DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Madaraka ya kulevya matamu sana ndo maana ata mtu akiharibu zaidi kujiengua hataki ndo wanachopenda kufoka hivo
 
hizi takataka zinazo itwa DC na RC zinapata kiburi sababu tu zina tumia sheria ya kipumbavu ya kuweka watu ndani kwa kutumia jeshi la polisi na hapo tu ndipo wanapo jiona wao wapo juu kuliko wengine lakin nje ya hapo ni taka taka tuu
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile



Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'
Anautafuta ukuu wa mkoa wa Arusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kwanza kwa haraka haraka unaweza sema anamwambia gambo
 
Mimi sijaelewa hapa.

Yaani Darasani yupo Mwalimu, alafu kaingia Mwanafunzi kachelewa Monitor ndio anamfokea Mwanafunzi huyo mbele ya Mwalimu.

Hapa kuna mawili, Monitor anajiona ni Mjuaji kuliko hata Mwalimu, au Mwalimu haoni kosa la huyo Mwanafunzi linalostahili kufokewa.
 
Mkuu nimeona umezungumza maoni yako ambayo kiasi kikubwa uko sahihi, Ila kabla ya kumdhalilisha mtu kwenye umma lazima uwe na uhakika wa kile kilichomfanya yeye kuchelewa hapo alipo.Labda kwa kuzungumza ukweli ninaoufahamu juu ya tukio kwa sababu mimi naishi na huyu mkurugenzi kwake ila pia siwezi kuzungumza kwa kutetea upande wowote lakini nitazungumza namna stori ilivyokuwa na dr alivyofika nyumbani alivyotuambia nini kilitokea kabla ya kuenea mitandaoni.Ilikuwa ni juzi siku ya Jumanne usiku wakati mkurugenzi anarudi nyumbani alitukuta tumekaa sebuleni tunaangalia filamu ya marehemu Steven Kanumba dar 2 lagos chanel ya St swahili, alivyofika baada ya kumsalimia alikuwa tofauti na tulivyomzoea yaani hakuwa na furaha kuna simu ikawa imeingia ya kiongozi mmoja hivi wa serikali akamuuliza mkutano wenu umeendaje, akwambia haukuwa vizuri kulikuwa na tatizo baada ya kusikia hivyo ilibidi kupunguza sauti ya tv ili kusikiliza kilichotokea baada ya kuongea na simu akaanza kutuelezea ilivyokuwa.
Kwa kifupi ilikuwa hivi...... Asubuhi ya Jumanne viongozi hawa yaani Dc, Rc, Rpc, Ded na wengine walikuwa wamepanga kwenda ziara nahisi ilikuwa Arumeru hivyo wakati wanajiandaa kuondoka pale ofisini Mkurugenzi akawa amesahau baadhi ya documents ofisini hivyo akaomba kuzichukua haraka ili waondoke wakati anachukua documents hizo, akatoka nje akakuta msafara umeshaondoka ikiwepo gari ya King'ora ambayo hufanya gari na watu barabarani kupisha msafara hivyo basi akapanda kwenye gari lake na kuondoka ili kuwahi,Hivyo basi kutoka ofisini Sekei hadi kwenye mkutano Arumeru kulikuwa na foleni sana njiani pia Magari na watu hawa kupisha gari ya Mkurugenzi kwa sababu hakukuwa na gari ya king'ora kuonesha kuwa anawahi sehemu.
Baada ya purukushani hizo Mkurugenzi alifanikiwa kufika akiwa amechelewa kati ya dakika tano hadi kumi kwa hiyo kabla hajaeleza kitu chochote ndio akakutana na fedheha ya namna hii.Hivyo basi ningependa kushauri mtu yoyote kabla ya kutoa hukumu au kumuona mtu .. amekosea ni bora kwanza kusikiliza nini kimesababisha tatizo. kwa hiyo kwa tukio hili la Jumanne mheshimiwa Jerry Muro alikuwa akijua kabisa mkurugenzi amechelewa kwa sababu walimuacha bila kumpa taarifa wakati walikuwa pamoja na alikuwa anachukua documents ambazo ni mhimu kwa ajili ya mkutano wa siku ile hivyo inaweza kuwa Dc alifanya hivyo aidha kwa kupanga au bila kufikiria.
Ila Jerry ana tatizo la kupanic sana apunguze mihemko cheo ni dhamana kuumbuana vile haipendezi si angemwambia pembeni, kujitaftia umaarufu kwa kuumiza wengine huwa kuna mwisho mubaya, mi mwenyewe naona Jerry ali overeact had wa pembeni wakaona aibu, pia kuna video alimfunga mwananchi bila kumsikiliza mbona Joketi anafanya vzuri na hana mihemko ya kuzalilisha watu.
 
Ila Jerry ana tatizo la kupanic sana apunguze mihemko cheo ni dhamana kuumbuana vile haipendezi si angemwambia pembeni, kujitaftia umaarufu kwa kuumiza wengine huwa kuna mwisho mubaya, mi mwenyewe naona Jerry ali overeact had wa pembeni wakaona aibu, pia kuna video alimfunga mwananchi bila kumsikiliza mbona Joketi anafanya vzuri na hana mihemko ya kuzalilisha watu.

kweli mfano baadhi ya hizi video
 

Attachments

Aisee Muro hajiamini. Tulidhani Jokate ndio ataharibu zaidi.. kumbe mzee mzima ndio anaxidi kuharibu kwa KUPANIK.
Mara amsemee mbovu mbunge Nasary. Hivi Muro ile ofisi ya one room unataka ufanyie nini ? Hopeless and bogus guy
 
Katika hali ya kuonesha kujisahau, kupitiwa au kutozoea nafasi yake, Jerry muro alijikuta akijitambulisha kama mkuu wa mkoa badala ya mkuu wa wilaya....

Clipp hii hapa chiniView attachment 859349
Ndoto za mchana huwaga za kweli ujue, we subiri atakapoletwa Mzizima hapo halafu huyo wa mzizima akapewa wizara ya simu na ndege (dreamliner)!
 
Katika hali ya kuonesha kujisahau, kupitiwa au kutozoea nafasi yake, Jerry muro alijikuta akijitambulisha kama mkuu wa mkoa badala ya mkuu wa wilaya....

Clipp hii hapa chiniView attachment 859349

Ushauri wangu tusimjadili Jerry Muro huku mioyoni mwetu tukiwa tumetawaliwa na itikadi zetu za Uchama / Usiasa bali tumjadili Kiutendaji zaidi. Ndiyo anaweza akawa ana mapungufu yake kama Binadamu yoyote yule ila nasi pia tusisahau kwamba Watendaji wengi wa Serikalini katika ngazi mbalimbali walikuwa wameshajisahau, wamelemaa na kuzifanya Ofisi za Serikali kama vile ni kwa Wajomba na Shangazi zao. Kwa maoni yangu ni mapema mno kama siyo sana kuanza kusema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro hafai / hatoshei katika hiyo nafasi.
 
Back
Top Bottom