Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."

Pia soma:

Attachments

  • 5693904-733139b74b770431863bceb3e11f571f.mp4
    2.3 MB
Sasa ni kwanini wamemtumbua Nape ambaye na yeye alisema UKWELI kama huuhuu!!🤔
Na ni kwanini wanaanza kusema ukweli kipindi hiki tena bila kuulizwa?
Au ndo ukweli wa ule msemo, " karma never forget your address" inakurudia tu hata kama ni baada ya miaka 100!
 
Huyu ni sawa na alivyoropoka Nape tu, hakuwa na nia njema ila kadukuliwa kwa Bahati mbaya
Very true ,Kuna madiwani watakua walichukizwa maana sio kwa kujimwambafy huko anawafokea Kama watoto kwamba bila ya yeye na hisani ya CCM madiwani si chochote

Ndio maana kwenye viapo huwaga wanasema NTATUNZA SIRI NA SITO TOA SIRI ZA SERIKALI
 
Najaribu kuwaza aliechomesha hiyo video na kutoa nnje maneno ya humo kikaoni.

Muogope sana mwanadamu Mnafki anaekuchekea chekea.

Washamchomesha mwenzao tayari.
 
Very true ,Kuna madiwani watakua walichukizwa maana sio kwa kujimwambafy huko anawafokea Kama watoto kwamba bila ya yeye na hisani ya CCM madiwani si chochote

Ndio maana kwenye viapo huwaga wanasema NTATUNZA SIRI NA SITO TOA SIRI ZA SERIKALI
Bila DC, DED na DSO sidhani kama Kuna Diwani wa ccm anaweza kushinda. Hata DC kasema ukweli kama ulivyo.
 
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."

Pia soma:

Luka 12:2-4

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
 
Ni vyema mkawa na Umoja wa kutetea maslahi yenu mbali na Vyama vyenu. Mmedhalilishwa vya kutosha. Umoja ndo silaha yenu
 
Kule kuvalishwa majoho!!. Hadi leo unajua maana yake..?
 
Back
Top Bottom