukanana hadharani.

Unamtukana DED na kumuita mpuuzi na mpumbavu hadharani, halafu unategemea awasimamie watendaji wa Halmashauri. How that possible? Atawasimamiaje wakati wameona akiitwa mpuuzi na mpumbavu hadharani? Na wenyewe watampuuza tu kama ulivyompuuza wewe. Ni aibu viongozi kuzozana hadharani. Wahenga walisema wazazi wapumbavu pekee ndio wanaoweza kugombana mbele ya watoto. Kulikua na tatizo gani mngeendelea na hiyo ziara then badae mkae na kujadili?

Halafu kichekesho unamlaumu DED kwa kuchelewa dakika 10, lakini wewe umepoteza dakika nyingi zaidi kumtukana. Hivi lengo lako lilikua kuokoa muda kweli?

Huyu Dr.Wilson Mahela ni PhD holder. Amefundisha chuo kikuu UDSM muda mrefu wakati wewe ukifanya ukanjanja kwenye media. Amekuzidi umri, amekuzidi elimu, amekuzidi busara. Kama umeshindwa kumheshimu kwa nafasi yake basi ungemheshimu hata kwa umri wake tu.

Then huyo DED unayemdhalilisha ndo anayekuweka mjini. Tunajua maDC hamna budget. Mnalelewa na ofisi za DED kwa kila kitu. Hadi mafuta ya gari mnaomba kwao. Sasa how comes unamdhalilisha mtu anayekufanya usurvive? Kesho ukimuomba mafuta akikunyima utamfanya nini? Au ndo utaita tena macamera uanze kumtukana? Growup na uache sifa za kijinga. Uongozi ni kujifunza. Take time to learn from your elders kabla ya kukurupuka. Unajidhalilisha na kumdhalilisha aliyekuteua.!

Mkuu naomba nirekebishe hili bandiko kdg, amemuita mpuuzi na siyo mpumbavu, by the way katika vijana wajinga waliopewa madaraka yasiyo endana na uwezo ni pamoja na Jerry Muro! Hapa JPM aliteleza! Kampani ya Le mutuz, Bashite hii unategemea nini???
 
Muro alikuwa sahihi kabisa kumfokea huyo DED.
Haiwezekani Mkuu wa Wilaya awahi safari pamoja na Bosi wake Mkuu wa Mkoa, na wakae wamsubiri DED ambaye ni mdogo kicheo.
Mkuu wa Wilaya lazima amkaripie DED kwa kumchelewesha yeye DC, pamoja na bosi wake Gambo RC
Wa kukaripia hapo ni DC Jerry Muro na sio RC Gambo
Hapo Protokali imezingatiwa kabisa.
Vijana wako kazini kwa ari na kasi kubwa, tuache mazoea ya kizamani.
Tusihamishie hasira zetu toka juu na kuzileta chini kwa hao vijana.
 
Gambo tangu aambiwe wapumbavu sn ninyi baada ya kufeli movie ya kuwaleta wahamaji amepotea
 
Back
Top Bottom