Wewe unadhani kwenda chato yeye kama marehemu kunamsaidia nini?
Au hiyo heshima yeye kama marehemu inamsaidia nini?
Watu wameacha hata kutembelea kaburi la nyerere kinachosaidia tu ni kwamba siku aliyokufa ni siku ya kitaifa.
Hivi wakati nyerere anakufa ulikuwa ushazaliwa au ushajitambua? Kama ulikuwa tayari basi utaelewa kuwa hata hili la magu ni kawaida na kitapita tu.
Maisha lazima yaendelee resources za nchi hii zielekezwe kutatua changamoto za walio hai.
Nchi zinazoendelea hasa kusini mwa jangwa la sahara tuko busy sana na siasa na mambo ambayo hayana tija kwa jamii. Tuko busy sana na kulinda wapiga kura, public holidays, uchawa, kujipendekeza, kupeana vyeo, na wizi wizi kuliko kufanya mambo ya maana.