Ndugu zangu, bila kufumua mfumo wa kusuka kila kitu upya ni bure kabisa. Tungekuwa tumerudisha madaraka na maamuzi kwa wananchi haya mambo yanafanywa kimkoa au kiwilaya kwa kutumia viongozi halali waliochaguliwa na wananchi na siyo hivi vyangudoa. Wananchi wangewawajibisha viongozi wao kama wanaona wanalegalega na usalama unakuwa wa mashaka. Hata kama ni kuajiri local security gurds ingekuwa rahisi kwani kila sehemu ingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato na kuwalipa. Hawa washenzi wameshatuona sisi ni mazuzu ndiyo maana wanatoa amri za kijinga kama hizi. Unawezaje kumwambia dereva au mfanyakazi yoyote akeshe akilinda wakati kesho yake anatakiwa kazini na kodi analipa? Hizo kodi zinaenda wapi?