LGE2024 DC Malinyi, Waryuba awahakikishia wananchi Usalama na Amani kipindi cha Uchaguzi

LGE2024 DC Malinyi, Waryuba awahakikishia wananchi Usalama na Amani kipindi cha Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba ameyasema hayo wakati aliposhiriki uchaguzi marathoni Wilayani Malinyi kwa lengo la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura Novemba 27, 2024.
IMG_0887.jpeg

DC Waryuba amesema kuwa huu ni wakati sahihi kwa wananchi kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba kushiriki kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
IMG_0885.jpeg

Naye Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Malinyi, Ndugu Khamis Jaaphar Katimba amesema matarajio yake ni kuhakiksha kuwa asilimia 90 ya waliojiandikisha wanapiga kura.

Hata hivyo kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Malinyi Ndugu Abdulrahim Hamid amesema kuwa jukumu walilonalo Wananchi ifikapo tarehe 27 Novemba, ni kuhakikisha wanafanya maamuzi sahihi ya kuchagua chama kitakachopeleka mbele maendeleo ya Wananchi
IMG_0884.jpeg

IMG_0886.jpeg
 
Back
Top Bottom