DC Jokate Mwegelo atoa siku saba kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao

Idadi polisi sio kubwa kiasi cha kuwawezesha kulinda mitaa na vitongoji vyote vya nchi hii.
Hivyo Ulinzi Shirikishi ni muhimu sana. Muhimu ni kuwekwa utaratibu maalumu wa jinsi gani ufanyike na wananchi waelimishwe juu ya umuhimu wa wao kujilinda. Tukiwaachia Polisi kila kitu tutaendelea kupigwa
Yani nilinde sungusungu
Una utani wewe
 
Maswali ambayo DC alipaswa kuwauliza polisi:
1. Je walikuwa na taarifa za tukio?
2. Hizo taarifa walipata saa ngapi?
3. Je wananchi wana namba za simu za polisi?
4. Na kama hawana, wamefanya juhudi gani kuhakikisha wanazo?
5. Walifika kwenye eneo la tukio saa ngapi?
6. Kwa nini walifika muda huo na sio mapema zaidi?
7. Wana rejista ya taarifa wanazopata kuhusu matukio?
8. Je wanafanya doria? Kama hawafanyi, kwa nini hawafanyi?
Na akumbuke kuwa ulinzi shirikishi maana yake raia wanashirikiana na polisi. Hii ina maana wanakuwa na polisi wanapofanya doria ili kuhakikisha GPO inafuatwa. Vigilantes ni watu hatari, wakiachiwa peke yao watadhuru sana watu.

Amandla...
 
Ulinzi shirikishi ni hiari asilazimishe
Kama anataka ulazima waweke taa mitaa yote na cctv kwa hela za walipa kodi maana mmetukamua kila kona

Police patrol ni kazi yao kutulinda na mabunduki yao ama watulipe na bunduki wagawe (hapo nimeongea kama akili zao)
 
Tuliwaambia kipindi cha Magufuri wizi ulikoma,watu wakawa wanabisha,hatukuwahi kusikia hizi ngojera,kila mtu aliwajibika kwa kazi yake,sasa kazi ya polisi tunapewa sisi wananchi, wakati kuna watu wanakula mshahara na mavx kwa kodi ya mlala hoi,Kama polisi kazi imewashinda kuna jeshi la ziada liazimwe
Bas lifumuliwe tuajiriwe wananchi
 
Unadhani polisi wapo wengi wa kutosha kulinda kila mtaa?

Isitoshe suala la usalama/ulinzi huanzia kwa mtu binafsi.

Kama hutaki kuchangia ulinzi wako binafsi shauri yako.
Kwa hiyo kama hawatoshi serikali haina plani zaidi ya kuwapa wananchi kazi? Je silaha tunapewa ama?
 
Ulinzi shirikishi haupo kisheria na ni wa hiari, wananchi waelimishwe umuhimu wake na washawishiwe kujiunga nao na sio kutumia nguvu kama DC wangu anavyofanya, police ni wajibu wao kulinda raia na mali zao (wamekula kiapo),police watching na siasa na watekeleze wajibu wao bila y kuingiliwa na politicians. Wazo ni zuri ila lifanyike kiustaarabu sio vitisho(mrema na sungusungu yake...Adv.Mabere alimfundisha sheria)
Ulinzi Shirikishi upo kisheria mkuu wangu
 
DC. Jokate Mwegelo: Ametoa siku saba kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo ametoa siku saba kwa wenyeviti wa serikali za mitaa wilayani humo kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi.

Agizo hilo amelitoa leo Aprili 29,2022 alipokuwa akizungumza na wenyeviti hao katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo katika Manispaa hiyo.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka viongozi hao kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linapewa kipaumbele ili kuwezesha wananchi kuishi kwa usalama.

"Ninatoa siku 7 muhakikishe kule ambapo hakuna vikundi vya ulinzi shirikishi mnaanzisha vikundi hivyo na kule ambapo vilikuwepo ila vinalegalega mviimarishe".Alisema Mhe.Jokate

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam,Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa uhalifu unatokea pale ambapo hakuna ulinzi na kusisitiza kuwa suala la ulinzi ni jukumu la kila raia.

"Ili uhalifu utokee lazima kuwepo na fursa,na fursa ni pale ambapo hakuna ulinzi kwa kile ambacho mhalifu anachokusudia kufanya".Alisema Afande Muliro.

Kikao hicho ambacho kilihusisha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na baadhi ya vikundi vya ulinzi shirikishi kilikuwa na lengo la kuweka mikakati ya jinsi ya kukabiliana na wimbi la vitendo vya uhalifu ambavyo vimeanza kujitokeza kwa siku hizi za karibuni.

View attachment 2205003

View attachment 2205004

View attachment 2205005

View attachment 2205006

View attachment 2205007

View attachment 2205008
Vibaka wengi ni watoto wa hawa hawa viongozi ambao walikataa shule wenyewe.
 
Idadi polisi sio kubwa kiasi cha kuwawezesha kulinda mitaa na vitongoji vyote vya nchi hii.
Hivyo Ulinzi Shirikishi ni muhimu sana. Muhimu ni kuwekwa utaratibu maalumu wa jinsi gani ufanyike na wananchi waelimishwe juu ya umuhimu wa wao kujilinda. Tukiwaachia Polisi kila kitu tutaendelea kupigwa
Wakati wa jpm polisi walikuwa wangapi ? tumia akili kufikiri acha kutumia kijambio kufikiri
 
Unadhani polisi wapo wengi wa kutosha kulinda kila mtaa?

Isitoshe suala la usalama/ulinzi huanzia kwa mtu binafsi.

Kama hutaki kuchangia ulinzi wako binafsi shauri yako.
Wapo mbona wanapotaka kupiga watu virungu wanatoa lesho kuwa Askari mmoja anaweza kushugurikia watu 100, kwani hao vibaka ni wangapi? kipindi cha Magufuri walifanyaje mpaka hao panya wakakomeshwa, kingine Samia ndiye ameongeza hao vibaka, kufukuza machinga mtaani kumefanya vibaka kuongezeka maana wengine walikuwa wamejiajili kwa njia ya umachinga, Sasahivi Samia kawafukuza wote,unafikiri wataishije wasipo kaba watu?
 
Polisi wanataka kusukumia jikumu lao kwa raia wasio na ujuzi wala silaha.
Nashauri wale polisi wakali sana Kingai, Mahita, Goodluck na Jumanne wapelekwe Temeke wakapambane na panya road
 
DC. Jokate Mwegelo: Ametoa siku saba kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo ametoa siku saba kwa wenyeviti wa serikali za mitaa wilayani humo kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi.

Agizo hilo amelitoa leo Aprili 29,2022 alipokuwa akizungumza na wenyeviti hao katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo katika Manispaa hiyo.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka viongozi hao kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linapewa kipaumbele ili kuwezesha wananchi kuishi kwa usalama.

"Ninatoa siku 7 muhakikishe kule ambapo hakuna vikundi vya ulinzi shirikishi mnaanzisha vikundi hivyo na kule ambapo vilikuwepo ila vinalegalega mviimarishe".Alisema Mhe.Jokate

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam,Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa uhalifu unatokea pale ambapo hakuna ulinzi na kusisitiza kuwa suala la ulinzi ni jukumu la kila raia.

"Ili uhalifu utokee lazima kuwepo na fursa,na fursa ni pale ambapo hakuna ulinzi kwa kile ambacho mhalifu anachokusudia kufanya".Alisema Afande Muliro.

Kikao hicho ambacho kilihusisha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na baadhi ya vikundi vya ulinzi shirikishi kilikuwa na lengo la kuweka mikakati ya jinsi ya kukabiliana na wimbi la vitendo vya uhalifu ambavyo vimeanza kujitokeza kwa siku hizi za karibuni.

View attachment 2205003

View attachment 2205004

View attachment 2205005

View attachment 2205006

View attachment 2205007

View attachment 2205008
Macho mawili ya picha ya pili yanatosha kabisa kufanya huo ulinzi
 
Kwa hiyo polisi wanalipwa kwa kazi gani?
Does it mean ule upuuzi wa kulinda sungusungu?
Yaani nikeshe usiku nazunguka mitaani na rungu bila malipo halafu kesho yake niende ofisini kwangu?
Hivi vidangaji vya bongo muvi vilipewa vipi machaka kama haya!!!
"Yaani nikeshe usiku nazunguka mitaani na rungu bila malipo halafu kesho yake niende ofisini kwangu?"
[emoji23][emoji23][emoji119][emoji23][emoji119]
 
Ulinzi shirikishi haupo kisheria na ni wa hiari, wananchi waelimishwe umuhimu wake na washawishiwe kujiunga nao na sio kutumia nguvu kama DC wangu anavyofanya, police ni wajibu wao kulinda raia na mali zao (wamekula kiapo),police watching na siasa na watekeleze wajibu wao bila y kuingiliwa na politicians. Wazo ni zuri ila lifanyike kiustaarabu sio vitisho(mrema na sungusungu yake...Adv.Mabere alimfundisha sheria)
Imekuwa kama lazima.
Nilisikia fununu huku mtaani kwetu eti usipoenda kulinda unalipa elfu kumi.
 
Huyu DC sijajua ni kipi ataweza kufanikisha!! Kama kazi inamlemea Kwa Huruma zake, Fikiria unatoka Dar kwenda Mkuranga unakaa Mbagala masaa mawili Kwa foleni, sababu DC ameshindwa kupanga wafanya biashara!! Haoni huruma Kwa watu wanavyopotezewa muda!? Lile tatizo la Mbagala halihusiani na ujenzi WA barabara ila kukosa ufuatiliaji WA DC,
 
Wakati wa jpm polisi walikuwa wangapi ? tumia akili kufikiri acha kutumia kijambio kufikiri
Hivi huwezi kujibu hoja kwa ustaarabu bila kutukana? Kuna sehemu yoyote kwenye hoja yangu nimetukana? Anyway nimesamehe. Acha maisha yaendelee
 
Kwa hiyo polisi wanalipwa kwa kazi gani?
Does it mean ule upuuzi wa kulinda sungusungu?
Yaani nikeshe usiku nazunguka mitaani na rungu bila malipo halafu kesho yake niende ofisini kwangu?
Hivi vidangaji vya bongo muvi vilipewa vipi machaka kama haya!!!
Ulinzi shirikishi ni jambo la kawaida; huwezi kutegemea polisi wachache kulinda kila sehemu.
 
Ulinzi Shirikishi upo kisheria mkuu wangu
Acha uongo, nipe vifungu vyake vya kisheria na kumbuka Mwendazake aliuua huu ili apate kufanikisha alichokitaka,usalama na wajibu wa jeshi la polisi kisheria sio raia, hizi CPF ni za kujitolea sio lazima, tumekosea wapi kama nchi?
Imekuwa kama lazima.
Nilisikia fununu huku mtaani kwetu eti usipoenda kulinda unalipa elfu kumi.
Tumeruhusu maisha yetu yaamuliwe na politicians na chawa wao...police state
 
Back
Top Bottom