DC Jokate Mwegelo atoa siku saba kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao

Yani nilinde sungusungu
Una utani wewe
 
Maswali ambayo DC alipaswa kuwauliza polisi:
1. Je walikuwa na taarifa za tukio?
2. Hizo taarifa walipata saa ngapi?
3. Je wananchi wana namba za simu za polisi?
4. Na kama hawana, wamefanya juhudi gani kuhakikisha wanazo?
5. Walifika kwenye eneo la tukio saa ngapi?
6. Kwa nini walifika muda huo na sio mapema zaidi?
7. Wana rejista ya taarifa wanazopata kuhusu matukio?
8. Je wanafanya doria? Kama hawafanyi, kwa nini hawafanyi?
Na akumbuke kuwa ulinzi shirikishi maana yake raia wanashirikiana na polisi. Hii ina maana wanakuwa na polisi wanapofanya doria ili kuhakikisha GPO inafuatwa. Vigilantes ni watu hatari, wakiachiwa peke yao watadhuru sana watu.

Amandla...
 
Ulinzi shirikishi ni hiari asilazimishe
Kama anataka ulazima waweke taa mitaa yote na cctv kwa hela za walipa kodi maana mmetukamua kila kona

Police patrol ni kazi yao kutulinda na mabunduki yao ama watulipe na bunduki wagawe (hapo nimeongea kama akili zao)
 
Bas lifumuliwe tuajiriwe wananchi
 
Unadhani polisi wapo wengi wa kutosha kulinda kila mtaa?

Isitoshe suala la usalama/ulinzi huanzia kwa mtu binafsi.

Kama hutaki kuchangia ulinzi wako binafsi shauri yako.
Kwa hiyo kama hawatoshi serikali haina plani zaidi ya kuwapa wananchi kazi? Je silaha tunapewa ama?
 
Ulinzi Shirikishi upo kisheria mkuu wangu
 
Vibaka wengi ni watoto wa hawa hawa viongozi ambao walikataa shule wenyewe.
 
Wakati wa jpm polisi walikuwa wangapi ? tumia akili kufikiri acha kutumia kijambio kufikiri
 
Unadhani polisi wapo wengi wa kutosha kulinda kila mtaa?

Isitoshe suala la usalama/ulinzi huanzia kwa mtu binafsi.

Kama hutaki kuchangia ulinzi wako binafsi shauri yako.
Wapo mbona wanapotaka kupiga watu virungu wanatoa lesho kuwa Askari mmoja anaweza kushugurikia watu 100, kwani hao vibaka ni wangapi? kipindi cha Magufuri walifanyaje mpaka hao panya wakakomeshwa, kingine Samia ndiye ameongeza hao vibaka, kufukuza machinga mtaani kumefanya vibaka kuongezeka maana wengine walikuwa wamejiajili kwa njia ya umachinga, Sasahivi Samia kawafukuza wote,unafikiri wataishije wasipo kaba watu?
 
Polisi wanataka kusukumia jikumu lao kwa raia wasio na ujuzi wala silaha.
Nashauri wale polisi wakali sana Kingai, Mahita, Goodluck na Jumanne wapelekwe Temeke wakapambane na panya road
 
Macho mawili ya picha ya pili yanatosha kabisa kufanya huo ulinzi
 
"Yaani nikeshe usiku nazunguka mitaani na rungu bila malipo halafu kesho yake niende ofisini kwangu?"
[emoji23][emoji23][emoji119][emoji23][emoji119]
 
Imekuwa kama lazima.
Nilisikia fununu huku mtaani kwetu eti usipoenda kulinda unalipa elfu kumi.
 
Huyu DC sijajua ni kipi ataweza kufanikisha!! Kama kazi inamlemea Kwa Huruma zake, Fikiria unatoka Dar kwenda Mkuranga unakaa Mbagala masaa mawili Kwa foleni, sababu DC ameshindwa kupanga wafanya biashara!! Haoni huruma Kwa watu wanavyopotezewa muda!? Lile tatizo la Mbagala halihusiani na ujenzi WA barabara ila kukosa ufuatiliaji WA DC,
 
Wakati wa jpm polisi walikuwa wangapi ? tumia akili kufikiri acha kutumia kijambio kufikiri
Hivi huwezi kujibu hoja kwa ustaarabu bila kutukana? Kuna sehemu yoyote kwenye hoja yangu nimetukana? Anyway nimesamehe. Acha maisha yaendelee
 
Ulinzi shirikishi ni jambo la kawaida; huwezi kutegemea polisi wachache kulinda kila sehemu.
 
Ulinzi Shirikishi upo kisheria mkuu wangu
Acha uongo, nipe vifungu vyake vya kisheria na kumbuka Mwendazake aliuua huu ili apate kufanikisha alichokitaka,usalama na wajibu wa jeshi la polisi kisheria sio raia, hizi CPF ni za kujitolea sio lazima, tumekosea wapi kama nchi?
Imekuwa kama lazima.
Nilisikia fununu huku mtaani kwetu eti usipoenda kulinda unalipa elfu kumi.
Tumeruhusu maisha yetu yaamuliwe na politicians na chawa wao...police state
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…