DC Meatu: TAKUKURU inachunguza tuhuma za Watumishi waliochukua fedha za michango ya Wananchi kujenga Shule

DC Meatu: TAKUKURU inachunguza tuhuma za Watumishi waliochukua fedha za michango ya Wananchi kujenga Shule

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa Kata ya Kabondo Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu kuomba Serikali kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa kufuatilia madai ya ‘upigaji’ wa fedha za Wananchi uliotokea katika Kata hiyo, suala hilo limetolewa ufafanuzi.

Kusoma zaidi hoja hiyo, bonyeza hapa ~ Kata ya Kabondo (Simiyu) tulichanga Tsh. 30m Ujenzi wa Sekondari, Akaunti ya Benki imebaki na Tsh Laki 5 na ujenzi ni 0%

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura anafafanua madai hayo kuwa Wananchi walichangisha Tsh. Milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari kisha mradi kutofanyika:

Hilo suala nalifahamu ila hoja iliyoandikwa kuhusu kiasi cha fedha kilichokusanywa kilikuwa kama Sh milioni 16, mpango ilikuwa kujenga madarasa mawili na jengo la Walimu katikati.

Tunazo taarifa ya idadi ya kaya zilizochanga na zilizotoa nusu, niliagiza TAKUKURU wakafanye kazi ya uchunguzi.

Ilionekana pia kuna fedha walikuwa wanalipwa Wajumbe ili wasimamie, tuliagiza zirudishwe, jumla ya Tsh laki nane zimerudishwa, hilo lilisimamiwa na ofisi ya OCD.

Hela yetu imerejeshwa kwa makusudi ya kuendelea na mradi, Mkurugenzi tumemuagiza achukue hatua kwa Watumishi wake wa ngazi ya Kata kwa kuwa ndio mamlaka yake ya nidhamu.

Upande wa ujenzi umeanza na sasa umefikia ngazi ya renta lakini TAKUKURU nao wanaendelea na kazi yao.

Halmashauri imeshatoa hela kwa ajili ya kusaidia finishing ya huo mradi.
 
Back
Top Bottom